Pupa ya kutaka kushika madaraka, itaiangusha CHADEMA tena

Pupa ya kutaka kushika madaraka, itaiangusha CHADEMA tena

BongoTz,
Choo cha kisasa maana yake ni kwamba kina maji, karatasi za kuchambia pamoja na flush zinazofanya kazi. So kama watu wameharibu hivyo vitu, then hilo sio tatizo la Kikwete na serikali yake. Hilo ni tatizo la wananchi wenyewe.
Mkuu wangu hapo ndipo unaposhindwa kuelewa Tanzania. Choo cha kisasa ni choo cha kukaa kwisha!... maswala ya maji unaweza kumwagia kwa ndoo na kipudu kinakokwenda anajua Mungu.. Ni toka ujenzi wake ndio maana tunazungumzia sana Infrastructure yetu mbovy. Huwezi kwenda choo ukakuta maji na karatasi kwa sababu vitu hivyo ni adimu na pengine watakwambia ghali. tembelea vyoo ulivyovitaja utagundua kwamba hakuna maji wala karatasi za kuchambia. Hii ndio fact.
Well, najaribu kuielemisha jamii (through articles and stuff)--itambue kuwa tabia ya kulaumu viongozi wa juu wa serikali hali wananchi wenyewe wanafaya vitu vya kijingakijinga (kama kuiba mafuta ya transformer, kuiba mabomba ya maji, kupaka kinyesi kwenye vyoo vya umma, kukojoakojoa ovyo uchochoroni, na kukaa vijiweni na kupiga porojo badala ya kujiajiiri); haitatupeleka kokote hata kama utaweka malaika waitawale Tanzania.
Pili, wizi wowote ule unapozidi ni dalili kubwa ya Unemplyment. Ajira hakuna au kazi hazilipi.
Kama serikali inashindwa kuanzisha ajira basi fahamu kwamba watu hao watatafuta njia nyingine za kujipatia kipato kwani maisha hayasubiri Mkapa au Jk watakapofikisha miaka 10 ya ahadi zao..Iweje watu hao hao wakiwa Ulaya hawayafanyi wanayoyafanya Bongo?.. iweje sisi tulozaliwa na kukulia tanzania tumeweza kuishi nchi hizi kama wazungu hali tumezoea kuchambia kuta ikiwa kweli ni tabia yetu?..
 
Mkuu hapa unazungumzia Mtazamo wa Democratic na projection yao ambayo inapingwa na Republican. Hivyo kuandika kupunguza deficit haina maana yoyote ikiwa wananchi hawakubaliani na mahesabu hayo kwani Republican wanachosema Healthcare itaongeza gharama za kufanya biashara...
Mkuu, inaelekea hujui kabisa unachokizungumza hapa... ama unataka tu kubisha ili watu wakusifie. Hizo projections hazikuwa mtazamo wa Democratic. Hizo projections zilitolewa na Congressional Budget Office (CBO) which is a very respected non-partisan agency in Washington. That's a fact, na wala haijalishi kabisa Republican watakachosema...

Hivyo, Independent sii lazima wasikubaliane na kila kitu cha Democratic ili uwe independent..unaweza kuunga moja au hata mengi lakini ukapinga mengineyo ambayo kwako ni muhimu hivyo usikichague chama hicho au mgombea fulani..Wapo watu tanzania leo hii wameamua kuwa Independent kwa sababu tu CCM imeshindwa kuwathibiti Mafisadi na kama JK ataweza kuwashawishi upya pengine wanaweza kurudi.
Totally agree with you here... Ila maelezo yako ya kwanza kuhusu kwanini Independents wanaonekana kumkimbia Obama [kwasasa] yalikuwa nje ya mstari. Ndo' maana ilinilazimu kukukosoa/sahihisha.

Does it matter?..Au ndio ktk kusahihishana ili mradi tu ujumbe ufike. Well, nadhani umeelewa kwamba serikali inaweza kuwa problem..na ndicho tunachosema sisi kwamba serikali ya CCM ndio Problem haiwezi kuwa solution ya matatizo yetu.
Oh, yes it matters a lot! Cuz in your previous reply, ulikuwa unajaribu kujenga hoja kwamba hiyo ndo' ilikuwa campaign slogan ya Regan [which is not true]. No, serikali sio tatizo. Tatizo ni wananchi wenyewe. Kwasababu wananchi ndo' wana nguvu ya kuiweka serikali yeyote ile madarakani (ukiondoa serikali za kimabavu). So kama wananchi wenyewe wameshindwa kutumia haki yao ya kidemokrasia kupima na kisha kumchagua kiongozi mwenye sera na mipango madhubuti ya kuwaletea maendeleo, na kumkataa kiongozi mbabaishaji. then that's their own problem.

P.S. Usishangae kuwa nime-skip kujibu some stuff like stimulus and healthcare/insurance... I did that cuz "I respect your right to be wrong" maana nime-provide majibu kuhusu hizo issues already, ila tu wewe ndo' hutaki kuelemika.
 
chama imara cha kisiasa ni lazima kwanza kiwe na muundo thabiti, mtandao mzuri wa kisiasa unaoanzia ngazi moja hadi nyingine pamoja na kuwa na mfumo unaosadifu wa kisera na kiitikadi na kutambulika, achilia mbali kukubaliwa na wananchi.

Chadema chama ambacho kwa bahati mbaya sana kimebahatika kukubalika kikanda na kuungwa mkono na kundi la kabila la kichaga, bado hakijajipanga na kuonekana wazi kama "a real political party" ili kuivuta na kuishawishi hadhira kubwa inayoishi vijijini na mijini kwamba wao ndio wanaostahili kuiongoza tanzania na sio ccm.


mizizi na nguvu za ccm ni kubwa mno katika nchi yetu, anayepuuza ukweli huu ni mpuuzi jasiri asiyejua kupambanua baina ya mbivu na mbichi, na bila shaka hataki kwa makusudi kujua ukweli wa mambo ulivyo.


msingi imara wa chama cha taa ulijengwa kutokana na harakati za machifu wa tanganyika katika dhati ya kupambana wakiwemo baadhi yao kina mangi meli, kinjikitile, mirambo, kimweri, mkwawa, makunganya, bushiri na wengine--wakati kukubalika kwa chama cha tanu ni matokeo ya nguvu na juhudi za chama cha taa.


kwa msingi huo kuimarika na kukubalika kwa ccm ni kutokana na kujijenga kwa vyama vya tanu/asp ambavyo ni vyama viasisi vya siasa katika tanganyika na zanzibar tokea miaka ya 1954 na 1957.


ccm inatofauti sana kimtazamo na vyama kama upc cha uganda, mcp cha malawi, na unip cha zambia au kanu kilichokuwa kikitawala kenya.


