Q & A ya Mhe. Rais & Mhe. Abdallah Possi

Kwanini asiachane na Abdalah Bulembo au Kabudi ambao hawajaapa kuwa wabunge?, nadhani hao bado wapo kwenye process ya kuwa wabunge, hawajawa wabunge mpaka watakapo apa.
 
Kwanini asiachane na Abdalah Bulembo au Kabudi ambao hawajaapa kuwa wabunge?, nadhani hao bado wapo kwenye process ya kuwa wabunge, hawajawa wabunge mpaka watakapo apa.
Akiachana nao itaonekana wazi amekurupuka, ili kuua so imebidi amtoe kafara Posi
 
Pole sana mpiga dili!
 
Akiachana nao itaonekana wazi amekurupuka, ili kuua so imebidi amtoe kafara Posi
Kwahiyo tatizo ni kukiri makosa? Yeye akubali kukiri kosa halafu atimue msaidizi wake, itakuwa imeeleweka kuwa ameshauriwa vibaya
 
tuisome na ibara ya 36 (1),(2) na(3).....ya katiba JMT...
 
hizo ndizo akili zinazoitwa za mwendo kasi...na mbaya zaidi mwenye akili hizo ndiye tuliye mkabidhi panga atufyekee kichaka...kichaka ambacho ndani yake kuna miti tunayoitegemea ya dawa...nadhani miti yote ata ile yenye kutoa matunda ivi sasa imekatwa na kuharibiwa vibaya.
 

Mkuu Paskali salaam

Nasita kukubaliana na kauli yako ya mwisho kuwa Tanzania hatuna wanawake wenye sifa ya kuwa wabunge. Maana sifa ya kuwa mbunge ndio sifa kuu ya kuteuliwa kuwa mbunge. Hivi kweli mkuu Paskali ukiambiwa utafute wanawake watatu wenye sifa ya kuwa wabunge utakosa nchi nzima? Hata kama ni unyanyapaaji huu umezidi. Hata kama mhe amejipambanua kuteua wasomi, je ukiambiwa kutafuta PhD holders wanawake watakosa kufika watano? Mbona tunawaona vyuoni wakifundisha? Mbona kuna wanawake wengi sana wenye Masters tunawafahamu. Kama haitoshi, kwa mujibu wa katiba ya JMT sifa ya kuwa mbunge sio Masters/PhD/Prof bali ni kujua kusoma na kuandika.

Hivyo, ni kusema kwa TZ nzima hakuna wanawake 10 wanaojua kusoma na kuandika?
 
→→Siku zote kiongozi anafanana na anaowaongoza...

Kabla ya kumnyooshea kidole JPM tuanze kujitizama sisi tuliomchagua....
 
Mmmmmh hya wacha tuwaachie wanaojua sheria wtufafanulie
 
Kwanini asiachane na Abdalah Bulembo au Kabudi ambao hawajaapa kuwa wabunge?, nadhani hao bado wapo kwenye process ya kuwa wabunge, hawajawa wabunge mpaka watakapo apa.
Anajua akifanya hivyo hatimae atakuwa ametoa ujumbe hadharani wa kukiri kwamba alivurunda!
 
Kwa aibu kama hii lazima mawaziri, makatibu wakuu na watumishi waandamizi wa serikali wabaki midomo wazi. Hivi huyu Rais ana washauri?
Hivi ninyi mnaowalaumu washauri wa Rais hampati hisia kuwa hamuwatendei haki ; kama watu wazima pambanueni silka, haiba, na hata carible ya mkuu hivi kama hivyo ndivyo alivyo jukwaani hadharani je huko kwenye vikao Vya faragha?
 
Mkuu Chaque Number, sijasema kuhusu sifa tuu, nimesema sifa na vigezo, jee unavijua vigezo? , kama huvijui then naomba tuu ukubaliane na mimi kuwa hatuna wanawake wa kutosha wenye kukukidhi sifa na vigezo, wangekuwepo, wangeteuliwa. Kitendo cha kuteuliwa wanaume 6 wanawake 2, ni proof kuwa wanawake hawapo wa kutosha!.

Paskali
 
tuisome na ibara ya 36 (1),(2) na(3).....ya katiba JMT...
Kwanini usingeweka hapa hizo Ibara ili watu wajiongeze?! Wengine tunatumia nokia torch zisizo na uwezo wa ku-download pdf files! Na kama ni hardcopy zipo accessible kwa wachache!!
 
Ndugu Pasco sidhani kama ni sahihi kuthibitisha kauli yako ya kuwa hatuna wanawake wa kutosha wenye sifa za kuteuliwa kuwa wabunge kwa premises kwamba mpaka sasa wameteuliwa wawili tu dhidi ya wanaume sita.

Ieleweke kwamba raisi halazimishwi kufanya teuzi hizo kwa mara moja bali anafanya hivyo kulingana na uhitaji wake na anapoona ni vema kufanya hivyo. Kwa hiyo suala la uteuzi wa wabunge wawili wa kike halikuwa suala la upatikanaji wao (ninavyoamini) bali hivyo ndivyo ilivyompendeza mwenye mamlaka.

CN
 

Hongera Chige, hiyo ndiyo tafsiri sahihi "IN CONTEXT".

Inasikitisha kuona juhudi na lundo la "watafsiri" wenye kulazimisha vifungu ili kupata maana wanazoztaka. Ni wazi hawajui kanuni za fasiri na urari. Jambo lolote lenye kueleweka maana, halihitaji tafsiri. Swali ni je kuna mtu yeyote ambaye akisoma Ibara ya 71 haelewi ina maana gani???
 
Kwenye hii mada naona kuna watu wawili wana kuja sana speed kujustify maelezo yoooote ya Dr Possi kuteuliwa kuwa Balozi tukubali kukataa Mh aliteleza swala LA wanawake wenye uwezo wapo sana ila jamaa ni mfumo dume yaani hata hawa wengine ni bhasi tu
 
Vizuri...! Swali litakuwa Je, Dr. Possy aliteuliwa kutokana na uamachama wake CCM au vinginevyo? Kama uteuzi wake umeetokana na u-CCM wake basi itabidi wamvue uanachama ndipo anaweza kupoteza sifa za kuwa mbunge vinginevyo; atabaki kuwa mbunge!!!
Wabunge wakuteuliwa hawana chama mkuu.
 
Wabunge wakuteuliwa hawana chama mkuu.
Kama ndivyo basi hafukuziki... labda ajiuzuru au kufanya mambo yanayoweza kumuondolea sifa ya kuendelea kuwa mbunge!
 
Hivi ninyi mnaowalaumu washauri wa Rais hampati hisia kuwa hamuwatendei haki ; kama watu wazima pambanueni silka, haiba, na hata carible ya mkuu hivi kama hivyo ndivyo alivyo jukwaani hadharani je huko kwenye vikao Vya faragha?
Ni ukweli mtupu...! Hana dalili na wala haoneshi dalili japo kwa mbali kwamba ni mtu anayekuwa standby kusubiri ushauri hata ule ulie kinyume na maono yake!
 
Tasfida mujarabu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…