Raia Mwema na JamiiForums wanapotosha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raia Mwema na JamiiForums wanapotosha?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mchambuzi, Oct 12, 2010.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu wanajamiiforums, ningependa to share article ifuatayo na natarajia kwamba since we dare to talk openly, hatutaone ikifutwa au wanachama wa jamiiforums kama mimi kuwa suspended kwa madhumuni ya kulindana na kufichana. Jamiiforums Oyee! Enjoy.
  ___________________________________________________________________________________

  UPOFU WA GAZETI LA RAIA MWEMA NA YALIYOJIFICHA KUHUSU KURA ZA MAONI KATIKA TOVUTI YA JAMII FORUMS.

  Tarehe 22/09/2010 gazeti la Raia Mwema lilichapisha habari katika ukurasa wake wa mbele likisema ``wanamtandao wampa slaa 76% ’’ kama mtanzania mtaalamu wa masuala ya mitandao ya kijamii (Social Network) nilifuatilia kwa kina na umakini mkubwa suala hili, na kugundua upotoshwaji wa taarifa hiyo kwa asilimia mia moja.


  Aidha sina hakika kama mhariri wa gazeti hilo ana utaalamu wa teknolojia hii mpya na kama alitambua hili nitakaloandika kabla ya kuchapisha habari hiyo.

  Ninaandika haya kuufahamisha umma wa Tanzania karibu laki nane wanaotumia mtandao na pia wananchi wengi walioamini kazi za gazeti hilo kabla ya ya kuchapisha uozo huu ambao unaweza kutuletea matatizo kwa taifa. sitaki kuamini kwamba mhariri alikuwa na maslahi binafsi katika kuchapisha habari hiyo na pia siamini kwamba gazeti kama hili halina mtaalamu mchambuzi wa habari na taarifa toka mtandaoni.

  UKWELI NA UCHAMBUZI


  kwanza kabisa gazeti limesema wanamtandao wakati habari nzima imezama katika mtandao wa Jamii forum tu na kuacha mitandao mingine kama Wanabidii, wazalendoforum, Issa Michuzi Blog, Mjengwa Blog, na Bongo Celebrity,Haki Ngowi,Mrokim, n.k.

  Aidha takwimu zote ni za tarehe 22/09/2010 siku ambayo gazeti hilo lilichapisha habari hiyo. Jamii forum mpaka tarehe 22/09/2010 ilikuwa na wanachama wapatao 22,032.

  Siku hiyo wakati naandika takwimu hizi watumiaji walikuwa 3,886 kati yao 557 walikuwa wanachama (Members) na 3329 waliobaki walikuwa wageni (Visitors) ambao hawa ni wale watembeleao tovuti bila kuwa wanachama kwa lengo la kusoma kilichopo au kupata taarifa fulani, kati ya hawa wengine huwa ni wanachama ambao hawajaingia kama wanachama kwa muda husika.

  Kwa maana hiyo hapo juu utaona kwamba 14% tu ya watumiaji wa mtandao huu ndio wanachama huku 86% wakiwa ni wageni (hawa huweza kusoma , kupiga kura lakini hawawezi kutoa maoni).
  Kwa undani zaidi kama tarehe 22/09/2010 ni wanachama 557 tu walitumia mtandaohuo , basi ni asilimia 2.64 tu ya wanachama wote ndio watumiaji huku asilimia 97.36 ikiwa ni watumiaji wasio wanachama, tarehe 22/09/2010 washiriki walikuwa wa kura ya maoni walikuwa ya mtandao huo ilikuwa nia washiriki 6,873.

  JAMBO LA MSINGI NI HILI


  Kama 14% tu ya watumiaji ndiyo wanachama basi wanachama walioshiriki kura hiyo ni 985. Kwa maana hiyo basi 86% ya kura zilizobaki yaani 5,888 zilipigwa na wageni, wanachama waliopenda kuingia kama wageni, ili kufanya utaratibu wa kupiga kura mara mbili na kwa kawaida mwanachama hutakiwa apige kura mara moja tu ila ukiwa mgeni unaweza kupiga hata mara mia moja.