vyama hivi navyo vilikataa kujikita na kuweka mizizi ili kulishika kundi la watu hasa mababa-kwabwela wanaoishi vijijini na kulazimishwa kutambua kwamba mafanikio na ujio wa uhuru wao ulitokana na vyama hivyo.


kiuhalisia na kinadharia vyama hivyo mara baada ya uhuru vilibadilika na kuwa vyama vya kibwenyenye na kimwinyi kwa kuusahau kabisa kuutazama umma wenye nguvu za maamuzi na utafutaji wa ridhaa ya kudumu (ccm nayo ilijaribu kubadilika lakini sio kwa kasi kubwa ya kutisha kama ilivyokuwa kwa majirani zetu wa uganda, kenya, malawi na zambia. Shukrani za peee kwa hayati kambarage nyerere, mwasisi wa ccm).


wanaojaribu kuitazama ccm kwa jicho rahisi wafanye pia utafiti mgumu ili kutambua matokeo kamili kabla na baada ya ujio wa vyama vingi huku wakiidurusu kwa weledi hali ya mambo na wakati ulikuwaje kwa nyakati hizo.


tanu haikupata kazi ya suluba ya kujenga matawi mapya toka mwaka 1954 kilipoanzishwa kuanzia kanda ya mashariki, lake zone ,kaskazini na kusini mwa tanzania na hatimaye kusambaa nchi nzima, kutokana na kurithi matawi yoye toka kwa chama kikongwe cha taa.


kuzaliwa kwa ccm tarehe 5,2,1977 na kuenea kwake ilikuwa ni kama kuua tembo kwa bua kutokana na chama hicho kuiga tabia ya nyoka anayejibua gamba, na yeye kubaki akiwa ni nyoka yuleyule mwenye sumu kali.


tanu iliutumia vizuri mfumo wa chama kimoja na kueneza siasa zake hadi kwenye taasisi za serikali, mashirika ya umma, vyuo vikuu, sekondari hadi hata kwenye vikosi vya ulinzi na usalama.


haikuwa kazi nyepesi inayoweza kuleta hasara haraka au kwa ulaini kama iliyovyazamwa na inavyoendelea kutazamwa na baadhi ya wahariri a mambo ya kisiasa.


base ya tanu ni taa. Base ya ccm ni tanu na asp. Cuf inatokana na vuguvugu la kamahuru, nccr -mageuzi ni mkusanyiko wa wanaharakati waliolilia mageuzi ya kikatiba tokea miaka ya 1990. Lakini chadema chimbuko lake halisi hasa ni nini na wapi? Au ndiyo ili iliyoelezwa kuwa something like "chagga develpement manifesto"?


takriban miaka 27 ilipita chini ya chama cha tanu kikiwaimbisha na kuwachezesha kwata wananchi chini ya zama ya nguvu ya chama kushika hatamu tangu pale mfumo wa vyama vingi ulipopigwa marufuku mwaka 1965; fursa na nafasi hii haikutumiwa ipasavyo huko zambia, uganda, malawi na kenya, na huu ndio ukweli wa mambo, ila anayetaka kubeza hawezi kuzuiwa.


ccm haikulala usingizi wa pono pale ulipoingia mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, ilianzaa kujichimbia kisiasa, kuingiza wanachama wapya, kujinadi mbele ya umma na kuubeza upinzani kwa nguvu ya hoja.


ni kweli serikali zake zimekuwa zikikabiliwa na matatizo mengi tokea awamu ya kwanza hadi hii ya sasa tuliyonayo--huku chama chenyewe kikijitutumua kwa bidii kulinda hadhi yake na kujivunia rasilimali watu.


katika awamu ya kwanza mashirika yote ya umma yalifujwa, hakuna aliyefikishwa mahakamani, awamu ya pili walikamatwa watu wakisafirisha dhahabu uwanja wa ndege wa kimataifa wa dar ess salaam, kesi ikayeyuka huku katika awamu ya nne tumeshuhudia mikataba mibovu ya madini na wizi katika akaunti ya epa na bot ikifanyika katika awamu ya tatu bila hatua zozote za kisheria kuchukuliwa dhidi ya waharifu/husika.


ccm mara kadhaa kimekuwa kikijikosoa na kujipanga kutokana na kupata msaada wa mtandao wake uliojengeka tanzania nzima kwa miaka mingi.


vyama vya tanzania vina pupa ya kutaka kushika madaraka ya juu vianze kwanza kujijenga ndani ya halmashauri za wilaya, bunge na baraza la wawakilishi huku vyenyewe vikitambua mitandao yao ili kupata ushindi ni dhaifu.


serikali ya ccm chini ya rais jakaya kikwete imejitahidi kupambana na ubadhirifu wa mali ya umma, kukemea rushwa na kwa bahati nzuri kesi ziko mahakamani zikiwakabili vigogo wazito. Ingawa wengi wa hao wahusika wanataachiwa huru bila kupata adhabu wanayostahii, lakini hilo pekee ni jambo linalowaongezea wananchi mapenzi na hamu ya kuendelea kuiamini ccm, nje ya hilo ukifuatilia utekekezaji wa ilani ya uchaguzi ya ccm toka awamu ya tatu hadi ya nne, tanzania imepiga hatua (ingawa sio kubwa sana kimaendeleo).


barabara, zahanati na huduma za maji safi zinatia moyo kinyume na miaka ile mara baada ya kupata uhuru, vyama vya bongo vijizatiti, viongozi wake wajitume na wasitegemee wao kuja kufaidi matunda ya nguvu zao, wafanye kama walivyofanya kina mkwawa na mangi meli.


kuimarika na kujengeka kwa chadema kuna tofauti sana na kujengeka kwa cuf. Chadema mwanzo wake unatokana na safu ya waasisi wa chama hicho. Brown ngululupwi, edwin mtei, bob makani, costa shinganya, na kimesera. Hili lilikuwa ni kundi la masetla watupu na halikuwa la wanasiasa waliotambulika na kufanya kazi za kisiasa.


cuf ni chama kilichomega nguvu ya ccm zanzibar baada ya wanachama wake vigogo wapatao saba walipofukuzwa mwaka 1988 akiwemo seif sharif hamad mtu aliyewahi kuwa waziri kiongozi wa smz.


vigogo wengine ni khatib hassan khatib aliyewahi kuwa mhazini wa ccm na mnec--hamad rashid mohamed ambaye aliwahi kuwa naibu waziri wa fedha na mambo ya ndani ya nchi, juma ngwali na masoud omar wakiwa wakuu wa mikoa.


