Raia Mwema na JamiiForums wanapotosha?

Aliyosema yote ni kweli kwani hata humu JF kuna watu kazi yao ni kutukana tuu kama mtu atatoa hoja ya kuipinga chadema na wahusika wala hawachukui hatua za dhati kwa watu hao(wengi waliofungiwa ni wale walioisema vibaya chadema au wanaochafuana wao kwa wao)na utaona hata post zinazohusu kupiga debe chadema zinashabikiwa sana kuliko zile zinazoipinga chadema.Kwakweli hapa sasa pamekuwa ni kijiwe cha baadhi ya watu wasio na utaifa ambao kazi yao ni kubomoa tuu.

Pamoja na yote hayo wakae wakijua mwenye mbili havai moja hivyo ccm ushindi kama kazi kwa njia yoyote ile,narudia kwa njia yoyote ile huyo mtu wao wanaomtakasa hatapata hata 13% ya kura zote,kaeni mkisubiri ila mjue Utaifa kwanza na utashi wa vyama baadae kwani baada ya uchaguzi tunarudi wote pamoja.

Elimikeni jamani!

Mimi nashindwa kuelewa huyo mwana diplomasia, kwake ukweli ni nini? je mtu akisema JK ameshindwa kazi, kwa nini yeye hafafanui jinsi jk alivyofanikiwa? Badala ya kujadili hoja anajadili watu. Mwana diplomasia gani huyo? tutajie jina lake
 
Si mmeona wenyewe jinsi hawa jamaa wanavyotukana!


Habari ndiyo hiyo. Watanzania siku hizi hawataki kusoma habari za hovyohovyo. Wataandika Mtanzania, uhuru, Sinavyeti, Cheza REDE, TBC1, Uhuru, Mtanzania. Hayo magazeti siku hizi watu wanavutia tumbaku tu na kufungia maandazi na kuendea ile ''ofisi kuu''. Watu wanayapita kama hawayaoni. Wananunua magazeti lulu kama Raia Mwema, Mwanahalisi, Mwananchi na kuyaweka kwenye maktaba zao na hapa JF wanachambua wenyewe- habari za hovyo wanaflushi. Hujaelewa tu wewe wa udaku -Mbea.
 
Hivi na wewe una ubongo wowote unaokuweka katika kundi la watu makini.

Mtu wa ovyo, huandika ovyo; anastahili jibu la ovyo.

This thread was removed, edited then brought back, for starters, even the title is not what i had originally. This is the title i had on the initial thread:
UPOTOSHAJI WA RAIA MWEMA NA JAMII FORUMS. It has been changed into:
Raia Mwema na JamiiForums wanapotosha?
 
This thread was removed, edited then brought back, for starters, even the title is not what i had originally. This is the title i had on the initial thread:
UPOTOSHAJI WA RAIA MWEMA NA JAMII FORUMS. It has been changed into:
Raia Mwema na JamiiForums wanapotosha?

Nilijibu hiyo thread kwa bahati mbaya kwa jina la mtu mwingine - MIKOLE. Kuna mtu alisahau to log out where i am.
 
Nilijibu hiyo thread kwa bahati mbaya kwa jina la mtu mwingine - MIKOLE. Kuna mtu alisahau to log out where i am.

ha ha ha ha ha .. mchambuzi umepatikana leo ... ha ha ha ha ha ha ha hahaha ha ha na mi-id kibao. Mzee mzima chalii
 
Nilijibu hiyo thread kwa bahati mbaya kwa jina la mtu mwingine - MIKOLE. Kuna mtu alisahau to log out where i am.
Hahaha, you don't say.

Mchambuzi hiyo mitandao mingine uliyoitaja wanaendesha kura za maoni na kama JF/Raia Mwema wanapotosha mtandao upi uko sahihi?
 
I agree with Mchambuzi, nimevote mara 10 kule kwa mwananchi...
Wewe tunakujua umezoea wizi tu,. hata 31 October umejiandaa na umeandaliwa na mabwana zako upige kura mara 10!! ona aibu na uwe mzalendo upige kura mara moja na ukubali kushindwa wala usichakachue kura zetu.
Waweza pia kuijenga nchi ukiwa upinzani kwa kuwakosoa walioko madarakani! CHADEMA watakapokuwa wameshika Dola, watakubali kukosolewa na kwa pamoja tutaijenga nchi. hatutawabagua wala kuwanyanyapaa wapinzani
 
Habari kwa hisani ya Said kinyozi(0716-679116) na Ahmad Mikole(0772-235918)

[I]MWANADIPLOMASIA NGULI NCHINI ATOA KARIPIO KALI KWA RAI MWEMA, MWANAHALISI, JAMII FORUMS[/I]

Lile sakata la vyombo vya habari kutumiwa na wanasiasa kwaajili ya kueneza propaganda za vyama limezidi kushika kasi baada ya leo hii mida ya saa nane mchana msasani jijini Dar es salaam mwanadiplomasia nguli ambaye ana uzoefu wa siku nyingi katika maswala ya kitaifa na kimataifa kuweka wazi kuwa kuna waandishi ambao ni dhahiri kuwa kazi imeanza kuwashinda kwa kuvunja viapo vya taaluma yao na kuanza kutumika kama vyombo vya propaganda vya baadhi ya vyama vya siasa.