  MAANA YAKE


  Kura za maoni mtandaoni zinapimwa ubora wake kwa tofauti kati ya mwanachama wa tovuti husika waliopiga kura na idadi ya kura zilizopigwa . Jinsi tofauti inavokuwa kubwa ndivyo jinsi ubora wake unavyopoteza maana kwa suala hili tofauti ni 5,888 sawa na 86%.

  ANGALIZO

  Je ni kweli gazeti hili linatuchukulia watanzania kuwa ni wajinga kiasi hicho ? kwamba lilitumia ujinga wetu kwa kutuletea habari hii ya upotoshaji ili kutuibia mamilioni ya shilingi kwa nakala tulizonunua siku hiyo? Au wamiliki wake waliamua maksudi kutupotosha ili kubeba chama na mgombea fulani? Gazeti la Raia Mwema lilijiaminisha kwa jamii ya Watanzania kama gazeti la uchambuzi yakinifu , leo linaandika habari zisizo na uchambuzi wa kina kwa maslahi yao binafsi?, bodi ya Raia Mwema imesheheni waandishi wazoefu hili hawakuliona kweli?

  Aidha jamii forum baaada ya kugungua udhaifu uliopo wiki chache zilizopita utaratibu wa kupiga kura hizo ulibadilishwa ambapo sasa ni lazima uwe mwanachama ili ushiriki, hiki ni kiini macho kweli? Na jee zile 5,888 walizopiga wasio wanachama zimefutwa ? watanzania makini tuko macho na wapotoshaji kama hawa .

  Aidha kwenye kitabu kinachoitwa Constructing Public Opinion, How political elites do what they like and why we seem to go along with it by Justin Lewis.

  Chapter 1. Why numbers matters and why we should be suspicious of them, niliisoma na ndipo nilipopatwa na hamu ya kufuatilia habari ya gazeti la Raia Mwema na kura za maoni ya Jamii forum. Cha ajabu hakuna taasisi yoyote ama chama chochote kilichohoji mazingaombwe haya. Tumeshuhudia makala mbali mbali kama jumapili ya mwezi huu ya tarehe 10 ambapo Gazeti la Tanzania Daima lilikuwa na makala zaidi ya nne kuhoji uhalali wa Redet chini ya DR. Bana kutoa takwimu za Uchaguzi na kuonesha nani kaongoza. Redet imepita mikoa 26 ya nchi hii na kuongea na wapiga kura tena ni watu halisi sio pen names kama wa Jamii Forums.

  Binafsi siwezi kuchukua kura za maoni za Jamii forum kama kigezo zipo sababu nyingi za msingi mfano Slaa, Mbowe, Mnyika hadi mzee Mtei ni wanachama waandamizi wa wa Jamii forum kwa maneno mengine jamii forum ni uwanja wao, jukwaa lao la propaganda kwa muda mrefu na wamekuwa wakipata upendeleo wa waziwazi pia kumekuwa na uonevu kwa wanachama watakaoonekana kutomkubali Dr. Slaa na chama chake wanachama hao hufungiwa kama vile, Nostradamus, padre, nassy nakadhalika wanafungiwa hadi baada ya uchaguzi kuisha kwa vile tu hoja zao zinamkera Dr. Slaa au wanachama wake bila sababu maalum.

  Jamii Forums is not a neutral Ground na hakuna Fairness kwa vyama vingine vya Siasa with exceptional of Chadema.

  Aidha kipimo cha kupima kura za maoni zilizipigwa na mtandao huu bado ni kizungumkuti wengi wao wamekuwa wakitumia majina bandia na wengine wana majina zaidi ya kumi ukifuatilia mtiririko wa hoja unatambua kuwa huyu ni mtu mmoja hata kama angetumia majina kumi.

  Pia haijulikani kama watu hawa ni watu halisi mfano utaona majina kama mwanakijiji, nyani ngabu, mswahili, chuma, buguruni kwa mnyamani, Inzi, na mengine kama hayo .

  Gazeti la Raia Mwema kama chombo cha habari kilicho makini hakikustahili kutumia chanzo cha habari zake mfano wa jamii forum kutuletea watanzania.