wanasiasa wengine waliopevuka kisiasa ni pamoja musa haji kombo aliyewahi kuwa katibu mtendaji mkuu wa ccm, juma othman juma aliyekuwa mjumbe wa nec, ali haji pandu waziri wa sheria katika smz, soud yusuf mgeni waziri wa kilimo pamoja na maulid makame abdallah aliyewahi kuwa waziri mdogo wa afya zanzibar.


kundi hili la cuf kwa kiasi kikubwa liliweza kuibana mbavu ccm kutokana na wao kuitambua misingi ya kuunda chama cha siasa na kukieneza kama taasisi.


nieleweke wazi kwamba sikipigii chapuo chama cha cuf ila nimefanya utafiti na kuiona tofauti kubwa kati ya ccm, chadema na cuf. Chadema wajenge kwanza mizizi na kundi lililopo sasa lisitegemee kula matunda ya juhudi hizo.


chama cha chadema na vingine katika tanzania vinapaswa kujifunza na kupita katika barabara ya chama cha liberal party cha uingereza amacho hakikuwa na papara ya kushika madaraka haraka bali kilitafuta kwanza amana na hatimaye kikaaminiwa.


cuf wanaelekea kuingia katika medani za serikali zanzibar baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, hatua hiyo pekee ukiwa mtu mkweli utaweza kujua usahihi wa tathmini yangu.


bado siamini kutokana na utafiti mdogo nilioufanya kwamba chadema kimejiandaa na kimejijenga kimfumo, kisera na kimtandao kiasi kwamba kiweze kushinda katika uchaguzi wa mwaka huu na kuongoza dola.


jambo hili kwa chadema sitaki kabisa niliamini moyoni mwangu, naomba lisistawi kabisa kwenye mishipa ya fahamu zangu na kwenye ubongo wangu pia.


chadema hakitashinda kutokana na kwamba bado ni kichanga, kiliwahi kusifiwa na mwalimu julius nyerere kwamba kina sera zenye mwelekeo lakini kina upungufu wa wanasiasa, ni sawa tu na timu ya soka yenye nyota haba wa kuleta ushindi.


safu ya kina wilbroad slaa, zitto kabwe, john mnyika, halima mdee, philemon ndesamburo, maulida komu na mabere marando ni kundi la wasomi wa fani za kitaaluma wakikosa mtaji na ujuzi wa mizungu ya ufanyaji wa siasa.


slaa ni mwanasiasa mahiri, mwepesi wa utambuzi wa mambo, hata kutoka kwake ccm baada ya kukatwa jina lake na kupachikwa kwa patrick qorro katika kura za maoni kulilalamikiwa sana na mwalimu julius nyerere.


slaa ni yeye peke yake kinara ndani ya chadema akizungukwa na timu hafifu isiyo na uwezo ama ukomavu wa kisiasa wa kukiletea ushindi chama hicho. Kwa upande mwingine, ccm bado kina ngome kubwa, viongozi wengi wenye amana mbele ya umma ambao hawakuona umuhimu wa kujitoa ndani ya chama hicho kwa wingi na kujiunga na kambi ya upinzani.


chadema, nccr na tlp ni vyama vinavyoweza kuja kujiimarisha katika siku nyingi zijazo usoni, cuf kwa upande wa bara nao wamo katika msafa wa vyama hivi vitatu, hawajawa na timu imara na pia kiongozi wake profesa ibrahim lipumba hajaungwa mkono na wasomi wenzake wa chuo kikuu cha dare es salaam kuonyesha kama anakubalika.


hata yeye lipumba anaonekana yuko peke yake. Ni sawa kabisa na kusema mchezaji nyota wa brazil "kaka" aamue kusajiliwa na balimi ya bukoba kisha timu hiyo ghafla itarajiwe kutandaza kabumbu safi uwanjani, aifungie magoli mengi timu hiyo, hata aiwezeshe ichukue ubingwa wa ligi kuu. Wa-da-nga-yi-ka wenzangu hebu tusijidanganye. Hiyo ni ndoto ya mchana. Hilo haliwezekani kwa mwaka huu na hata baada ya miaka kumi na tano ijayo, chadema isitegemee kushinda kwasababu bado hakijajipanga vizuri.


mungu ibariki afrika, mungu ibariki tanzania!


p.s. [makala hii imeandikwa na antar sangali, mwandishi wa bongotz.com]
hivi huu si ndo wanaita utumbo jamani,au mnasemaje?
 
Mkuu, inaelekea hujui kabisa unachokizungumza hapa... ama unataka tu kubisha ili watu wakusifie. Hizo projections hazikuwa mtazamo wa Democratic. Hizo projections zilitolewa na Congressional Budget Office (CBO) which is a very respected non-partisan agency in Washington. That's a fact, na wala haijalishi kabisa Republican watakachosema....
Naona hatuelewani lugha sasa soma hata hii habari Bofya

Totally agree with you here... Ila maelezo yako ya kwanza kuhusu kwanini Independents wanaonekana kumkimbia Obama [kwasasa] yalikuwa nje ya mstari. Ndo' maana ilinilazimu kukukosoa/sahihisha.
Hakuna kitu hukukosoa kitu ila mimi ndio nimekukosoa baada ya wewe ulipotosha kuonyesha kuwa independent wana mahusiano na itikadi za Demokratic..Uliandika hivi:- independents wengi wamemkimbia kwasababu the whole wing of democratic part wanaonekana kama wimps fulani (they don't stand in what they believe/wanacompromise mno!). Na sii kweli kwani Independent hawajali compromise za Domecratic ila priority zao kuwezeshwa..
Oh, yes it matters a lot! Cuz in your previous reply, ulikuwa unajaribu kujenga hoja kwamba hiyo ndo' ilikuwa campaign slogan ya Regan [which is not true]. No, serikali sio tatizo. Tatizo ni wananchi wenyewe. Kwasababu wananchi ndo' wana nguvu ya kuiweka serikali yeyote ile madarakani (ukiondoa serikali za kimabavu). So kama wananchi wenyewe wameshindwa kutumia haki yao ya kidemokrasia kupima na kisha kumchagua kiongozi mwenye sera na mipango madhubuti ya kuwaletea maendeleo, na kumkataa kiongozi mbabaishaji. then that's their own problem.
Na ndio maana hukunielewa toka mwanzo kwani the message ilikuwa kukuonyesha jinsi serikali inavyokuwa responsible na matokeo yoyote. Kushindwa kwa CCM hakuwezi kutokana na wananchi ikiwa serikali yenyewe haikubali kuwa ndio tatizo. Hata Nyerere alijiuzuru akakubali kushindwa na sii kwamba wananchi wake ndio walishindwa..Hivyo hotuba ya Reagan lini na wapi sii sababu ila maana ya maneno yale hata kama angesemea ******.
P.S. Usishangae kuwa nime-skip kujibu some stuff like stimulus and healthcare/insurance... I did that cuz "I respect your right to be wrong" maana nime-provide majibu kuhusu hizo issues already, ila tu wewe ndo' hutaki kuelemika
Mkuu wangu kuhusu healthcare/insurance unaweza izungumzia ujuavyo na sii majibu ulotoa kwa sababu hayawahusu kabisa wapigakura. Na hata viongozi wanaogombea viti vyao wanamkimbia Obama sii kwa sababu wao hawakubaliani ila wanajua fika kwamba wapigakura sehemu zao wanapinga package ya Obama kwa sababu itawagharimu wananchi wapiga kura. hakuna mwananchi mpigakura anayejua kila kitu kilichomo ndani ya package ya Obama ila kile walichoahidiwa.. sasa kwa nini wasimpe kura Obama hali hawakuisoma package nzima wao kujua kimekosekana kitu gani..After all American wapigakura wengi ni wavivu, wajinga na wanaotaka majibu staright to the point..
 
