Raia wa Botswana afungwa miaka mitatu kwa kuishi nchini kinyemela

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,474
8,323
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemuhukumu raia wa Botswana, Theo Leborang kulipa faini ya Sh1 milioni au kwenda kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuishi nchini kinyume cha sheria na kutoa taarifa za uongo kwa Maofisa wa Uhamiaji.

Hukumu hiyo imetolewa jana Jumanne Januari 11, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu, Francis Mhina baada ya kukiri kosa linalomkabili.

Hakimu Mhina alisema mshtakiwa alikiri kosa lake hivyo Mahakama hiyo inamtia hatiani kwa shitaka linalomkabili.

Mhina alisema kwa kuwa mshtakiwa amekiri kosa lake hivyo Mahakama hiyo inamuhukumu kulipia faini ya Sh 1 milioni au kwenda jela kifungo cha miaka mitatu.

Awali, akisoma hoja za awali Wakili wa Serikali, Hadija Masoud alieleza Januari 6, 2023 mshtakiwa huyo akiwa raia wa Bostwana alikamatwa katika eneo la Posta one stop akiishi nchini bila ya kuwa na kibali cha kuishi nchini

Hadija alidai mshtakiwa huyo anamiliki hati ya kusafiria yenye namba BN0258427 iliyotolewa nchini Botswana ambayo imekwisha muda wake.

Katika shitaka la pili, alidai Januari 6, 2023 katika eneo la Posta one stop, Theo alitoa taarifa za uongo kuhusu utaifa wake kwa nia ya kujipatia kitambulisho cha utaifa kwa kujaza fomu namba 111011401202301050026 huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Alidai Theo alikamatwa na kufanyiwa mahojiano na alikiri alitoa taarifa za uongo yeya siyo raia wa Tanzania ni raia wa Botswana.
Hadija baada ya kumsomea maelezo ya awali aliiomba Mahakama hiyo itoe adhabu Kali ili owe fundisho kwa wengine.

"Hatuna kumbukumbu yeyote ya mshtakiwa kutenda makosa na ninaiomba mahakama hili itoe hukumu kwa mujibu wa sheria,"alidai Hadija

Akitoa utetezi wake mahakamani hapo, Theo aliiomba mahakama hiyo imsamehe kwa kuwa alidanganywa afanye hivyo itamsaidia yeye kupata uhalali wa kuendelea kuishi nchini bila kwenda katika ofisi za uhamiaji.

MWANANCHI
 
Nchi imekuwa shamba la Bibi kweli kweli. Uhamiaji pitieni kwenye viwanda vya wahindi, wachina Waarabu na wapakstani, huko kuna wageni kibao wanaofanya kazi bila vibali. Yani mtu anakuwa na visitors visa lakini anafanya chochote atakacho what a shame.
 
Wamwachie tuu,afu tuachane na mipaka ya wakoloni,kila mtu awe huru kwenda popote ndani ya Afrika kujitafutia mkate wa kila siku.
 
Mnaosapoti ni vile hii amani inawazuzua ila kumbukeni kuna vijana wenzetu wanakesha kuilinda hii amani ambayo mnataka ipotee kisa huruma zisizo na msingi,
Kusiwe na mipaka!!!
Watz hawalioni hilo..... Mtu anatafuta mpaka NIC Sasa huyo ni mtu mwema. Na Kwa mazingira ya Botswana na Tz siyo rahisi kupang'ang'ania huenda ni mamuluki. Ooooooooooooh
 
Nchi imekuwa shamba la Bibi kweli kweli. Uhamiaji pitieni kwenye viwanda vya wahindi, wachina Waarabu na wapakstani, huko kuna wageni kibao wanaofanya kazi bila vibali. Yani mtu anakuwa na visitors visa lakini anafanya chochote atakacho what a shame.
Wacha fitna wewe.Unachosema si kweli na unawatukana uhamiaji bure.
 
Watz hawalioni hilo..... Mtu anatafuta mpaka NIC Sasa huyo ni mtu mwema. Na Kwa mazingira ya Botswana na Tz siyo rahisi kupang'ang'ania huenda ni mamuluki. Ooooooooooooh
Huko Botswana pamoja na sifa unazozijua binadamu wana vionjo tofauti si kila mmoja ni kula tu.Huenda kuna vitu kwa yeye kaona Tanzania panamfaa zaidi.Akilipa hizo 1000.000 Apewe fursa aishi nchini bila shida.
 
Huko Botswana pamoja na sifa unazozijua binadamu wana vionjo tofauti si kila mmoja ni kula tu.Huenda kuna vitu kwa yeye kaona Tanzania panamfaa zaidi.
Ndio aishi nchi ya watu kinyemela!?
Utamjuaje kama ni muaminifu je kama ni jambazi limetoroka huko kwao
 
Watz hawalioni hilo..... Mtu anatafuta mpaka NIC Sasa huyo ni mtu mwema. Na Kwa mazingira ya Botswana na Tz siyo rahisi kupang'ang'ania huenda ni mamuluki. Ooooooooooooh
Hawezi kua mwema,
Baada ya muda anakaribisha kigroup chake cha Human trafficking aanze kuuza ndugu zetu kama njugu.
 
Akilipa ana rejeshwa kwao, akienda jela, kifungo kikiisha ni kwao na anaweza zuiliwa kuingia kwa muda fulani

Ndio maana ukienda ubalozini kutoa taarifa za uongo una pigwa zuio la kuingia nchini kwao

Yule muiran amerejeshwa kwao, wapo wengi pia walio pewa zuio kutoka mataifa makubwa (donor countries)
 
Binadamu wote ni ndugu zangu Afrika ni moja.

Nachukizwa sana na mipaka ya Afrika.
Mimi nilikua nagoma kutoa rushwa pale Chirundu border ili kulipa eti upite Watanzania wengi kwa uoga wao walikuwa wanaweka hela rand 100 mpaka 200 hapo Messina kwenyewe wananijua siwezi kutoa rushwa kupita Afrika kwa ramani za Wazungu...
 
Kabisa mkuu,
Ndio maana kanuni ya TANU ilisema 'binadamu wote ni ndugu zangu... Afrika ni moja'

Tunapaswa kuungana kuachana na mamipaka ya wakoloni.
 
Back
Top Bottom