  ZAIDI


  Unapofanya utafiti ni vyema kuwashirikisha wahusika kama wapiga kura nakadhalika, Raia Mwema wana uhakika na hao waliopiga kura jamii forum kama wana sifa za kupiga kura na wana sifa za kufanya hivyo kwani inaeleweka wazi wengi washiriki wa jamii forum wako nje ya nchi na hasa marekani kwenye miji ya Detroit, Michigan, New York na kadhalika, ili Slaa apate asilimia sabini na sita ni lazima chama chake kiwe na muundo unaoeleweka chenye matawi ya kutosha nchi nzima, sina hakika kama CHADEMA kina matawi ya kutosha Namtumbo, Ruangwa , Nachingwea , Pemba, Masasi na kadhalika .

  Dr. Slaa kama Katibu Mkuu wa Chadema ameyumba sana kusimamia katiba ya Chadema wako wanachama wamevuliwa na kufukuzwa uanachama mbele yake kwa kuonewa, usawa wa mgawanyo wa Viti maalum vyote kulundikwa wa watu wa mkoa mmoja hata watu wa Tarime ambao waliongoza kwa kukipigia kura hawakuambulia kiti cha ubunge wa Viti maalum,kina Kafulila wamefukuzwa kwa vile hawakutakiwa kuwa viongozi,haya yote yametokea mikononi mwa Slaa kama kiongozi na mtendaji mkuu, anapata wapi 76%?kweli hawa Jamii Forums ambao wanajiita Great Thinkers walimtizama Dr. Slaa nje na ndani?Kashindwa kuilinda katiba ndogo ya Chadema ataweza kuilinda katiba kubwa ya nchi yetu?

  Udhaifu wa kiuongozi aliona Slaa kwenye maeneo mengi tukimuacha kwenye maisha yake binafsi amefeli, ameshindwa kuhakikisha kuwa anapatika hata mtu mmoja kwenye viti maalum anayetokea Zanzibar ili kuleta usawa akachukua wote toka Kilimanjaro tena bila kikao chochote cha chama chake zaidi ya kila kiongozi kutaja mtoto wake au ndugu yake,haya ni machache yanaonesha huhitaji kuwa GREAT THINKER kujua Slaa hana uwezo wa kupata 76%.

  Sijawahi kusikia uwepo wa chama hiki sehemu kama Unguja, Chake Chake,Chumbi n.k wakifanya kampeni za urais chama ambacho hakijafika hata Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania kitapata vipi asilimia sabini na sita ya kura za uraisi?, hata wakati wakitafuta mgombea mwenza wa Dr. Slaa huko Zanzibar ni wazi haikuwa kazi rahisi kwao kwani walihangaika sana na kuambulia mhitimu wa darasa la saba, mchuuzi wa samaki wa soko la darajani unguja mheshimiwa Said Mzee, wanapata vipi asilimia sabini na sita.

  Na mwanasiasa nguli

  Crispin Alpha
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hatudanganyiki kura yangu kwa Slaaa!
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nami sidanganyiki na hasa viongozi wa CCM wanapoweweseka na kuwa na vitu vya namna hii ndani ya vichwa vyao
   
 4. Lord

  Lord Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwani kura zote zilipigwa 22/09/2010? Mbona ushahidi wako umeelemea sana tarehe hiyo??? Suala la nani alipiga hiyo kura na status yao admin wa jamiiforums ndo anajua.
   
 5. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  so...??!!
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani hawa jamaa wako so desperate sijawahi kuona CCM ikihaha namna hii!!!!!!!! This tells how JF iko so influential.
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  :A S 112:blah blah CRAP
   
 8. d

  dotto JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hatudanganyikiiiiiii!!
  Hatudanganyikiiiiiii!!
  Hatudanganyikiiiiiii!!
  Hatudanganyikiiiiiii!!
  Hatudanganyikiiiiiii!!
  Hatudanganyikiiiiiii!! Tumesema
  hatudanganyikiiiiiii!! Na tena
  hatudanganyikiiiiiii!!
   
