Nimegundua mdogo wangu ana mahusiano ya kimapenzi na Mpenzi wangu

Raymanu KE

JF-Expert Member
Jan 20, 2022
6,820
12,573
Habari za muda huu wanajamvi? Ni matumaini yangu kwamba mnaelendea vyema na majukumu yenu.

Nimekumbwa na msongo mkubwa sana wa mawazo baada ya kugundua mdogo wangu wa kiume Ana mahusiano ya kimapenzi na Mpenzi wangu ninayempenda kwa dhati Sana.Kwa hyo Naomba mnishauri vizuri baada ya kusoma kisa changu kifuatacho.

Nina mpenzi wangu mwenye miaka 24 na nimedate naye kwa muda wa miezi Saba Sasa.Ni mwanamke ambaye ninampenda kea dhati yangu yote na nilikuwa na malengo makubwa Sana naye ikiwemo ndoa.

Tumekuwa tunapendana Sana na Mara nyingi anakujaga home kwetu kunitembelea mixer kutangamana na familia yangu( ndugu na wazazi wangu).

Alijenga mazoea makubwa Sana na familia yangu hasa ndugu yangu mdogo wa kiume ( ninamzidi na miaka 4) Hadi wakafikia hatua ya kubadilishiana mawasiliano wakawa wanaongea kwa pigo za kishemeji shemeji.

Hilo sikuwa na tatizo nalo maana nilijua huyu Ni ndugu yangu mdogo namwaminia kwahyo sikuwahi waza kwamba anaweza date na demu wangu.

Huyu mpenzi wangu nilikuwa nampenda kwa dhati Sana na toka nianze kudate naye Wala sijawahi mcheat na demu mwingine.Nilikuwa namprovaidia Kila kitu ambacho mwanamke anahitaji kutoka kwa mpenzi wake.Nilikuwa namtazamia kula yake,mavazi,nauli,hela ya saloon,namuungia bundle na vocha kwenye simu yake,namtoa out mixer hela ya matumizi mengine ya kawaida.Chumbani Napo nilikuwa Nampa tango Yaani nilikuwa napiga shoo za nguvu Hadi ananistukia.Kwahyo ninaweza kusema kwamba mpaka muda huu sijawahi mzingua kwa lolote.

Naye hakuwahi kuonesha ishara za kudate na mwanaume mwingine tofauti na Mimi mpaka leo nilipogundua kwamba anadate na mdogo wangu Leo mida ya asubuhi tulikuwa sebuleni kwa mama tunashusha kiamsha kinya mixer kupiga story za matukio.Mdogo wangu alikuwa amekaa mkabala na Mimi na simu yake alikuwa ameiweka juu ya meza.

Sasa kipindi tunaendelea kunywa chai alikuja rafiki yake akamwita nje waongee kdgo.Alipotoka ghafla simu yake ikaanza kuita nikaona jina imeandika " SAM" afu number Nikaona ni ya huyo mpenzi wangu kbsa.Nilishtuka Sana na nikaanza kujiuliza kwanini mdogo amsevu mpenzi wangu( shemeji yake) jina tofauti na lake.Mpenzi wangu anaitwa Suzie afu yeye amemsevu SAM,kwanini?

Nikajua Kuna kitu kitakuwa kinaendelea Kati ya Hawa wawili.

Brother aliporudi ndani nikamwambia simu yake ilikuwa inaita akaichukua akaona missed call akasema this is confidential akatoka nje akampigia.Waliongea muda mrefu Sana nami nikawa nimechanganyikiwa mazima Moyo ukaanza kutetemeka Hadi nikashindwa kuendelea kunywa chai.

Aliporudi ndani nilijifanya sijui kinachoendelea nikachora plan ya kumuomba simu yake niujue ukweli wote.Nilianza kuzuga zuga kwamba nahitaji kuongea na mshikaji wangu mmoja nifanye naye biashara fulani muhimu kbsa ila Sina vocha kwenye simu.

Nikamwambia mdogo wangu Kama Ana credit kwenye simu yake anipe japo kwa dakika tano nionge na jamaa aje tufanye biashara.Bro hakumaind Sana akachukua simu akaweka password akanikabidhi nikatoka nje.

Moja kwa Moja nilingia kwenye what's up yake nikafungua chats za Sam( ambaye ndio mpenzi wangu Sasa). Aisee nilihisi nimepigwa na kitu kizoto kichwani mwangu baada ya kusoma baadhi ya charts Kati ya mdogo wangu na Mpenzi wangu.

Nilikugundua Hawa wawili Wana mahusiano ya kimapenzi yaliyo serious kbsa.Texts za mahaba na picha za uchi ndo zimesheheni kwenye what's ya ndugu yangu.Mpaka wakaelezana walivyoenjoy sex kipindi fulani

Nilibujikwa na machozi mengi Sana mixer kosononeja moyono baada ya kukutana na Mambo ambayo kamwe sikuwahi tarajia kama yanaweza kutokea.Nilifuta machozi yangu nikaosha uso ili kuficha sonona yangu.Nilimrudishia simu yake nikatoka upesi huku natetemeka Sana.

Kiukweli Nina hasira nyingi Sana kwa ndugu baada ya kugundua unyama anaonifanyia na Mpenzi wangu.Nawaza Mambo mengi kichwani na nimekosa amani ya moyoni kbsa.Muda huu nipo kwenye baa fulani kwenye mtaa najianda kuagiza pombe ninywe nilewe nijaribu kupoza maumivu ninayohisi pindi nitakapomaliza kuiwasilisha hii thread kwenu Wana JF mnipe ushauri.

