Rafiki yangu nahisi ana matatizo ya akili, haachi tabia ya kucheza cheza hovyo

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
N i aina ya wale watu ambao kitendo ha masikio yao kusikia mziki unakita basi mwili utashawishika kucheza.

ni age mate, ana miaka 31, tunafanyia kazi shirika moja la kiserikali ila yeye alihamishiwa kituo kingine, kwa hio sikua nae karibu kwa mwaka hivi zaidi ya kuwasiliana kwenye simu.

nimekutana nae tena naona tabia yae hajabadilika.

kikweli kucheza kwake hakuwadhuru watu lakini kiheshima inakuwa kama haiendani na umri wake

yaani yeye mkiwa kwenye graduation za wadogo zenu au ndugu akisikia muziki atacheza bila aibu, kanisani akienda nako anacheza sana muziki kuzidi hata wale watu maalum, kukiwa na sherehe atacheza sana, n.k.

kuna yale magari ya matangazo huwa anafungwa spika. we! we! we! yani likipita ni bora umwachie nafasi yake atangulie maana watu wanaweza kudhani wewe na yeye kazi yenu ni wacheza mziki.

hii inaingia hadi ofisini ana mazoea sana ya kucheza. akiamka kidogo tu kujinyoosha lazima acheze cheze, akiinga kwenye gari yake muziki ni lazima, n.k.

Mkiongea kuhusu miradi , yeye anakwambia ana sav pesa au anaweza kuomba mkopo afungue shule ya kucheza, ni mzima kweli huyu?? utapata wapi wateja wa kucheza??

hata watu ofisini wanamjua kwa "yule anaependa kucheza" kama jina limewatoka.

ni kucheza, kucheza, kucheza, dancing/

je kuna watu kama huyu au hii ni special case
 
Je, kucheza huko kunamletea maswaibu ya aina yeyote? Inamvunjia heshima? Inazorotesha ufanisi wake kazini?

Kama kwa namna yeyote haimuathiri basi hana shida. Ndiyo, ni matatizo ya kiakili ambayo kila mmoja wetu anayo kwa kiwango chake.
 
Back
Top Bottom