Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,193
- 3,011
Nimekuwa nikifuatilia huu mjadala tangu mwanzo lakini kwa kifupi ni kuwa kilichoandikwa na mchambuzi aliyetuma thread hii ni wazi kuwa kinauhalisia na kimethibitishwa kwa mifano halisi aliyoitoa katika thread yake lakini pia upotopoto wa majibu na hoja zilizofuata katika kujaribu kuipinga na kuikanusha hoja hiyo ya msingi nao ni mfano mwingine kuwa msingi wa hoja za ALPHA ni imara sana. Inasikitisha kuona kuwa kwa kiasi kikubwa wachangiaji wa hoja hii ambao ni contemporary great thinkers of TZ..,bado wanaususuwavi wa fikra na ugubugubu wa mawazo. Sijui inahitajika lugha gani isemwe ili watu wafahamu kuwa hoja inajibiwa kwa hoja..,lakini ni kwa bahati mbaya kubwa iliyopo kwa great thinkers wa "jamiiyetu" kujibu hoja kwa porojo kisha kujinadi kuwa porojo zao zinanguvu kuliko hoja.
Na wewe uliye great thinker kuliko wengine, hoja hapa ni IPI?