Rafiki yangu akisikia mziki anaoupenda anaucheza bila kujali eneo, je ni pepo?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
Huyu ni rafiki yangu tangia zamani na mpaka leo tupo karibu, tunafanya nae kazi shirika moja na ni moja ya marafiki zangu wachache ambao tumejuana muda mrefu.

Sasa huyu rafiki yangu anapenda sana muziki kuucheza tangu sekondari, huko chuo ndio kabisa alikuwa mzee wa disco sana, na hata nilipofatilia historia yake hata huko shule ya msingi alikuwa hivi hivi.

Yaani iwe ni barabarani, kwenye hafla, gari la matangazo lipite, iwe ni hafla 9kasoro misiba) n.k Akisikia mziki anaoupenda atacheza tu, Kumzua ni kazi sana.

Pia ukizingatia na umri umeenda saizi ni 31 anaingia kiukweli inakuwa taabu kidogo, Leo tulikuwa tumetoka kazin watu wanne hivi kwenda ofisi ya nje ya mji kidogo kikazi, Tulipofika huko kwenye tulipokelewa vizuri mziki si ukapiga bwana, eh mwenzetu aliona sehemu ambayo tupo nae ni kama hakuna uwazi, alienda mbele nafasi ya wazi kidogo akaanza kujitumbuiza kwa kucheza muziki, kiukweli hata wageni wengine walishangaa, baadhi walikuja kutuuliza kama huyu rafiki yangu anafanya kazi na sisi au tumemleta tu kama afiki.

Kiukweli hadi saa nyingine unaweza kuogopa kutembea nae, maana mnaweza kuwa kwenye shughuli ya heshima kidogo unawaza tu hivi dj akipiga ngoma anazopenda jamaa itakuwaje sasa.

Je, hii ni kawaida?
 
Kila mtu na starehe yake wengine wakiona demu mwenye chura anaweza kuacha hata kula ili mradi amuangalie au akamtongoze.
Nasema mwache acheze muziki kwa kuwa Ni ruksa na kawaida kwenye nchi yetu.

Umesahau wale wabunge la katiba miaka ile walipokata mauno na kutingisha shanga ndani ya ukumbi wa bunge?

Narudia tena mwache rafiki yako afurahie muziki maana maisha ni mafupi sana.!!!
 
Wakati mwingine akicheza, mrekodi kwenye simu yako, halafu tuwekee hiyo clip ili tukuamini kwa 100%
 
Jamaa sio mnafiki, anafanya ile mwili wake unataka na si kuangalia binadamu wa pembeni.Sio kwamba wewe hutaki kucheza ukisikia kamuziki unakokapenda ila kinachokufanya usicheze ni ile watanionaje.
 
Bora yy ana open hisia zake anywhere any time ,kuliko ukawa unataman kitu alafu una ogopa watu watasemaje...
 
Aloo mi hata niwe na Nani...ikipigwa ngoma Kali lazima nitikisike ....ebu fikiria ngoma Kama survivor- ya destiny child...au dude benie man....
 
Inaelekea ni mcheshi sana pia MTU mwenye furaha sema watu wengi huwa tunajizuia kucheza ila tuko kama rafiki yako
Watu wa aina hiyo huwa na maisha marefu sana maana kitu inaitwa stress au magonjwa ya moyo huwa wanayasikia kwa nyie mnaomshangaa... Hakuna kitu bora kwa mwili wa binadamu kama furaha na kujiachia...
 
Back
Top Bottom