 9. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Ni kwamba nimezuiwa kujibu humu au? my responses do not go through. admin, naomba msaada.
   
 10. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Mwananchi www.mwananchi.co.tz
  Kuongoza Tanzania 2010-2015 kura yako utampa nani?
  Willibrod Slaa - CHADEMA (47) 88.7%
  Jakaya Mrisho Kikwete - CCM (6) 11.3%
  Mutamwega Mugahywa - TLP (0) 0%
  Hashim Rungwe - NCCR-Mageuzi (0) 0%
  Ibrahim Lipumba - CUF (0) 0%


  Number of Voters
  : 53
  First Vote
  : Tuesday, 12 October 2010 11:18
  Last Vote
  : Tuesday, 12 October 2010 13:49


  2. ThisDay www.thisday.co.tz
  Do you approve or disapprove of President Jakaya Kikwete's overall job performance (2005-2010)?

  Approve (7%, 10 votes)

  Disapprove (92%, 124 votes)

  Undecided (1%, 1 votes)
  Total Votes: 135

  3. JamiiForums www.jamiiforums.com
  Jakaya Mrisho Kikwete (CCM) (2,016) 21.93%
  Willibrod Slaa (CHADEMA) (6,308) 68.63%
  Ibrahim Lipumba (CUF) (262) 2.85%
  Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi) (484) 5.27%
  Mutamwega Mugahywa (TLP) 121 1.32%
  Total votes: 9191
   
 11. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Bwana Crispin Alpha: Jifunze na ufuzu Tofauti ya kutizama na kuona!

  Unapo Tizama Uadilifu na Ukamilifu wa Uongozi wa JK Kikwete Unaona nini?

  Unapotizama Uozo wa Uongozi wa CCM dhidi ya Maadili na Taifa Unaona nini?

  Unapoona Kikwete ameingizwa Madarakani kwa Njia za Kihuni za EPA nk ...Niambie umetizama nini?

  So ....Ondoa vihoja vyako visivyogusa issue za kijamii ... na statistics za kipuuzi.. Kabla ya kutetea hoja Tizama na uone unajaribu kutetea nini!!

  Tafakari hoja Hii: Kama Kikwete angedhubutu kumfukuza kazi EL na RA na ma engineer wakuu wa EPA etc ... miaka mitano iliyopita leo ungehitaji kuandika mada uliyoandika...

  Andika mada zenye mantiki kwa jamii na si kupotezea watu muda hapa....!!!

  CCM is corrupt!! ... na hilo halihitaji viji statistics vya kijinga kulikwepa...!!

  Raia Mwema na Jamii Forums ni vyombo madhubuti vya kuulinda Utanzania wa Tanzania na Watanzania wake! Uviheshimu!!!
   
 12. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Mna matatizo ya kuremba upupu..endeleeni salama..
   
 13. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nitumie usemi wa siku hizi: Jamii Forums inatisha!
   
 14. M

  Mugo"The Great" JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 7, 2007
  Messages: 263
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  UKWELI NA UCHAMBUZI
  Aidha takwimu zote ni za tarehe 22/09/2010 siku ambayo gazeti hilo lilichapisha habari hiyo. Jamii forum mpaka tarehe 22/09/2010 ilikuwa na wanachama wapatao 22,032.Siku hiyo wakati naandika takwimu hizi watumiaji walikuwa 3,886 kati yao 557 walikuwa wanachama (Members) na 3329 waliobaki walikuwa wageni (Visitors) ambao hawa ni wale watembeleao tovuti bila kuwa wanachama kwa lengo la kusoma kilichopo au kupata taarifa fulani, kati ya hawa wengine huwa ni wanachama ambao hawajaingia kama wanachama kwa muda husika.

  Kwa maana hiyo hapo juu utaona kwamba 14% tu ya watumiaji wa mtandao huu ndio wanachama huku 86% wakiwa ni wageni (hawa huweza kusoma , kupiga kura lakini hawawezi kutoa maoni). Kwa undani zaidi kama tarehe 22/09/2010 ni wanachama 557 tu walitumia mtandaohuo , basi ni asilimia 2.64 tu ya wanachama wote ndio watumiaji huku asilimia 97.36 ikiwa ni watumiaji wasio wanachama, tarehe 22/09/2010 washiriki walikuwa wa kura ya maoni walikuwa ya mtandao huo ilikuwa nia washiriki 6,873.


