R.I.P mwanaJF!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,724
Viongozi wangu,

Salaam!

Kwa heshima na Taadhima naomba tukumbuke thread hii
HII-HAPA


Nimetaarifiwa na mwan-JF wa hapa Arusha kuwa mnamo tarehe 24/12/2010 member mwenzetu fulani waJF aliyekuwa anajulikana kwa jina la mtaani kama Abuu Mkongo alikuwa anasafiri kutoka Arusha kwenda Same kwao kwaajili ya sikuuu za mwisho wa mwaka, na akapata ajali katika kijiji cha Kileo-Mwanga iliyochukua maisha yake, akiwa kwenye gari no T391 PMG, aina ya Toyota Subaru, ambapo chanzo cha ajali ni kupasuka kwa tairi ya mbele.

Abuu alikuwa ni member active sana wa JF, lakini cha kusikitisha ni kwamba mleta habari(ambaye ndiye aliyemshawishi kujiunga na JF enzi hizo) hakuwahi kujua huyu marehemu alikuwa anatumia ID gani katika mabandiko yake...:sad: (hivyo mabandiko na posts zake zitalala doroo, na hatimaye kupotea kabisa baada ya muda..)

Aidha marehemu huyu alikuwa akifanyia kazi Ofisi ya ITV/Radio One -Arusha, akiwa kama muandaaji picha.

Mungu alilaze pema roho ya marehemu.
ABUU%252520MPIGA%252520PICHA0001%255B1%255D.JPG


 
Duh so sad jamani mi naomba anaetaka my id anione kwenye pm ili nikiaga dunia aweze kua access na kuwajuza,r,i,p braza!
 
kweli hizi ID na real name inapaswa member ajue jinsi ya kujitambulisha angalau kwa member mmoja,
lakini hii yote ya kufichaficha inatokana na wtu kutojiamini ama kuwa na wsiwasi wa kushughulikiwa kwa njia moja ama nyingine
mathalani sisi tuko ofisini (Dept) moja wana JF zaidi ya sita lakini hakuna mtu anaejua ID ya mwningine na kila mtu anafanya ni siri,

NAWAOMBA NDUGU ZANGU KWA SABABU TUMESHAINGIA HUMU JF TUJARIBU KUANGALIA NI NANI AMBAYE UNAENDANA NAE (KIMISIMAMO, KIUUANDISHI, HOBBIES NK), BASI TUJARIBU KUJENGA URAFIKI WA KARIBU ILI HATA KAMA UTAKAPOPATA TATIZO HUYO ANAYEKUFAHAMU ATAWAJULISHA MEMBER WENGINE

KUNA MEMBA HUMU ALISHAPATA MSIBA WA BABU YAKE ARUSHA, NA BAADA YA KUWEKA HUKU AKAJIKUTA YUPO NA NDUGU YAKE AMBAYE ALIKUWA ANAMWONA KILA SIKU HUMU JF

RIP ABUU
 
Back
Top Bottom