Chama imara cha kisiasa ni lazima kwanza kiwe na muundo thabiti, mtandao mzuri wa kisiasa unaoanzia ngazi moja hadi nyingine pamoja na kuwa na mfumo unaosadifu wa kisera na kiitikadi na kutambulika, achilia mbali kukubaliwa na wananchi.

CHADEMA chama ambacho kwa bahati mbaya sana kimebahatika kukubalika kikanda na kuungwa mkono na kundi la kabila la Kichaga, bado hakijajipanga na kuonekana wazi kama "a real Political Party" ili kuivuta na kuishawishi hadhira kubwa inayoishi vijijini na mijini kwamba wao ndio wanaostahili kuiongoza Tanzania na sio CCM.


Mizizi na nguvu za CCM ni kubwa mno katika nchi yetu, anayepuuza ukweli huu ni mpuuzi jasiri asiyejua kupambanua baina ya mbivu na mbichi, na bila shaka hataki kwa makusudi kujua ukweli wa mambo ulivyo.


Msingi imara wa chama cha TAA ulijengwa kutokana na harakati za machifu wa Tanganyika katika dhati ya kupambana wakiwemo baadhi yao kina Mangi Meli, Kinjikitile, Mirambo, Kimweri, Mkwawa, Makunganya, Bushiri na wengine--wakati kukubalika kwa chama cha TANU ni matokeo ya nguvu na juhudi za chama cha TAA.


Kwa msingi huo kuimarika na kukubalika kwa CCM ni kutokana na kujijenga kwa vyama vya TANU/ASP ambavyo ni vyama viasisi vya siasa katika Tanganyika na Zanzibar tokea miaka ya 1954 na 1957.


CCM inatofauti sana kimtazamo na vyama kama UPC cha Uganda, MCP cha Malawi, na UNIP cha Zambia au KANU kilichokuwa kikitawala Kenya.


Vyama hivi navyo vilikataa kujikita na kuweka mizizi ili kulishika kundi la watu hasa mababa-kwabwela wanaoishi vijijini na kulazimishwa kutambua kwamba mafanikio na ujio wa uhuru wao ulitokana na vyama hivyo.


Kiuhalisia na kinadharia vyama hivyo mara baada ya uhuru vilibadilika na kuwa vyama vya kibwenyenye na kimwinyi kwa kuusahau kabisa kuutazama umma wenye nguvu za maamuzi na utafutaji wa ridhaa ya kudumu (CCM nayo ilijaribu kubadilika lakini sio kwa kasi kubwa ya kutisha kama ilivyokuwa kwa majirani zetu wa Uganda, Kenya, Malawi na Zambia. Shukrani za peee kwa hayati Kambarage Nyerere, mwasisi wa CCM).


Wanaojaribu kuitazama CCM kwa jicho rahisi wafanye pia utafiti mgumu ili kutambua matokeo kamili kabla na baada ya ujio wa vyama vingi huku wakiidurusu kwa weledi hali ya mambo na wakati ulikuwaje kwa nyakati hizo.


TANU haikupata kazi ya suluba ya kujenga matawi mapya toka mwaka 1954 kilipoanzishwa kuanzia kanda ya Mashariki, Lake zone ,Kaskazini na Kusini mwa Tanzania na hatimaye kusambaa nchi nzima, kutokana na kurithi matawi yoye toka kwa chama kikongwe cha TAA.


Kuzaliwa kwa CCM tarehe 5,2,1977 na kuenea kwake ilikuwa ni kama kuua tembo kwa bua kutokana na chama hicho kuiga tabia ya nyoka anayejibua gamba, na yeye kubaki akiwa ni nyoka yuleyule mwenye sumu kali.


TANU iliutumia vizuri mfumo wa chama kimoja na kueneza siasa zake hadi kwenye Taasisi za serikali, mashirika ya Umma, vyuo vikuu, sekondari hadi hata kwenye vikosi vya ulinzi na usalama.


Haikuwa kazi nyepesi inayoweza kuleta hasara haraka au kwa ulaini kama iliyovyazamwa na inavyoendelea kutazamwa na baadhi ya wahariri a mambo ya kisiasa.


Base ya TANU ni TAA. Base ya CCM ni TANU na ASP. CUF inatokana na vuguvugu la KAMAHURU, NCCR -Mageuzi ni mkusanyiko wa wanaharakati waliolilia mageuzi ya Kikatiba tokea miaka ya 1990. Lakini CHADEMA chimbuko lake halisi hasa ni nini na wapi? Au ndiyo ili iliyoelezwa kuwa something like "Chagga Develpement Manifesto"?


Takriban miaka 27 ilipita chini ya chama cha TANU kikiwaimbisha na kuwachezesha kwata wananchi chini ya zama ya nguvu ya chama kushika hatamu tangu pale mfumo wa vyama vingi ulipopigwa marufuku mwaka 1965; fursa na nafasi hii haikutumiwa ipasavyo huko Zambia, Uganda, Malawi na Kenya, na huu ndio ukweli wa mambo, ila anayetaka kubeza hawezi kuzuiwa.


CCM haikulala usingizi wa pono pale ulipoingia mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, ilianzaa kujichimbia kisiasa, kuingiza wanachama wapya, kujinadi mbele ya umma na kuubeza upinzani kwa nguvu ya hoja.


Ni kweli serikali zake zimekuwa zikikabiliwa na matatizo mengi tokea awamu ya kwanza hadi hii ya sasa tuliyonayo--huku chama chenyewe kikijitutumua kwa bidii kulinda hadhi yake na kujivunia rasilimali watu.


