Puma Energy (Tz) hivi karibuni ilinunua hisa toka kwa BP (Tz) na hivyo kuchukua vituo vya kuuza mafuta toka kwa ilizokuwa BP (Tz). Jana, jumapili tarehe 18 Novemba mida ya kama saa 2 na nusu hivi asubuhi, nilipata shida ya gari yangu kukata mafuta ghafula nikiwa barabara ya Ally Hassan Mwinyi karibu kabisa na Red Cross. Ili kuondoa usumbufu kwa madereva wengine, mimi na familia yangu tukaona tulisukume gari hadi kituo cha mafuta cha Puma ambacho hakikuwa mbali toka hapo. Mi nikawaomba wahusika pale kwenye hicho ktuo niache gari kwa muda wakati namtafuta fundi aje alishughulikie. Wale waheshimiwa wakakataa kata kata. Nilishangaywa na kupigwa butwaa, kwani eneo lao ni kubwa na mimi nilipatwa na emergency, kitu ambacho sikukipangia. Na hao jamaa walituona mimi na mke wangu na mtoto wa kiume tukihangaika kusukuma lile gari. Lakini, licha ya kutosaidia hata kidogo hata kuegesha gari pale kwa muda wlikataa kata kata. Hawa ndio investors tunaowakaribisha Tanzania, ambao wala hawawathamini Watanzania isipokuwa tu pale unaponunua mafuta. Hayo ndiyo tutegemee toka Puma Energy (Tanzania).