  My take:

  Ama kweli Tanzania tumejaliwa wachambuzi wa mambo, lakini bado tu maskini sana nadhani wachambuzi wenyewe ni kama huyu Mchmabuzi aliyeandika hii Article ili kupotosha Watanzania na "kujaribu" kuharibu Credibility ya Raia Mwema.

  I think Mchambuzi huyu ana PhD feki kama ya JK ya uchambuzi ndiyo maana hajui kuwa figure hiyo ya washiriki 6,873 haikupatikana tarehe hiyo bali ni Cumulative.

  Nani amekuambia kuwa asie member anaweza kupiga kura? Mimi nimejaribu kupiga kura bila ku-log in na imenikatalia, kwa hiyo ni wewe unayejaribu kupotosha watu.

  In Short 2010 - HATUDANGANYIKI.
   
 15. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wanajamiiforums, ningependa kuandika machache tu kuhusu upotoshaji mkubwa sana uliofanywa na mwanajamvi mwenzetu katika article yake iliyoko kwenye hili jukwaa. Kwa vile JF tuna dare to talk openly........ jamiiforums oyeee! Enjoy:

  Kwanza mchambuzi kaanza hivi:

  Huu ni uongo uliokithiri, hakuna wakati wowote ambao wanachama wa jamiiforums wamefungiwa eti kwa vile tu wameandika habari dhidi ya ccm. Wanachama hufungiwa wakiwa wamevunja sheria na hii inatokea kwa pande zote (mf .... mpiganaji mwenzangu masanilo sasa hivi amekula kibano cha zaidi ya wiki).

  Pili, thread zinazohamishwa hapa zinatokea pande zote .. kwa maoni yangu ... thread zinazompondea Kikwete zinahamishwa/kufungwa kuliko kawaida (fuatilia malamiko yangu binafsi kwenye jukwaa la malalamiko kama wewe ni member wa JF).

  Nitaacha pumba nyingi za mchambuzi na nitajibu machache, mfano hili:


  Hizo blog alizotaja zote hazina poll, kulikuwa na haja gani ya kutafuta poll kule ambako hakuna poll?

  kwani kuna makosa kuchagua siku moja kati ya 366 za mwaka ... poll ni snap shot ya kinachoendelea katika wakati fulani, hiki ndicho kilitokea.

  Walichoandika Raia mwema si cha uongo ... waliandika ukweli wa polls za jamii forums

  Huu ni uongo mkubwa sana, watumiaji wengi wa jamii forums sasa hivi wako Tanzania, na hata kama hawako tannzania, je ni makosa kupiga kura ya maoni?

  Sasa haya matusi, yaani wewe unajiaona ni bora kuliko wana JF wote? hii mianaccm inauzi kweli.

  poll zote za mtandaoni hata zile za gazeti la serikali zinamwonyesha Slaa akiwa na kura zaidi ya asilimia 75? Unabisha hili pia?

  Mwanasiasa nguli? ......... Bwa ha hahahaaha
   
 16. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145

  I agree with Mchambuzi, nimevote mara 10 kule kwa mwananchi...
   
 17. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sijaona majibu stahili ya post hii.Ukweli ingekuwa wakubwa wa jamii forums watoe majibu ya kina na muafaka.Majibu ya" hatudanganyiki" hayana uzito kwa sababu hayakujibu hoja iliyowekwa mbele yetu.
   
 18. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Afadhali upupu utaoga kuliko kuuumwa na nyoka mwenye sumu!
   
 19. A

  Awo JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Hiyo si sawa na REDET waliohoji wajumbe wa nyumba kumi ambao wote ni CCM?
   
 20. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wewe andika tu kujustify upupu wako na fedha ulizopewa kumuosha JK, ukweli ni kwamaba jamaa hakubaliki wala habebeki!!

  VOTE CCM OUT!!!
   
Loading...