Katika awamu ya kwanza mashirika yote ya umma yalifujwa, hakuna aliyefikishwa mahakamani, awamu ya pili walikamatwa watu wakisafirisha dhahabu uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar ess Salaam, kesi ikayeyuka huku katika awamu ya nne tumeshuhudia mikataba mibovu ya madini na wizi katika akaunti ya EPA na BoT ikifanyika katika awamu ya tatu bila hatua zozote za kisheria kuchukuliwa dhidi ya waharifu/husika.


CCM mara kadhaa kimekuwa kikijikosoa na kujipanga kutokana na kupata msaada wa mtandao wake uliojengeka Tanzania nzima kwa miaka mingi.


Vyama vya Tanzania vina pupa ya kutaka kushika madaraka ya juu vianze kwanza kujijenga ndani ya halmashauri za wilaya, Bunge na Baraza la Wawakilishi huku vyenyewe vikitambua mitandao yao ili kupata ushindi ni dhaifu.


Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete imejitahidi kupambana na ubadhirifu wa mali ya umma, kukemea rushwa na kwa bahati nzuri kesi ziko mahakamani zikiwakabili vigogo wazito. Ingawa wengi wa hao wahusika wanataachiwa huru bila kupata adhabu wanayostahii, lakini hilo pekee ni jambo linalowaongezea wananchi mapenzi na hamu ya kuendelea kuiamini CCM, nje ya hilo ukifuatilia utekekezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM toka awamu ya tatu hadi ya nne, Tanzania imepiga hatua (ingawa sio kubwa sana kimaendeleo).


Barabara, zahanati na huduma za maji safi zinatia moyo kinyume na miaka ile mara baada ya kupata Uhuru, vyama vya Bongo vijizatiti, viongozi wake wajitume na wasitegemee wao kuja kufaidi matunda ya nguvu zao, wafanye kama walivyofanya kina Mkwawa na Mangi Meli.


Kuimarika na kujengeka kwa CHADEMA kuna tofauti sana na kujengeka kwa CUF. Chadema mwanzo wake unatokana na safu ya waasisi wa chama hicho. Brown Ngululupwi, Edwin Mtei, Bob Makani, Costa Shinganya, na Kimesera. Hili lilikuwa ni kundi la masetla watupu na halikuwa la wanasiasa waliotambulika na kufanya kazi za kisiasa.


CUF ni chama kilichomega nguvu ya CCM Zanzibar baada ya wanachama wake vigogo wapatao saba walipofukuzwa mwaka 1988 akiwemo Seif Sharif Hamad mtu aliyewahi kuwa Waziri Kiongozi wa SMZ.


Vigogo wengine ni Khatib Hassan Khatib aliyewahi kuwa mhazini wa CCM na MNEC--Hamad Rashid Mohamed ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mambo ya Ndani ya Nchi, Juma Ngwali na Masoud Omar wakiwa wakuu wa Mikoa.


Wanasiasa wengine waliopevuka kisiasa ni pamoja Musa Haji Kombo aliyewahi kuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM, Juma Othman Juma aliyekuwa mjumbe wa NEC, Ali Haji Pandu Waziri wa Sheria katika SMZ, Soud Yusuf Mgeni Waziri wa Kilimo pamoja na Maulid Makame Abdallah aliyewahi kuwa Waziri mdogo wa Afya Zanzibar.


Kundi hili la CUF kwa kiasi kikubwa liliweza kuibana mbavu CCM kutokana na wao kuitambua misingi ya kuunda chama cha siasa na kukieneza kama taasisi.


Nieleweke wazi kwamba sikipigii chapuo chama cha CUF ila nimefanya utafiti na kuiona tofauti kubwa kati ya CCM, CHADEMA na CUF. CHADEMA wajenge kwanza mizizi na kundi lililopo sasa lisitegemee kula matunda ya juhudi hizo.


Chama cha CHADEMA na vingine katika Tanzania vinapaswa kujifunza na kupita katika barabara ya chama cha Liberal Party cha Uingereza amacho hakikuwa na papara ya kushika madaraka haraka bali kilitafuta kwanza amana na hatimaye kikaaminiwa.


CUF wanaelekea kuingia katika medani za serikali Zanzibar baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, hatua hiyo pekee ukiwa mtu mkweli utaweza kujua usahihi wa tathmini yangu.


Bado siamini kutokana na utafiti mdogo nilioufanya kwamba CHADEMA kimejiandaa na kimejijenga kimfumo, kisera na kimtandao kiasi kwamba kiweze kushinda katika uchaguzi wa mwaka huu na kuongoza dola.


Jambo hili kwa CHADEMA sitaki kabisa niliamini moyoni mwangu, naomba lisistawi kabisa kwenye mishipa ya fahamu zangu na kwenye ubongo wangu pia.


CHADEMA hakitashinda kutokana na kwamba bado ni kichanga, kiliwahi kusifiwa na Mwalimu Julius Nyerere kwamba kina sera zenye mwelekeo lakini kina upungufu wa wanasiasa, ni sawa tu na timu ya soka yenye nyota haba wa kuleta ushindi.


Safu ya kina Wilbroad Slaa, Zitto Kabwe, John Mnyika, Halima Mdee, Philemon Ndesamburo, Maulida Komu na Mabere Marando ni kundi la wasomi wa fani za kitaaluma wakikosa mtaji na ujuzi wa mizungu ya ufanyaji wa siasa.


Slaa ni mwanasiasa mahiri, mwepesi wa utambuzi wa mambo, hata kutoka kwake CCM baada ya kukatwa jina lake na kupachikwa kwa Patrick Qorro katika kura za maoni kulilalamikiwa sana na Mwalimu Julius Nyerere.


Slaa ni yeye peke yake kinara ndani ya CHADEMA akizungukwa na timu hafifu isiyo na uwezo ama ukomavu wa kisiasa wa kukiletea ushindi chama hicho. Kwa upande mwingine, CCM bado kina ngome kubwa, viongozi wengi wenye amana mbele ya umma ambao hawakuona umuhimu wa kujitoa ndani ya chama hicho kwa wingi na kujiunga na kambi ya upinzani.


Chadema, NCCR na TLP ni vyama vinavyoweza kuja kujiimarisha katika siku nyingi zijazo usoni, CUF kwa upande wa Bara nao wamo katika msafa wa vyama hivi vitatu, hawajawa na timu imara na pia Kiongozi wake Profesa Ibrahim Lipumba hajaungwa mkono na wasomi wenzake wa Chuo Kikuu cha Dare es Salaam kuonyesha kama anakubalika.