Natamani ninywe sumu nikafe tu maana mwanamke niliyekuwa na malengo makubwa Nate ndo huyo ananicheat na ndugu yangu.Waliowahi kupatwa na maumivu ya mapenzi bila Shaka wanajua magumu ninayopitia muda huu.

Akili zimesimama,Moyo unauma,kichwa kinaumwa na mwili unatetemeka.Bado nampenda Sana na kumuhitaji mpenzi wangu ila Niko njia panda sijui nifanyeje tu.

Ushauri wenu utanifaa zaidi katika huu msala nilionao.
 
Habari za muda huu wanajamvi? Ni matumaini yangu kwamba mnaelendea vyema na majukumu yenu.Nimekumbwa na msongo mkubwa sana wa mawazo baada ya kugundua mdogo wangu wa kiume Ana mahusiano ya kimapenzi na Mpenzi wangu ninayempenda kwa dhati Sana.Kwa hyo

Ushauri wenu utanifaa zaidi katika huu msala nilionao.
Pole, mwachie dogo zigo we fanya ile ela uliyokuwa unatumia kumhudumia idundulize ukapange uhame kwa mama.

We kwanza chukua tena simu ya dogo uchukue ushahidi kisha wachane ukweli na uwaambie umeacha waendelee na mahusiano.

Uwa tunaamini sana wadogo zetu ila wanakulaga sana mashemej wao
 
Habari za muda huu wanajamvi? Ni matumaini yangu kwamba mnaelendea vyema na majukumu yenu.Nimekumbwa na msongo mkubwa sana wa mawazo baada ya kugundua mdogo wangu wa kiume Ana mahusiano ya kimapenzi na Mpenzi wangu ninayempenda kwa dhati Sana.Kwa hyo Naomba mnishauri vizuri baada ya kusoma kisa changu kifuatacho.
Ngoja nikwambie kitu, kama umeamini ni kweli Waite wote wakalishe hafu waambie walete simu zao waoneshe chati zao Kisha waambie endeleeni na mapenzi yenu na wewe ondoka kaendelee na mambo mengine wasichana ni wengi tu wazuri na waaminifu.

Mwisho usiwe na roho nyepesi yaani unywe sumu kisa mwanamke ebo! Huo ni utoto
 
Una malengo nae na unakunywa chai ya familiar
Habari za muda huu wanajamvi? Ni matumaini yangu kwamba mnaelendea vyema na majukumu yenu.Nimekumbwa na msongo mkubwa sana wa mawazo baada ya kugundua mdogo wangu wa kiume Ana mahusiano ya kimapenzi na Mpenzi wangu ninayempenda kwa dhati Sana.Kwa hyo Naomba mnishauri vizuri baada ya kusoma kisa changu kifuatacho.
U
 
Et unywe sumu ufe!!? 😂😂😂😂 Ukifa tu wenzio wanaoana kabsa.

We hapo waoneshe kuwa umeishajua kila kinachoendelea alaf focus kwenye mambo yako ya muhim usiwaoneshee chuki wala nini achana nao tu hio pia ni adhabu tosha
 
Mbona issue yako ni ndogo tu,yaani ujiue kwa ajili ya jitu mlilokutana mkiwa tayari mmeota vuzi,
Kata mawasiliano kimyakimya na ikiwezekana hama hapo kwenu kajitegemee,akikutafuta mwambie uko busy utamcheki na akiendelea zaidi mwambie maagizo yote kuhusu yeye umemuachia mdogo wake,hivyo kama ni pesa mdogo wako atampa,pia kama na tango mdogo wako pia atampa,na kumbuka kizuri kula na nduguyo acha uchoyo.
 
Habari za muda huu wanajamvi? Ni matumaini yangu kwamba mnaelendea vyema na majukumu yenu.Nimekumbwa na msongo mkubwa sana wa mawazo baada ya kugundua mdogo wangu wa kiume Ana mahusiano ya kimapenzi na Mpenzi wangu ninayempenda kwa dhati Sana.Kwa hyo Naomba mnishauri vizuri baada ya kusoma kisa changu kifuatacho.

Halafu huyo sio mke wako maana naona unajimilikisha wakati hujaoa Bado,

Hapa umekuja kuomba ushauli huko dogo anamtafuna shemela from the back,

Kaa kwa kutulia halafu uhame nyumbani ukapange geto ili huyo mdogo wako asijue moves zako.
 
Habari za muda huu wanajamvi? Ni matumaini yangu kwamba mnaelendea vyema na majukumu yenu.Nimekumbwa na msongo mkubwa sana wa mawazo baada ya kugundua mdogo wangu wa kiume Ana mahusiano ya kimapenzi na Mpenzi wangu ninayempenda kwa dhati Sana.Kwa hyo Naomba mnishauri vizuri baada ya kusoma kisa changu kifuatacho.
Sasa hapa ni kweli dogo kakosea sana lakini kuna vitu vichache naomba kukushauri:

1. Lazima ufahamu pamoja na makosa huyo mwanamke ni mwenye kupita ila ndugu yako huwezi kupata mwingine abadani hivyo ni vema kumweka chini dogo na kumweleza ukweli.

2. Mwanamke ambaye hujamwoa huwezi kumwajibisha kwa asilimia 100 vinginevyo utanitafutia pressure za bure...

3. Hakuna ushemeji usiokuwa na mipaka vinginevyo utalia tu... lazima ushemeji uwe na mipaka.

Ushauri wangu: Achana na huyo mwanamke na usonge mbele lakini pia mweleze dogo ukweli alichokifanta siyo sawa na kwa sababu wazazi walimfahamu hyo msichana ni vema wakafahamu kilichotokea..

Tuoe na tuache uzinifu wandugu
 
Back
Top Bottom