Rafiki yangu alivyonishika mkono hadi kufanikiwa

Notorious thug

JF-Expert Member
Dec 29, 2021
2,817
10,594
Wanajukwaaa wazima nyie?

Kiasili mimi ni mzaliwa kutoka Nyanda za Juu Kusini ndani ya Mkoa flani hivi. Elimu yangu niliipata mkoa wa Kaskazini (Kilimanjaro) kuanzia kidato cha pili hadi Chuo nilisoma kule baada ya maza kupata kazi Kilimanjaro.

Nilibahatika kupata Rafiki yangu ambaye amekuwa kama ndugu likizo nilikuwa naenda kwao. Jamaa alikuwa anaishi na mfanyakazi wa ndani baada ya wazazi wake kuhamia Dar-es- Saalam kwao walikuwa wamejenga sana.

Likizo fulani nilimualika kwetu akaja, jamaa alishangaa sana Nyumba yetu ilivyokuwa (Low quality) alinichana palepale tukiwa nae kwamba natakiwa nikifanikiwa nijenge Nyumbani na mji wangu.

Baada ya kidato cha sita matokeo kutoka tulipata chuo kimoja pale Moshi. Tulivyomaliza mimi nilienda Arusha yeye akaenda Dar-es-Salaa. Baada ya kupotezana miaka miwili nilifanikiwa kukutana nae Dar-es-Salaam, jamaa alikuwa anapush Toyota Harrier ila alinidanganya la Mzee wake.

Jamaa alinipeleka Kimara mtaani kwao alikuwa na maduka mawili ya kwake nilichoka sana miaka miwili amewezaje. Kesho yake akanipeleka Kariakoo nilichoka maduka wanayo matatu moja la Baba yake moja lake moja la viatu vya kike la Dada yake.

Nilipata kuongea na Baba yake nikamweleza mambo yangu ikiwepo suala la kuoa akanishauri nilifute mara moja kwakuwa sijasimama kiuchumi, akanishauri nisirudi mkoa nibaki Dar kukimbizana na mishemishe kweli Baba yule alinipa chumba ndani ya nyumba yao pale Kimara ikawa asubuhi ni kuamka kwenda Kariakoo kukimbizana.

Alikuwa ananishauri sana ndani ya mwaka mmoja nihakikishe nimesimama mwenyewe kwani uwezo ninao kwenye biashara nilikuwa sina uzoefu ila kila siku tukirudi home lazima yule mzee aniite tupige hesabu nimepata sh ngapi, kwa siku tukawa na daftari kama tatu moja la kuanzisha duka langu, moja la kununua Kiwanja, moja la kuanza ujenzi.

Niliishi maisha ya kutokula bata na ubahili yule mzee alikuwa anatutoa weekend tu maisha yalikuwa magumu nilikuwa nakula kwa macho pisi kali za Kariakoo.

Baada ya Miaka miwili nimesimama na nimeanza Ujenzi huku nina Maduka mawili. Hakika ndugu yangu Kimaro umenitoa mbali🙏🏿🙏🏿.
 
Aisee Kuna siku nilikuwa hapo Moshi mjini enzi nimemaliza chuo. Sina hili Wala lile. Sasa natafuta tempo nikaambiwa ingia majengo seko. Sipajui ulizia binti akaniunganisha na teacher was kituo Chao Cha qt Nina simu haina dakika yule binti bana akaninunulia muda wa maongezi wa buku nikaongea ,ninashukuru kinyama. Nikaanza kusogea karibu kwake sema nikaona repulsion force ikabidi niikubali fosi iyo.

Yule binti Ana roho nzuri mno jamani sijawahi ona. Aliyemuoa akapata mke
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom