Pupa ya kutaka kushika madaraka, itaiangusha CHADEMA tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pupa ya kutaka kushika madaraka, itaiangusha CHADEMA tena

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BongoTz, Oct 4, 2010.

 1. BongoTz

  BongoTz JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 272
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chama imara cha kisiasa ni lazima kwanza kiwe na muundo thabiti, mtandao mzuri wa kisiasa unaoanzia ngazi moja hadi nyingine pamoja na kuwa na mfumo unaosadifu wa kisera na kiitikadi na kutambulika, achilia mbali kukubaliwa na wananchi.

  CHADEMA chama ambacho kwa bahati mbaya sana kimebahatika kukubalika kikanda na kuungwa mkono na kundi la kabila la Kichaga, bado hakijajipanga na kuonekana wazi kama "a real Political Party" ili kuivuta na kuishawishi hadhira kubwa inayoishi vijijini na mijini kwamba wao ndio wanaostahili kuiongoza Tanzania na sio CCM.


  Mizizi na nguvu za CCM ni kubwa mno katika nchi yetu, anayepuuza ukweli huu ni mpuuzi jasiri asiyejua kupambanua baina ya mbivu na mbichi, na bila shaka hataki kwa makusudi kujua ukweli wa mambo ulivyo.


  Msingi imara wa chama cha TAA ulijengwa kutokana na harakati za machifu wa Tanganyika katika dhati ya kupambana wakiwemo baadhi yao kina Mangi Meli, Kinjikitile, Mirambo, Kimweri, Mkwawa, Makunganya, Bushiri na wengine--wakati kukubalika kwa chama cha TANU ni matokeo ya nguvu na juhudi za chama cha TAA.


  Kwa msingi huo kuimarika na kukubalika kwa CCM ni kutokana na kujijenga kwa vyama vya TANU/ASP ambavyo ni vyama viasisi vya siasa katika Tanganyika na Zanzibar tokea miaka ya 1954 na 1957.


  CCM inatofauti sana kimtazamo na vyama kama UPC cha Uganda, MCP cha Malawi, na UNIP cha Zambia au KANU kilichokuwa kikitawala Kenya.


  Vyama hivi navyo vilikataa kujikita na kuweka mizizi ili kulishika kundi la watu hasa mababa-kwabwela wanaoishi vijijini na kulazimishwa kutambua kwamba mafanikio na ujio wa uhuru wao ulitokana na vyama hivyo.


  Kiuhalisia na kinadharia vyama hivyo mara baada ya uhuru vilibadilika na kuwa vyama vya kibwenyenye na kimwinyi kwa kuusahau kabisa kuutazama umma wenye nguvu za maamuzi na utafutaji wa ridhaa ya kudumu (CCM nayo ilijaribu kubadilika lakini sio kwa kasi kubwa ya kutisha kama ilivyokuwa kwa majirani zetu wa Uganda, Kenya, Malawi na Zambia. Shukrani za peee kwa hayati Kambarage Nyerere, mwasisi wa CCM).


  Wanaojaribu kuitazama CCM kwa jicho rahisi wafanye pia utafiti mgumu ili kutambua matokeo kamili kabla na baada ya ujio wa vyama vingi huku wakiidurusu kwa weledi hali ya mambo na wakati ulikuwaje kwa nyakati hizo.


  TANU haikupata kazi ya suluba ya kujenga matawi mapya toka mwaka 1954 kilipoanzishwa kuanzia kanda ya Mashariki, Lake zone ,Kaskazini na Kusini mwa Tanzania na hatimaye kusambaa nchi nzima, kutokana na kurithi matawi yoye toka kwa chama kikongwe cha TAA.


  Kuzaliwa kwa CCM tarehe 5,2,1977 na kuenea kwake ilikuwa ni kama kuua tembo kwa bua kutokana na chama hicho kuiga tabia ya nyoka anayejibua gamba, na yeye kubaki akiwa ni nyoka yuleyule mwenye sumu kali.


  TANU iliutumia vizuri mfumo wa chama kimoja na kueneza siasa zake hadi kwenye Taasisi za serikali, mashirika ya Umma, vyuo vikuu, sekondari hadi hata kwenye vikosi vya ulinzi na usalama.


  Haikuwa kazi nyepesi inayoweza kuleta hasara haraka au kwa ulaini kama iliyovyazamwa na inavyoendelea kutazamwa na baadhi ya wahariri a mambo ya kisiasa.


  Base ya TANU ni TAA. Base ya CCM ni TANU na ASP. CUF inatokana na vuguvugu la KAMAHURU, NCCR -Mageuzi ni mkusanyiko wa wanaharakati waliolilia mageuzi ya Kikatiba tokea miaka ya 1990. Lakini CHADEMA chimbuko lake halisi hasa ni nini na wapi? Au ndiyo ili iliyoelezwa kuwa something like "Chagga Develpement Manifesto"?


  Takriban miaka 27 ilipita chini ya chama cha TANU kikiwaimbisha na kuwachezesha kwata wananchi chini ya zama ya nguvu ya chama kushika hatamu tangu pale mfumo wa vyama vingi ulipopigwa marufuku mwaka 1965; fursa na nafasi hii haikutumiwa ipasavyo huko Zambia, Uganda, Malawi na Kenya, na huu ndio ukweli wa mambo, ila anayetaka kubeza hawezi kuzuiwa.


  CCM haikulala usingizi wa pono pale ulipoingia mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, ilianzaa kujichimbia kisiasa, kuingiza wanachama wapya, kujinadi mbele ya umma na kuubeza upinzani kwa nguvu ya hoja.


  Ni kweli serikali zake zimekuwa zikikabiliwa na matatizo mengi tokea awamu ya kwanza hadi hii ya sasa tuliyonayo--huku chama chenyewe kikijitutumua kwa bidii kulinda hadhi yake na kujivunia rasilimali watu.


  Katika awamu ya kwanza mashirika yote ya umma yalifujwa, hakuna aliyefikishwa mahakamani, awamu ya pili walikamatwa watu wakisafirisha dhahabu uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar ess Salaam, kesi ikayeyuka huku katika awamu ya nne tumeshuhudia mikataba mibovu ya madini na wizi katika akaunti ya EPA na BoT ikifanyika katika awamu ya tatu bila hatua zozote za kisheria kuchukuliwa dhidi ya waharifu/husika.


  CCM mara kadhaa kimekuwa kikijikosoa na kujipanga kutokana na kupata msaada wa mtandao wake uliojengeka Tanzania nzima kwa miaka mingi.


  Vyama vya Tanzania vina pupa ya kutaka kushika madaraka ya juu vianze kwanza kujijenga ndani ya halmashauri za wilaya, Bunge na Baraza la Wawakilishi huku vyenyewe vikitambua mitandao yao ili kupata ushindi ni dhaifu.


  Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete imejitahidi kupambana na ubadhirifu wa mali ya umma, kukemea rushwa na kwa bahati nzuri kesi ziko mahakamani zikiwakabili vigogo wazito. Ingawa wengi wa hao wahusika wanataachiwa huru bila kupata adhabu wanayostahii, lakini hilo pekee ni jambo linalowaongezea wananchi mapenzi na hamu ya kuendelea kuiamini CCM, nje ya hilo ukifuatilia utekekezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM toka awamu ya tatu hadi ya nne, Tanzania imepiga hatua (ingawa sio kubwa sana kimaendeleo).


  Barabara, zahanati na huduma za maji safi zinatia moyo kinyume na miaka ile mara baada ya kupata Uhuru, vyama vya Bongo vijizatiti, viongozi wake wajitume na wasitegemee wao kuja kufaidi matunda ya nguvu zao, wafanye kama walivyofanya kina Mkwawa na Mangi Meli.


  Kuimarika na kujengeka kwa CHADEMA kuna tofauti sana na kujengeka kwa CUF. Chadema mwanzo wake unatokana na safu ya waasisi wa chama hicho. Brown Ngululupwi, Edwin Mtei, Bob Makani, Costa Shinganya, na Kimesera. Hili lilikuwa ni kundi la masetla watupu na halikuwa la wanasiasa waliotambulika na kufanya kazi za kisiasa.


  CUF ni chama kilichomega nguvu ya CCM Zanzibar baada ya wanachama wake vigogo wapatao saba walipofukuzwa mwaka 1988 akiwemo Seif Sharif Hamad mtu aliyewahi kuwa Waziri Kiongozi wa SMZ.


  Vigogo wengine ni Khatib Hassan Khatib aliyewahi kuwa mhazini wa CCM na MNEC--Hamad Rashid Mohamed ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mambo ya Ndani ya Nchi, Juma Ngwali na Masoud Omar wakiwa wakuu wa Mikoa.


  Wanasiasa wengine waliopevuka kisiasa ni pamoja Musa Haji Kombo aliyewahi kuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM, Juma Othman Juma aliyekuwa mjumbe wa NEC, Ali Haji Pandu Waziri wa Sheria katika SMZ, Soud Yusuf Mgeni Waziri wa Kilimo pamoja na Maulid Makame Abdallah aliyewahi kuwa Waziri mdogo wa Afya Zanzibar.


  Kundi hili la CUF kwa kiasi kikubwa liliweza kuibana mbavu CCM kutokana na wao kuitambua misingi ya kuunda chama cha siasa na kukieneza kama taasisi.


  Nieleweke wazi kwamba sikipigii chapuo chama cha CUF ila nimefanya utafiti na kuiona tofauti kubwa kati ya CCM, CHADEMA na CUF. CHADEMA wajenge kwanza mizizi na kundi lililopo sasa lisitegemee kula matunda ya juhudi hizo.


  Chama cha CHADEMA na vingine katika Tanzania vinapaswa kujifunza na kupita katika barabara ya chama cha Liberal Party cha Uingereza amacho hakikuwa na papara ya kushika madaraka haraka bali kilitafuta kwanza amana na hatimaye kikaaminiwa.


  CUF wanaelekea kuingia katika medani za serikali Zanzibar baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, hatua hiyo pekee ukiwa mtu mkweli utaweza kujua usahihi wa tathmini yangu.


  Bado siamini kutokana na utafiti mdogo nilioufanya kwamba CHADEMA kimejiandaa na kimejijenga kimfumo, kisera na kimtandao kiasi kwamba kiweze kushinda katika uchaguzi wa mwaka huu na kuongoza dola.


  Jambo hili kwa CHADEMA sitaki kabisa niliamini moyoni mwangu, naomba lisistawi kabisa kwenye mishipa ya fahamu zangu na kwenye ubongo wangu pia.


  CHADEMA hakitashinda kutokana na kwamba bado ni kichanga, kiliwahi kusifiwa na Mwalimu Julius Nyerere kwamba kina sera zenye mwelekeo lakini kina upungufu wa wanasiasa, ni sawa tu na timu ya soka yenye nyota haba wa kuleta ushindi.


  Safu ya kina Wilbroad Slaa, Zitto Kabwe, John Mnyika, Halima Mdee, Philemon Ndesamburo, Maulida Komu na Mabere Marando ni kundi la wasomi wa fani za kitaaluma wakikosa mtaji na ujuzi wa mizungu ya ufanyaji wa siasa.


  Slaa ni mwanasiasa mahiri, mwepesi wa utambuzi wa mambo, hata kutoka kwake CCM baada ya kukatwa jina lake na kupachikwa kwa Patrick Qorro katika kura za maoni kulilalamikiwa sana na Mwalimu Julius Nyerere.


  Slaa ni yeye peke yake kinara ndani ya CHADEMA akizungukwa na timu hafifu isiyo na uwezo ama ukomavu wa kisiasa wa kukiletea ushindi chama hicho. Kwa upande mwingine, CCM bado kina ngome kubwa, viongozi wengi wenye amana mbele ya umma ambao hawakuona umuhimu wa kujitoa ndani ya chama hicho kwa wingi na kujiunga na kambi ya upinzani.


  Chadema, NCCR na TLP ni vyama vinavyoweza kuja kujiimarisha katika siku nyingi zijazo usoni, CUF kwa upande wa Bara nao wamo katika msafa wa vyama hivi vitatu, hawajawa na timu imara na pia Kiongozi wake Profesa Ibrahim Lipumba hajaungwa mkono na wasomi wenzake wa Chuo Kikuu cha Dare es Salaam kuonyesha kama anakubalika.


  Hata yeye Lipumba anaonekana yuko peke yake. Ni sawa kabisa na kusema mchezaji nyota wa Brazil "Kaka" aamue kusajiliwa na Balimi ya Bukoba kisha timu hiyo ghafla itarajiwe kutandaza kabumbu safi uwanjani, aifungie magoli mengi timu hiyo, hata aiwezeshe ichukue ubingwa wa ligi kuu. Wa-da-nga-yi-ka wenzangu hebu tusijidanganye. Hiyo ni ndoto ya mchana. Hilo haliwezekani kwa mwaka huu na hata baada ya miaka kumi na tano ijayo, CHADEMA isitegemee kushinda kwasababu bado hakijajipanga vizuri.


  Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania!


  P.S. [makala hii imeandikwa na Antar Sangali, mwandishi wa BongoTz.com]
   
 2. M

  Masauni JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mjinga ni wewe tena usiye na akili ya kufikiri.Uchambuzi wako ni wa kipumbavu tena umejaa hila na ufisadi.
   
 3. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Acha ubabaishaji mkuu, yaani unadhani watanzania bado wataendelea kudanganyika na makala yako ndefu iliyojaa chuki binafsi!!!. Huo umakini wa CCM uko wapi???, hao unaowaita viongozi wazuri wa CCM ya leo ndio akina nani?
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  umeenda shule hata kidogo? Go back to school to jeck up your sleepind brain bro. Badilika kifikra . Loh
   
 5. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  chadema wanataka madaraka hata kwa kupitia umwagaji wa damu wa wananchi!!! Nani atakubali amwage damu yake!! Viongozi wa chadema uongozi haupatikani kwa kutumia nguvu bali hoja!!!
   
 6. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 7. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  hivi wewe mpaka utukane huoni raha? Umeishiwa hoja? Si uombe msaada wa kujengewa hoja ili ujibu challenge uliyopewa hapo juu? Ndio maana ccm wamekataa kuhudhuria midahalo wanajuwa chadema wameshikwa na ugonjwa wa kichaa cha ikulu!!!
   
 8. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 9. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  ????????????????????????????????????????
   
 10. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 11. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 12. E

  Estmeed Reader Senior Member

  #12
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema ina umbali mrefu wa kwenda...kuwapata akina mama!

  Women Power hakuna ndani ya Chadema!
   
 13. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  hata huyu amekubaliana nawe:

  [​IMG]
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  BongoTz,
  Mkuu wangu nyakati hizo zimepitwa na wakati.. Sasa hivi chama ni sera zake ambazo zinakubaliwa na wananchi wake kwa wingi. Enzi za Kikomunist ati chama kimeshika hatamu zimepita, huu ni wakati Katiba inayoongoza nchi haina mwenyewe na sote tunafuata Katiba na sio chama..

  Leo hii Nguvu ya chama ni ushawishi wa sera zake kuuzika kwa wananchi kama vile unapeleka mazao yako sokoni. Ondoa kabisa yale mawazo ya wakati wa TANU ambayo watu walilazimika kuchagua TANU kwa sababu ndiye mtunzi wa katiba na mmliki wa njia kuu zote za uchumi na kila kitu..

  Maadam system nzima ya kiutawala itamkubali mgombea fulani kuwa rais wao haijalishi tena nguvu ya chama kwani CCM sio Katiba ya nchi kiasi kwamba Majeshi yetu na Usalama lazima washiriki kupinga matokeo ya uchaguzi kwa sababu tu Chaderma sii imara kama CCM. Swala ni nani anayekubalika zaidi kwa wananchi kwa sera zake - Period!

  Hofu kubwa ya Chadema na wananchi ni kama system (na majeshi yetu) haitamkubali Dr.Slaa baada ya ushindi lakini kama wao watampokea yeyote aloshinda basi CCM na JK hawana nguvu ya kufanya lolote dhidi ya vyombo hivi. Hofu yangu kubwa ipo hapo na sio CCM wala mtu mmoja kwani hata JK analindwa na katiba.
   
 15. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  "Mizizi na nguvu za CCM ni kubwa mno katika nchi yetu, anayepuuza ukweli huu ni mpuuzi jasiri asiyejua kupambanua baina ya mbivu na mbichi, na bila shaka hataki kwa makusudi kujua ukweli wa mambo ulivyo"

  Kadogoo unadhani Watanzania ni mabumbuwazi? Mizizi hiyo unayotaja imeenea na kuwa na nguvu ndiyo inayoimaliza CCM. Kwa taarifa yako ni kuwa CCM inafahamika kuwa Chama Cha Mafisadi hadi huko vijijini, kule yalikofika matawi yake na inaelekea kuporomoka huko. Nadhani unachotuambia sicho ambacho kipo bali unachotaka watu wajue, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba CCM imechuja. Kama kweli CCM inafahamika inakuweje Mgombea wake wa urais ajitengenezee mabango makubwa utafikiri bidhaa mpya inayoingia kwenye soko, au Chama kuwasomba watu kwenye mkutano wa kampeni kwa faida ipi? kama watu wana mapenzi na CCM kwanini wasiende kwa gharama zao kwenye mkutano?
   
 16. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  Ishi kwa Historia, na kujiamini kwamba kwa sababu CCM ina matawi hadi kwenye vitongoji, then ndiyo chama pekee kinachoweza kuongoza dola sasa suburi ushangae hii ni 2010. Hayo matawi ndiyo yatapiga kura this time. Watanzania si wale wa miaka ya 70 hadi 90. Sasa hivi kuna mabadiliko makubwa sana ndani ya miaka 5 tu hii iliyopita. Tatizo CCM hamsomi alama za nyakati.

  Huwezi kuwarudisha watu nyuma kama wanataka mabadiliko, huu ni mfumo gani unaojivunia? mfuno ulioshindwa kuwaletea wananchi hata chembe ya maendeleo?

  Unajua kusimama na kuitetea CCM hadharani lazima uwe na matatizo makubwa ndani ya ubongo, Chama gani hiki ambacho kinasema uwongo kwa umma? Wananchi wameshastuka na wamechoka, maisha magumu, ahadi hazitekelezwi, wizi wa mali za umma unazidi, kusimamia miradi ya maendeleo hakuna, Raslimari za taifa zinaporwa, Matanuzi makubwa ya pesa za umma serikalini, Miundombinu imebinafishishwa kwa ufisadi wa kimataifa - leo hii ndugu unasimama kutetea eti CCM eti ina misingi ya TANU na ISP? kweli?

  Jamani ifike mahala tuweke uzalendo mbele na tuache fitna, hatutaendea kamwe kwa kukumbatiana, watoto wetu watarithi nini katika nchi hii kama mambo yote yako hovyo hovyo? tunajenga taifa la wajinga, taifa la watu woga ni hatari sana.
   
 17. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  'Msingi imara wa chama cha TAA ulijengwa kutokana na harakati za machifu wa Tanganyika katika dhati ya kupambana wakiwemo baadhi yao kina Mangi Meli, Kinjikitile, Mirambo, Kimweri, Mkwawa, Makunganya, Bushiri na wengine--wakati kukubalika kwa chama cha TANU ni matokeo ya nguvu na juhudi za chama cha TAA.'

  Unataka kutufanya kama hatufahamu historia? T.A.A. (Tanganyika African Association) kilikuwa ni jumuia ya kujadili mambo mbali mbali ya kijamii mjini Dar es salaam. Wanachama wake wa awali walikuwa wakazi wa Dar ambao chama hicho kilikuwa ni kama club. Katika kufanya hivyo, wakajikuta wakielekea kwenye kuongea zaidi kutaka ukombozi wa mwafrika zama zile. Baadae ndipo kikabadilishwa na kuwa TANU. Si lazima chama cha siasa kianza rasmi kwa wadhifa huo, kuna mifano mingi tu, kwa mfano vyama vya wafanyakazi.

  Hivyo basi, Chadema, au shirikisho la watu wengine wale, wakiungana na wakiwa na malengo yanayofanana wanaweza kuwa na chama chao cha siasa. Hakuna chama kilichoundwa kikiwa tayari kinajua nyanja zote za kiuendeshaji kwa vile muundo wa chama na matokeo yake hutegemea vigezo vingi. Kusema kuwa ccm ndio chama tu kinachoweza kuongoza, huko ni kugandwa kwa wakati kwani ccm kimejiharibu chenyewe (self destruct) kutokana na kutoangalia na kufuata misingi ya kuanzishwa kwake. Itokeapo katika jamii ya kisiasa kuwa chama kinajiharibu chenyewe, matokeo halisi (logical conclusion) yake ni kutokea kwa vyama vingine ambavyo vitatekeleza matakwa ya watu wake.
   
 18. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #18
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  :preggers::preggers::preggers:
   
 19. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  CCM original wenyewe wamechoka,wamekaa kimya maana wanajua chama chao kimevamiwa na mafisadi.Ili kuonesha uzalendo wanapigia kura upinzani.Wewe mganga njaa ndo bado unapiga kelele.
   
 20. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  NI nguvu gani hiyo unayoiongelea ambayo chadema wanaitumia?Lingekuwa jambo la busara umshauri mgonjwa wenu kuwa kama yuko kwenye final stages basi asubiri muda wake aondoke kwa amani asitake kusomba na wengine wasio na hatia.Asituletee mabalaa hapa......
   
Loading...