Mtoto halali na hela
JF-Expert Member
- Aug 10, 2012
- 54,991
- 54,122
Na demu kaliwa
Tahadhari: Usije kujidhuru au kudhuru mtu mwingine kwa kipande cha nyama ambacho hata ukipewa miaka mia ya kukila, huwezi kukimaliza.Kwanza nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniponya na hili janga weekend iliyopita. Mimi Kama kijana nipende kuwashauri vijana wenzangu kuwa waache pombe japo ni ngumu sana.
Weekend nilikuwa viwanja fulani nikipata K-Vant na kitimoto kwa vile huwa kuna nyingine naacha ndani basi nilikunywa kidogo tu. Halafu nikasepa geto kupiga mdogo mdogo.
Sasa kipindi nafika geto nikashangaa masela niliyopanga nao wanaanza kucheka sana. Nikauliza shida nini? Moja akajibu kwa kejeli sana kuwa unaenda kulewa wakati demu wako analiwa na mshikaji wa hapa hapa. Bila kuhoji nikachukua siraha nikaenda kusimama kwa mlango wa mshikaji. Aisee nikajaribu kufungua but alikuwa kafunga.
Nikampigia Dem sim nikamuulza upo wapi saiv? "Akanijibu kwani wewe inakuhusu nini" duh! Niliumia sana but ningefanyeje? Nikamwandikia sms ya kumtusi akanirudishia inasema "unalazimisha mapenzi na Mimi sikupendi" Niliumia.
Basi nikapiga fujo pale mpaka watu wakajaa make mtaa wetu Ni Kama uswahilini vile. Wakanishauri mpaka nikatupa zile siraha nilizokuwa nimeshikilia. Ilikuwa kisu, rungu na panga. Aisee baada ya kuzitupa msikaji katoka anajiropokesha na Mimi nilikuwa tungu sana. Nilimuotea ngumi ya shavu mpaka nikaona anatema memo. Akanikaba mpaka chini make nilikuwa nimekunywa pombe nyingi sana. Nikaona anaweza kunioshea sana nikabahatisha nyama ya kung'ata bana aise nimemng'ata mpaka nikatoa nyama.
Vita ilikuwa Kali sana ila sikuumia hata kidogo lkn mpinzani wangu nimemjeruhi sana sana nilipoona atanizidi nguvu nikatumia meno. Kuna kidole chake nikila chite. Na sehemu ya zingine mpaka kaenda kuoshwa hospital. Hapa najua muda wowote naweza kuitwa KITUO CHA POLICE
Kuweka heshima kwa kung'ata!Kuweka heshima tu
Tafuta wa kuendana naye