Pwagu na Pwaguzi

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Vile vipindi vya Pwagu na Pwaguzi viliishia wapi?
Vilikuwa vinaburudisha na kufunza. Wale wazee walikuwa mahiri kweli.
Mimi nakumbuka kisa kimoja hiki:
"Pwagu alimshitaki Pwaguzi kuwa alimrembea rungu ikampasua kichwa. Katika kesi ili kuwa hivi:
HAKIMU: Bwana Pwaguzi, unasema Pwagu alikurembea rungu ukaumia kichwani ni kweli?
PWAGUZI: Muheshimiwa Bwana Hakimu ni kweli, ushahidi jeraha hili hapa.
HAKIMU: Pwagu una lipi la kusema?
PWAGU: Naomba kumhoji mdai, Bwana Hakimu, kwa ruhusa yako. [Hakimu anatoa ruhusa ya kuhoji].
PWAGU: Unasema nilikurembea rungu, uliniona?
PWAGUZI: Nilikuona.
PWAGU: Nilikuwa umbali gani?
PWAGUZI: Ulikuwa karibu sana, na ndio maana rungu ikatua juu ya kichwa changu.
PWAGU: Uliona kuwa nimekamata rungu mkononi?
PWAGUZI: Ndiyo!
PWAGU: Uliona jinsi nilivyokuwa ninajitayarisha kukurembea rungu hilo?
PWAGUZI: Ndio nilikuona, nilikuwa ninakuangalia shahidi macho yangu.
PWAGU: Nilipokurembea ulilikwepa?
PWAGUZI: Sikulikwepa!
PWAGU (Kwa Hakimu): Bwana Hakimu, mdai anasema aliniona nimekamata rungu mkononi, nikijitayarisha kulirembea, yeye ananitazama tu, nikamrembea nalo, yeye ananiangalia tu; Huoni Bwana Hakimu Pwaguzi alikuwa ananitega kwa makusudi nimrembee nalo?
HAKIMU: Pwaguzi, inaonesha ulikuwa unamtega mwenzako kwa makusudi. Kesi Dismiss.

Unakumbuka kisa gani cha Pwagu na Pwaguzi?
 
oooh yess, siku hiyo walipata tenda ya kupaka rangi ya nyumba ukutani. basi hawakubakiza kitu walipaka hadi watotop wa mwenye nyumba, aliporudi ile anashanga shanga na yeye wakaanza kumpaka, kilianguka kichapo hapo, walitoka nduki .......... huko mbele wakaanza kulaumiana wenyewe mwishowe ngumi zikafumka baina yao , na ndio mwisho wa mchezo.
 
...enzi zetu/baada ya kupata UHURU WA TANGANYIKA!
 
Enzi zile nikiwa mdogo, kabla
sijaanza darasa la kwanza na
hata baada ya kuingia shule ya
msingi tulizowea kusikiliza
vipindi vya Mahoka na Pwagu
na Pwaguzi, vikirushwa na Redio Tanzania, hakuna shaka
hawa jamaa walikuwa vinara
wa vichekesho kwa jinsi
walivyoweza kupangilia
vituko vyao japo tulisikia sauti
tu bila kuwaona.
 
Siku hizi TBC wanarudia hiyo michezo ya Pwagu na Pwaguzi.

Jamaa walikuwa Comedians wa nyakati zao.
 
F
huwa wanarudia siku na muda gan mkuu
Kila siku jtatu hadi ijumaa, saa saba kasoro robo na saa kumi na mbili kasoro robo...mara mbili kwa siku.

Ila tu siku hiyo kusiwe na kipindi maalum na kusiwe na mechi ya ligi kuu jioni.
 
Back
Top Bottom