sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,034
Ni wazi kabisa kipindi cha Trump, raisi wa Urusi alikuwa akimheshimu sana kiasi kwamba hakuweza kuthubutu kufanya haya anayoyafanya kwa sasa kwa sababu aliogopa response ambayo Trump angeichukua.
Kwa sasa Marekani inaongozwa na raisi mithiri ya mdori ambae media inatumia nguvu kubwa sana kuficha udhaifu wake madarakani ila mdori ni mdori tu mbele ya wababe kama kina Putin.
Putin baada ya kuivamia Ukraine kipindi cha Obama 2014, alitulia tuli kama maji mtungini alipoona Trump kashika madaraka, ila kwa sasa kaona raisi mdori kashika madaraka kaamua kuchukua majimbo mawili kabisa afidie na jimbo ambalo uwepo wa Trump ulimzuia kulichukua.
Ni dhahiri kwa sasa hata China huenda ni suala la muda tu kuamsha dude huko Hong Kong ama Taiwan.
Kwa sasa Biden ni kituko tu hasa kwenye ile aibu ya karne Afghanistan, yeye kama amiri jeshi mkuu alifanya uamuzi wa jeshi kuondoka Afghanistan kabla ya raia, matokeo yake raia wa Marekani wakabaki wamenasa bila mtetezi, Pia jeshi liliondoka likiwa limeacha silaha zenye thamani zaidi ya triloni 180 kwenye makambi, Tukio hili lilionesha wazi kabisa Biden kama amiri jeshi mkuu hakuwa na akili hata ya kawaida ya kuamuru kuwatoa raia wa nchi yake na kusafirisha silaha ama kuziharibu kisha hatua ya mwisho iwe kuliondoa jeshi, hali hii ilisababisha wanajeshi 13 kuuliwa, Media ilifanya juhudi kubwa kufanya hii ishu isiongelewe.
Xi Jin Ping anasubiri kupokezwa kijiti na Putin nae afanye yake, kama ni vikwazo washavizoea.
NYONGEZA:
Ikumbukwe ya kwamba Trump hakupatikana na hatia yoyote katika kashfa iliyoanzishwa kwamba alisaidiwa na urusi uchaguzi wa 2016,,, Ripoti ya Mueller ilitoka ikimsafisha dhidi ya kashfa hizo..
Baada ya Ripoti ya Mueller, uchunguzi wa chanzo cha kilichoanzisha hio kashfa ulianza, Hadi sasa uchunguzi unaendelea na kwa sasa kilichoonekana ni kwamba mama Clinton aliwalipa pesa ndefu majasusi waingilie mifumo ya Mawasiliano kwenye ikulu white house kubambikiza data zilizokuwa zikionyesha kuna mawasiliano kati ya white house na Marekani.