SASA HAWA HAWAKUONA DAILY NEWS.......... TOA MAONI JAMAN
Mwanadiplomasia huyo ambaye ameijengea jina Tanzania kutokana na uwajibikaji wake uliotukuka kimataifa alionyesha dhahiri kukerwa na vyombo hivyo vya habari. Huku mkononi akiwa na gazeti la Raia Mwema ambalo linaongozwa na Saed Kubenea na gazeti la Raia Mwema ambalo linaongozwa na Jenerali Ulimwengu ambayo yote hutolewa siku ya jumatano ,gwiji huyo aliyebobea katika mahusiano ya kimataifa anawataja waandishi Johnson Mbwambo,Lula wa Ndali Mwananzela, Godfrey Dilunga na Mwandishi anayetumia jina bandia la msomaji raia ambao wote ni waandishi wa Raia Mwema kuwa waandishi hao hawana hata chembe ya utaifa wala uzalendo kwa maana habari zao zimejikita kwenye kubomoa chama Fulani na kujenga kingine hakuishia hapo alimtaja pia Evarist Chalali ambaye anaishi uingereza kwa kusema kuwa huyu hana nia njema na Tanzania kwani habari zake zinazochapwa kwenye Raia Mwema zina harufu ya uchochezi.

Mwanadiplomasia huyo akiongea kwa masikitiko makubwa alisema waandishi hawa ambao amewataja kuwa wamesahau misingi na kanuni ya uanahabari badala yake kwa staili ya kujadili kwao hoja wamejipambanua kuwa ni wapiga debe wa CHADEMA na Dr slaa huku wao wakiendeleza wakiwaghilibu wasomaji wao kuwa wao ni neutral na hawaegemei upande wowote.

Kwa upande wa Mw3anahalisi mwanadiplomasia huyo anamtaja Saed Kubenea kuwa anataka kujitafutia umaarufu baada ya umaarufu wake kuporomoka kwa kasi ya ajabu na kiwango cha kutisha baada ya watanzania kubaini kuwa habari za gazeti lake la Mwanahalisi nyingi ni za kutengenezwa kutoka redio mbao na ndio sababu kwenye machapisho mbalimbali ya gazeti hilo waandishi huwa hawatajwi badala yake wasomaji wanafanyiwa danganya toto kwa kuandikiwa Na Mwandishi wetu, vilevile anawataja Ndimara Tegambwage ,Joster Mwangulumbi, Mwanakijiji na Ezekiel Kamwaga kuwa wana uandishi mtindo jazba kwani hushindwa kupangilia hoja zao ipasavyo na mara zote hongelea mambo mabaya tu na kamwe hawaandiki kuhusu mema………….. labda tuwaulize wanafanya hivi kwa faida ya nani? anahoji gwiji huyo. Mwanadiplomasia huyo anaenda mbele Zaidi na kuweka wazi kuwa anasikitishwa sana na tabia ya magazeti hayo kujinadi na habari zinazokwenda na vichwa vya habari Na Mwandishi Wetu ambazo mara nyingi huwa ni tetesi zisizo na kichwa wala miguu anatanabaisha gwiji huyo.

Gwiji huyo anatoa karipio pia kwa Jamii Forums kwa kusema kuwa hawapawsi kujiita Jamii Forums badala yake wajiite CHADEMA Forums kwani hoja zinazojadiliwa kwenye mtandao huo hazina hata chembe ya utaifa bali ni matusi kwa serikali na ni kama wimbi la propaganda chafu zinazoendeshwa na CHADEMA.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa mwanadiplomasia huyo anasema vichwa vya habari kama …………Laiti CCM ingetenda ya Nyerere japo robot u……………iliyoandikwa na Johnson Mbwambo kwenye gazeti la Raia Mwema la leo haina tafsiri nyingine ya kifalsafa bali kupandikiza chuki dhidi ya CCM ambacho ni chama kinachoongoza serikali kwaq sasa.

Mwanataaluma huyo aliyebobea katika diplomasia anaweka wazi kuwa waandishi wa habari ni mhimili wa nne wa jamii yoyote duniani lakini ni mhimili wa kwanza wa kujenga taifa lolote duniani hivyo wanahabari wasikubali kutumika kueneza propaganda za vyama vya siasa badala yake wajikite kwenye kuibua hoja za kujenga taifa pia waandike habari za kitafiti ambazo zitasaidia watanzania kujiletea maendeleo na mwishowe amewaasa watanzania kuwapuuza watu hao ambao amesema hawana hadhi ya kusikilizwa kwani wamedhihirisha kuwa hoja zao ni za kubomoa sio kujenga na hawana hata chembe ya uzalendo wala utaifa.
 
Sidhani kuna sababu ya kuhangaisha vichwa vyetu na huyo anayetajwa kama ''mwanadiplomasia nguli'' maana hao ndio chanzo cha matatizo lukuki tuliyo nayo. Hatujawahi ona wakitumia uzoefu wao au hiyo misifa wanayoitaka, yametokea mengi na yataendelea kutokea mengi, wamebaki kuyaangalia matumbo yao. Tumeshuhudia uhuni wa ajabu toka Daily News, je alikuwa msalani nini na sasa ndio ametoka, watuache, hizo za kuokotana na baadaye kuitana balozi zimepitwa na wakati, Africa itajengwa na waafrica wenyewe na hivyo hivyo kwa Tanzania, sasa wabomozi kama yeye wakajifie!! Amesikia hao waliofundisha hiyo mizezeta kukata watu mapanga na wapumbavu wanaibuka na kusema ni ukakamavu je hajaliona hilo, akumbuke kuna kitu kinaitwa freedom of expression, na mbaya zaidi hapa tena si freedom bali watu ni kama wanareport, maana mauzauza yao yamejaa!!
 
Sasa mbona huyo mwanadiplomasia aliyebobea jina lake limeachwa kapuni? Anaogopa kivuli chake?
 
nashangaaaaaaaaaa pia .... kaz kubwa ni kupiga kura ni bora tuache kuumiza vichwa na hao ambao hawana cha maana cha kusema
 
Ana bahati hakutajwa jina lake maana watu WANGEMLA MZIMAMZIMA.

Wee Nguli, naona umekuwa tayari OLD SCHOOL. Heri ukae pembeni na tutakuwa tukichota busara zako (kama unazo) na kuchukua SAMPLING kwa vibao vipya. Hata sisi siku tukifa, Tanzania bado itaendelea, sembuse nyie????
 
https://jamii.app/JFUserGuide you mwanadipromasia..sorry Mod usinifungie ila kaniudhi huyu...TUMECHOKA NA CCM, https://jamii.app/JFUserGuide YOU MWANADIPLOMASIA....
 
Mwanadiplomasia nguli, aliyebobea etc. Nguli kwa lipi? Amebobea kwa lipi? Ni mara ngapi magazeti ya mtanzania na Rai yamemtukana Slaa waziwazi na hakuna hata mtu mmoja alinyanyua mdomo kukemea? Ni mara ngapi magazeti ya uhuru yameandika habari za uongo kuhusu Slaa, yakisema ametumwa na kanisa, mara alishindwa upadri na vitu kama hivyo, huyo nguli alikuwa wapi? Au unguli umeanza leo baada ya kuona kitumbua kinataka kuponyoka mdomoni? Hawa ndiyo wachumia tumbo, njaa zinawasumbua.
 
aah nyie mnapoteza muda huyo siyo mwanadiplomasia wala nini, ni kada wa sisi m
hebu angalieni kwanza website yenyewe ni ya sisi m. angalia http://www.novadream.blog.com . Kwani kuna gazeti linaloongoza kwa kuandika habari za uchochezi kama gazeti la Uhuru na Mzalendo? vipi alikuwa nayo pia?

Je huyo mtu nguli asiye na jina anaweza akajilinganisha na watu wanao andika vitabu mpaka vikatumika kwenye mitaala ya shule kama Ndimara?

Jamaa wamechoka hata hawaelewi cha kuandika, mkuu naye ameamua kutunga lake " Eti watu wanataka kuingia magogoni huku wakiwa wameshika maiti" haha hah .

Hofu mchezo kuondoka feri ni noma pale kuna harufu nzuri n.k

Na watoto wa Shk. yahaya wanapitia pale pale!
 
Aisee
nimeitembelea hiyo source. jamaa hata heading zao zinakufanya ulie maana hawajui hata nini wanaandika.
Unakuta post kibao lakini comment ni moja tu ambayo inatolewa na mwenye blogu. na nimechunguza nimegundua kwamba mwenye blogu anapost humo kwa majina tofauti maana aina ya uandishi wake haina tofauti na hao news posters wake.

Nadhani alipewa hela na ccm akaaendeleze blog ya kufagilia chama tawala.
Msipoteze muda kujadili hii hoja maana hainamashiko wala reliable source. Wala hayupo huyo mwanadiplomasia Nguli wanayemsema. wala hakuna mazingira ya kuhojiana wala kupeana briefings. Halafu huko msasani wanakokutaja wanajenga chati tu la kufikirika. naamini hii story waliiandaa viunga vya manzese kwenye net cafe. na wameshavuta mkwanja.

Naongezea kusema kwamba. juko kwenye blogu yao hakuna chama chochote kinachotajwa against zaidi ya CHADEMA. yaani jamaa ni wa kupuuzwa big time
 
Back
Top Bottom