Hata yeye Lipumba anaonekana yuko peke yake. Ni sawa kabisa na kusema mchezaji nyota wa Brazil "Kaka" aamue kusajiliwa na Balimi ya Bukoba kisha timu hiyo ghafla itarajiwe kutandaza kabumbu safi uwanjani, aifungie magoli mengi timu hiyo, hata aiwezeshe ichukue ubingwa wa ligi kuu. Wa-da-nga-yi-ka wenzangu hebu tusijidanganye. Hiyo ni ndoto ya mchana. Hilo haliwezekani kwa mwaka huu na hata baada ya miaka kumi na tano ijayo, CHADEMA isitegemee kushinda kwasababu bado hakijajipanga vizuri.


Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania!


P.S. [makala hii imeandikwa na Antar Sangali, mwandishi wa BongoTz.com]

Kila chama cha siasa ambach kiko kwenye daftari la Tendwa kwa kupata usajili wa kudumu ndio kitakacho kabidhiwa dola mara baada ya kushinda uchaguzi mkuu ambao ni huru, haki na wazi. Nahisi wewe sio Mtanzania halisi!!!!!!!
 
chadema wanataka madaraka hata kwa kupitia umwagaji wa damu wa wananchi!!! Nani atakubali amwage damu yake!! Viongozi wa chadema uongozi haupatikani kwa kutumia nguvu bali hoja!!!

Na damu ya MAALBINO INAYOMWAGIKA KILA SIKU SIO DAMU??? NA DAMU YA WAGONJWA MAHOSPITALINI ANAOKOSA TIBA NZURI WAKATI WAKUBWA WOTE NA WATOTO WAO WANATIBIWA NJE YA NCHI SIO DAMU? DAMU INAYOMWAGIKA KWA VIFO VYA MAPEMA KWA WALALAHOI WATANZANIA SHAURI YA MAISHA YA SHURUBA SIO DAMU????

I just wonder - hivi wewe una comfortable life ya aina gani??? hivi wewe unawajali kweli Watanzania wanaoteseka kwa maisha duni??? Hivi unajua kuna watanzania wanakula mlo mmoja tena hafifu kwa siku????? THINK TWICE BEFORE YOU LEAP...................... akili yako imepumbazika sana ................KUWA KAMA WA - SOUTH AFRIKA WALIOAMUA KUIFIA NCHI YAO BILA KUOGOPA RISASI BALI WALIIMBA NYIMBO ZA UKOMBOZI HADI WALIUPATA UKOMBOZI
seems you are a COWERED!!! au HELA KIDOGO ULIZOHONGWA NDIO ZINAUPOTOSHA UFAHAMU WAKO???? POLE SANA!!!! KUWA MKWELI ......SIMAMA KWENYE HAKI - NDIVYO APENDAVYO MUNGU ALIYEKUUMBA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
tatizo mashabiki wachedema wote ni wagonjwa wa akili hamuwezi kushindana kwa hoja mpaka mtoe matusi. Wachanga wa siasa hamna jipya jifunzeni kujibu kwa nguvu za hoja na sio kutumia hoja za nguvu
 
Naona hatuelewani lugha sasa soma hata hii habari Bofya
Jeez, ona unavyochanganya mambo. Projections nilizokuwa na cite ni za healthcare sio stimulus. Plus, nashangaa umeniwekea article inayozungumzia stimulus package kwenye link uliyoambatanisha instead of healthcare. After all, article yenyewe unayoitoa ni ya Januray 5, 2009 (wakati ambapo Obama alikuwa anajaribu kutafuta compromise na viongozi wa congress kuhusu size ya package). That article is so yesterday mkuu!! Hivi huko uliko hupati latest news? Mkuu, acha tabia ya kugoogle na kupaste kama watoto wa elementary...lol

Hakuna kitu hukukosoa kitu ila mimi ndio nimekukosoa baada ya wewe ulipotosha kuonyesha kuwa independent wana mahusiano na itikadi za Demokratic..Uliandika hivi:- independents wengi wamemkimbia kwasababu the whole wing of democratic part wanaonekana kama wimps fulani (they don't stand in what they believe/wanacompromise mno!). Na sii kweli kwani Independent hawajali compromise za Domecratic ila priority zao kuwezeshwa..
Mkuu either huelewi kabisa politics za marekani zinavyokwenda ama unataka tu kubisha ili usifiwe. Hakuna kitu wamarekani wana-admire (including Independents) kama mtu anayesimama na kutetea kile anachokiamini. Latest polls zilizotoka hivi karibuni zinaonyesha Obama amepata bounce ndogo kwasababu ameanza kusimama na kutetea kile anachokiamini. Na hiyo upward swing kwenye polls imesababishwa in large part na Independents + Liberals ambao walikuwa wameanza kumkimbia kutokana na unnecessary compromise alizokuwa anazifanya na republican.

Mkuu wangu kuhusu healthcare/insurance unaweza izungumzia ujuavyo na sii majibu ulotoa kwa sababu hayawahusu kabisa wapigakura. Na hata viongozi wanaogombea viti vyao wanamkimbia Obama sii kwa sababu wao hawakubaliani ila wanajua fika kwamba wapigakura sehemu zao wanapinga package ya Obama kwa sababu itawagharimu wananchi wapiga kura. ..
Inaelekea wewe unaangalia too much fox news... Ah, vipengele vingi vya healthcare viko very popular kama ulikuwa hujui hilo. Plus, let me tell you something mkuu: Majimbo ya marekani yamegawanyika katika sehemu kuu tatu (Conservative, moderate, and liberal districts). Of course, kuna baadhi ya conservative democrats "blue dogs" wanaotoka kwenye conservative districts hao ndio wanaomkimbia Obama kwasababu districts zao zimejaa wingnuts kibao. Nasema baadhi kwasababu wapo wengine wanaotoka kwenye conservative districts lakini bado wanaedelea kuembrace Obama na hiyo sheria mpya ya healthcare unayosema/taja kuwa wapiga kura hawaipendi. Mfano mzuri ni congressman toka Virginia, Tom Perriello (ukiangalia latest polls hazionyeshi hicho unachokisema: eti 'wapiga kura wanapinga package ya Obama'). It's just a myth mkuu (a media creation thing). Anyway, you have the right to be wrong. And I respect that.
 
Totally agree with you here Ujengelele. But hao watu wako kwenye camp ya Kikwete b/c the alternative [CHADEMA or TLP or CUF or NCCR-MAGEUZI] is even worse... That's all.

Tunapima uhovyo wa CCM kutokana na kutawala NCHI kwa misingi ya wizi wa mali ya umma, kutowajibika, uchumi kulega, n.k Unaposema CHADEMA ni worse umewapima katika nini? Na kumbuka kipimo kiwe sawa na hicho cha CCM.
 
chadema wanataka madaraka hata kwa kupitia umwagaji wa damu wa wananchi!!! Nani atakubali amwage damu yake!! Viongozi wa chadema uongozi haupatikani kwa kutumia nguvu bali hoja!!!

kama vyombo vya usalama vipo,unatakiwa kukamatwa kuisaidia polisi,ili utoe ushahidi wa chadema kuwa tayari kumwaga damu,acheni kauli za kipuzi,tanzania bado itakuwepo bila ya ccm au vyama vya siasa.
 
Unataka kutuambia kuwa CCM ya TAA-TANU na ASP ndo CCM tunayoishuhudia sasa? Wewe ndo unataka kuwafanya Watanzania, Wadanganyika
 
[QUOTE
Jeez, ona unavyochanganya mambo. Projections nilizokuwa na cite ni za healthcare sio stimulus. Plus, nashangaa umeniwekea article inayozungumzia stimulus package kwenye link uliyoambatanisha instead of healthcare. After all, article yenyewe unayoitoa ni ya Januray 5, 2009 (wakati ambapo Obama alikuwa anajaribu kutafuta compromise na viongozi wa congress kuhusu size ya package). That article is so yesterday mkuu!! Hivi huko uliko hupati latest news? Mkuu, acha tabia ya kugoogle na kupaste kama watoto wa elementary...lol
]
[Mkuu wangu sio wewe uloandika hapo chini kwamba hukugusia Healthcare/insurance kwa sababu uloyaandika mwanzo ndio hali halisi ila mimi ndio sitaki kuamii!.. hata hivyo, sijui kama unakumbuka kwamba Mama Clinton alikuwa na healthcare projection yake tofauti na ile Obama wakiwa chama kimoja..Hizi fikra zimeanzia wapi kaa sii kwa kiongozi mwenyewe?..

Siku zote wenzetu wanachokizungumza kuhusu kiongozi ni vision yake ktk maswala iwe Healthcare, Stimulus au muswada wowote unaopelekwa bungeni, kwanza unatokana na vision ya kiongozi na ndio maana wanapiga kura kutafuta mwenye mvuto zaidi ktk undani wa sera zake.

Hata baada ya kuandikwa wapo Democratic ambao wanaweza kutokubaliana na projection hiyo na hakika yupo democratic aliyepinga healthcare ya Obama na ndivyo inavyoitwa hata kama imeandikwa peponi..Kwa hiyo sielewi unachojaribu kubisha hapa..Swala sii kuandikwa bali idea na vision nzima inawakilishwa vipi kwa wananchi wapigakura ambao wanaweza kutokubali hivyo kuathiri kura zake kaa inavyotokea sasa hivi. Hili ndio somo tulokuwa nalo hapa.
Mkuu either huelewi kabisa politics za marekani zinavyokwenda ama unataka tu kubisha ili usifiwe. Hakuna kitu wamarekani wana-admire (including Independents) kama mtu anayesimama na kutetea kile anachokiamini. Latest polls zilizotoka hivi karibuni zinaonyesha Obama amepata bounce ndogo kwasababu ameanza kusimama na kutetea kile anachokiamini. Na hiyo upward swing kwenye polls imesababishwa in large part na Independents + Liberals ambao walikuwa wameanza kumkimbia kutokana na unnecessary compromise alizokuwa anazifanya na Republican.
Bado unarudia yaleyale.. Kwa mgombea kuamini kile unachokiamini hakihusiani na Independet voters, They care most kile wanachokijali wao umekisimamia vipi (their interwest or priority cames first na sii hadithi nyingine..


Haya maswala ya mtu kuwa na msimamo yapo pande zote iwe Republican au Democtratic na wala sio Marekani tu ila sunia nzima hakuna mpigakura anayependa kiongozi asiyekuwa na msimamo hata sisi tunampiunga JK kwa sababu hana msimamo. Swala la Obama kurudisha umaarufu haitokani na kura za Independent bali Demnoctic wenyewe wanamwona akisimama imara na kujibu mapigo. Na itachukua nguvu kubwa zaidi kuzungumzia maswala yao na kuonyesha uwezo wake ktk maswala yao (independent) ndipo wanaweza kurtudisha imani yao.

Listen mkuu wangu, JK akinambia kesho kwamba Lowassa, Mkapa, Mramba, Karamagi na wengine wote wanatinga mahakamani - amini maneno yangu wapo watu wengi sana watabadilisha kura zao. Sasa kutokuwa na uhakika ni kiongozi gani wanamhitaji hadi sasa kunatokana na wagombea wote kutowaahidi ku deal na tatizo lao ndicho kinachowafanya kuwa independent. Kama unamkumbuka Lou Dobbs alikuwa akijiita Independent kwa sababu tu ya chuki yake na Immigrant hasa kutoka Mexico hali akitetea kwa mbali Demokratic (Pro Clinton against Obama).. ndivyo Independent wengine wanapatikana..
Inaelekea wewe unaangalia too much fox news... Ah, vipengele vingi vya healthcare viko very popular kama ulikuwa hujui hilo. Plus, let me tell you something mkuu: Majimbo ya marekani yamegawanyika katika sehemu kuu tatu (Conservative, moderate, and liberal districts). Of course, kuna baadhi ya conservative democrats "blue dogs" wanaotoka kwenye conservative districts hao ndio wanaomkimbia Obama kwasababu districts zao zimejaa wingnuts kibao. Nasema baadhi kwasababu wapo wengine wanaotoka kwenye conservative districts lakini bado wanaedelea kuembrace Obama na hiyo sheria mpya ya healthcare unayosema/taja kuwa wapiga kura hawaipendi. Mfano mzuri ni congressman toka Virginia, Tom Perriello (ukiangalia latest polls hazionyeshi hicho unachokisema: eti 'wapiga kura wanapinga package ya Obama'). It's just a myth mkuu (a media creation thing). Anyway, you have the right to be wrong. And I respect that.
Mkuu wangu nimekwambia hatuzungumzii Politics za Republican na Democratic bali jinsi gani wananchi wana ondoa imani yao kwa Obama hasa ktk swala la Helthcare pamoja na kwamba ndio njia. Hata mimi binafsi naiunga mkono tena naweza sema ingekuwa bure kabisaaa kama hapa Canada kwa sababu Marekani can afford it. Silaha kubwa ya Teaparty ni Healthcare ya Obama na wamepata wafuasi wengi tu tena wanatisha, hivyo kama wewe umemwona Tom Perriello akifanya vizuri basi elewa pia wapo wagombea kibao wa Democratric wanaipinga Healthcare package ya Obama baada ya kuipitisha wao na kujisogeza mbali kama vile wao hawahusiki..

Hii ni mbinu ya kisiasa haina maana yeyote kwetu isipokuwa tunazungumzia jinsi gani imekuwa sababu ya Obama kushuka ktk kura za maoni ikiwa ni pamoja na Uchumi ambao nimesema kwa mpiga kura anachojali yeye ni Ajira. Hawa watu wameisha endelea sii walokwama kama sisi tukisubiri misaada kama refugees, hivyo mwisho wa siku kiongozi mzuri kwao ni yule anayeweza kuongeza ajira..

Kama wewe unapinga kwamba ajira sii muhimu bali ni jukumu la wananchi kujitafutia jinsi ya kujiajiri, nadhani hakuna sababu ya kuendelea kulumbana hali tunatofautiana ktk mtazamo na ndivyo CCM na Chadema wanavyotofautiana ktk vipaumbele vyao au Kikwete na Kigoda ama Dr.Slaa.
 
..................... Yeah, wewe na wasomi wachache hapa JF mnaweza kuwa mmelizika na sera za Chadema na mko very ethused na candidancy ya Dr. Slaa, lakini ukweli ni kwamba, sio watanzania wote wanoshare the same enthusiasm.

Have you ever heard of something called "Editor in Chief"...? Kama unajua maana yake/responsibilities zake, then utajua ni kwanini na defend hii article kwa nguvu zote, ingawa mwandishi wake ni Antar Sangali.

mmh......Editor in Chief.......haya bana.............ungekosea herufi............ningeelewa..............lakini hiyo hata huwezi kusingizia "mothertongue imekuathiri"..............Mr./Ms/Mrs. Editor in Chief.............
 
tatizo mashabiki wachedema wote ni wagonjwa wa akili hamuwezi kushindana kwa hoja mpaka mtoe matusi. Wachanga wa siasa hamna jipya jifunzeni kujibu kwa nguvu za hoja na sio kutumia hoja za nguvu

I beg to differ with you!!
 
Hangover ya siasa za kikomunisti Tanzania itachukua muda kuisha. Wafuasi wengi wa CCM wamebaki wakiamini katika mfumo na enzi za chama kushika hatamu na kuwa na terror network iliyozagaa nchi nzima kwa lengo la kuwatisha watu. Of course CCM bado ina hang kwenye hiyo terror network ya Kikomunisti iliyojengwa kipindi hicho. Lakini ukweli sasa hivi ni kuwa chama hakina control kwenye hiyo terror network kutokana na wananchi wengi kuikataa. The network is still there, lakini ni kujidanganya kuwa mtandao huo ndo nguvu ya chama tawala chenye legacy ya sera za kikomunisti.

Uongozi wa nchi unafuata katiba na sheria na nchi inahitaji serikali ndogo tu iliyo na ufanisi. Tanzania hata mawaziri wanane tu wanatosha! Wizara zote zinamfumo wa utendaji hadi katika low level. Chama kinatakiwa kuwa na sera na mwelekeo, mtazamo na uwezo wa kuleta maendeleo kwa watanzania, hata kama ni chama kidogo tu. Chama chote hakiingii serikalini, bali kinakuwepo juu kwa ajili ya kudhibiti mwenendo wa kiutendaji wa serikali na kuhakikisha kuwa serikali ina archieve kile kinachotakiwa.

Kuweza kufanya hayo utagundua kuwa chama hakihitajiki kuwa na mtandao mkubwa unao-mimic mtandao wa serikali. Mfumo mkubwa wa chama tawala ni sehemu ya extension ya chama ku-control serikali, ambayo ni mazagazaga ya mifumo ya kikomunisti. Bongo TZ bado anaamini kuwa kwa chama chochote kuingia madarakani kinatakiwa kuwa na mfumo wa kikomunisti, uliozagaa nchi nzima kuhakikisha kuwa wananchi hawapati nafasi ya kukisema vibaya chama? Mfumo huo bado uko China, Korea kaskazini na Cuba. Hapa bongo, vyama vingine havihitaji kuiga aina hiyo ya mifumo mufilis ambayo ni liability kubwa kwa wananchi!
 
Sasa hivi challenge kubwa aliyo nayo JK ni kudhibiti mtandao mkubwa wa Chama cha Kikomunisti na Kuongoza serikali; ni kama vile anaongoza serikali mbili. Mtandao wa chama cha kikomunisti unahakikisha kuwa unadhibiti serikali kwa upande mmoja, vile vile kuwadhibiti wananchi kwa upande wa pili, kuhakikisha kuwa wananchi hawapati nafasi ya kufikiria na kutenda kinyume na vile chama kinataka. Ndo maana chama inabidi kiwe na mtandao mkubwa hasa mashinani huko waliko wananchi ili kuwadhibiti (na si kuwahamasisha).

Mtandao wa CCM (serikali ya pili kivuli) umeshakosa mwelekeo, Umejikita katika ufisadi, rushwa, ukachero uchwara na jinai zisizomithirika. Machafu hayo yote yanaufanya mfumo huo usiwe wa kutegemewa bali bomu linalosubiri kumlipukia kiongozi wa mfumo huo! Naam, kama chama cha kikomunisti huko Urusi kilivyowalipukia viongozi wao wakati ule (Kina Gorberchev). Hali ndo ilivyo sasa hivi kwa Kikwete. Mtandao wa kigaidi wa CCM ni kitisho kwake hasa, kwani sasa hivi mtandao ule umegawanyika vibaya na ni vigumu kujua ni nani amesimamia wapi.

Tiba kwa CCM ni kufanya mageuzi makubwa ya kuifanya CCM kiwe chama cha wananchi na si chama Mtandao kinachotegemea urasimu na mfumo wa uendeshaji unaoijaribu ku-rudufu serikali. Chama kikubwa namna hiyo ni mzigo mkubwa kwa wananchi maskini wa Tanzania na ni balaa kubwa kwa ustawi wao.

Vyama vya upinzani asilani visiige mfumo na mtandao huo wa ki-CCM ambao ni masalia ya mfumo tawala wa Kikomunisti tuliokuwa nao hapo nyuma.
 
Kwa hiyo kina Bongo Tz wanaoshabikia mfumo na mtandao dhalimu wa CCM ambao umekuwa ni kaburi kubwa la kuzikia mapato kiduchu ya mlalahoi wa bongo, na waendelee kulala katika usingizi wao na kuendelea kuota njozi za kutukuza mtandao. Ila wajue kuwa mtandao huo badala ya kukwajenga huko mashinani unawabomoa zaidi kwani malengo ya kuwepo kwa mfumo huo (kuwadhibiti watu) sasa hivi hayatekelezeki tena. Wananchi walishakataa kudhibitiwa na wako huru zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom