Puma Energy (Tanzania) – Haya Ndiyo Tutegemee?

F

Fresh Air

Member
Joined
Jun 9, 2011
Messages
23
Points
0
F

Fresh Air

Member
Joined Jun 9, 2011
23 0
Puma Energy (Tz) hivi karibuni ilinunua hisa toka kwa BP (Tz) na hivyo kuchukua vituo vya kuuza mafuta toka kwa ilizokuwa BP (Tz). Jana, jumapili tarehe 18 Novemba mida ya kama saa 2 na nusu hivi asubuhi, nilipata shida ya gari yangu kukata mafuta ghafula nikiwa barabara ya Ally Hassan Mwinyi karibu kabisa na Red Cross. Ili kuondoa usumbufu kwa madereva wengine, mimi na familia yangu tukaona tulisukume gari hadi kituo cha mafuta cha Puma ambacho hakikuwa mbali toka hapo. Mi nikawaomba wahusika pale kwenye hicho ktuo niache gari kwa muda wakati namtafuta fundi aje alishughulikie. Wale waheshimiwa wakakataa kata kata. Nilishangaywa na kupigwa butwaa, kwani eneo lao ni kubwa na mimi nilipatwa na emergency, kitu ambacho sikukipangia. Na hao jamaa walituona mimi na mke wangu na mtoto wa kiume tukihangaika kusukuma lile gari. Lakini, licha ya kutosaidia hata kidogo hata kuegesha gari pale kwa muda wlikataa kata kata. Hawa ndio investors tunaowakaribisha Tanzania, ambao wala hawawathamini Watanzania isipokuwa tu pale unaponunua mafuta. Hayo ndiyo tutegemee toka Puma Energy (Tanzania).
 
A

abubakar2012

New Member
Joined
Nov 21, 2012
Messages
1
Points
0
Age
42
A

abubakar2012

New Member
Joined Nov 21, 2012
1 0
Tunasikitika yaliotokea, tunayafanyia uchunguzi wa kina, suala la mteja kusukuma gari kituoni , lazima apewe msaada ikiwa Pump Attendants hawapo busy na mteja.
kwa hali yako, uliokuwa nayo na familia.. tutapenda uje kututembelea siku za kazi, maana tumejearibu kukaa na wafanyakazi wote (all shifts,) kila mmoja anasema haijatokea akiwa yeye siku hio... tutashukuru tukipata utembezi wako na tutazidi kuboresha huduma yetu

Asante
PUMA UPANGA SERVICE STATION
 
bwegebwege

bwegebwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2010
Messages
1,037
Points
1,195
bwegebwege

bwegebwege

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2010
1,037 1,195
Ni kawaida, mnaajiri watu hata hamuwapi Training ya kujua nini chaweza kutokea na ni nini waweze kufanya wakati huo! Mtu napatwa na tatizo hata msaada hapewi, hata kuulizwa haulizwi, anakataliwa msaada tu!! Ukiuliza utaambiwa " ndiohivyo, hapa haparusiswi kupaki etc", au "uongozi umekataza"...ukimwambia niitie basi huyo kiongozi unajibiwa majibu ya mavi.....

Lakini ingekuwa gari la MZUNGU mngeenda kumchekea! Au wakisimama polisi, hata kama wanatongoza mwanamke mnawachekea tu....
 
Mupirocin

Mupirocin

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Messages
1,681
Points
1,250
Mupirocin

Mupirocin

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2011
1,681 1,250
watanzania tunatatizo la poor customer care, hii unaweza kuta si wale wamiliki wa kampuni bali ni sisi wenyewe watanzania. tatizo hili la huduma kwa mteja ni kubwa sana nenda hata kwenye mitandao ya simu, migahwa tuko goigoi sana na poor reception, haya yapo hata kwenye familia na ndoa zetu hatuwafundishi watoto wetu kukaribisha vizuri wageni wanaokutembelea na hivyo kukua hivyo, pia wanandoa wengi wanajisahau ukilinganisha mlipokuwa kwenye uchumba hivyo kubeteka ndivyo ililvyo hata makazini, unapoanza kazi unaanza kwa moto kweli kadri unavyozoea kazi ndivyo unavyozidi kujenga kiburi. Pole sana mdau wabaya wetu ni watanzania wenyewe. sijui hili soko la Africa Mashariki tutalimudu vip mimi tu macho yangu tusianze kulalamika oooooh wakenya wanaajiriwa wengi n.k coz Kenya siku hizi ndo imekuwa SI unityetu for every thing. nao wanatusoma tu ujinga wetu na wanchukulia advantage hiyo.
Tuamke watanzania
 
Shark

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Messages
23,830
Points
2,000
Shark

Shark

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2010
23,830 2,000
Tunasikitika yaliotokea, tunayafanyia uchunguzi wa kina, suala la mteja kusukuma gari kituoni , lazima apewe msaada ikiwa Pump Attendants hawapo busy na mteja.
kwa hali yako, uliokuwa nayo na familia.. tutapenda uje kututembelea siku za kazi, maana tumejearibu kukaa na wafanyakazi wote (all shifts,) kila mmoja anasema haijatokea akiwa yeye siku hio... tutashukuru tukipata utembezi wako na tutazidi kuboresha huduma yetu

Asante
PUMA UPANGA SERVICE STATION
Sawa,
Salaam zangu zifike kwa Omary Bahdela na Abdulkadir
 
J

jensen muro

New Member
Joined
Jan 7, 2013
Messages
1
Points
0
J

jensen muro

New Member
Joined Jan 7, 2013
1 0
jamaa wanamalengo ya kuanzisha vituo 188 vya kuuzia mafuta na vituo 11 vya uhifadhi wa mafuta tz so watanzania ndo tunawaangusha hawa wawekezaji wala hatupaswi kuwalaumu kwa lolote
 
kmbwembwe

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Messages
6,886
Points
2,000
kmbwembwe

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2012
6,886 2,000
Puma Energy (Tz) hivi karibuni ilinunua hisa toka kwa BP (Tz) na hivyo kuchukua vituo vya kuuza mafuta toka kwa ilizokuwa BP (Tz). Jana, jumapili tarehe 18 Novemba mida ya kama saa 2 na nusu hivi asubuhi, nilipata shida ya gari yangu kukata mafuta ghafula nikiwa barabara ya Ally Hassan Mwinyi karibu kabisa na Red Cross. Ili kuondoa usumbufu kwa madereva wengine, mimi na familia yangu tukaona tulisukume gari hadi kituo cha mafuta cha Puma ambacho hakikuwa mbali toka hapo. Mi nikawaomba wahusika pale kwenye hicho ktuo niache gari kwa muda wakati namtafuta fundi aje alishughulikie. Wale waheshimiwa wakakataa kata kata. Nilishangaywa na kupigwa butwaa, kwani eneo lao ni kubwa na mimi nilipatwa na emergency, kitu ambacho sikukipangia. Na hao jamaa walituona mimi na mke wangu na mtoto wa kiume tukihangaika kusukuma lile gari. Lakini, licha ya kutosaidia hata kidogo hata kuegesha gari pale kwa muda wlikataa kata kata. Hawa ndio investors tunaowakaribisha Tanzania, ambao wala hawawathamini Watanzania isipokuwa tu pale unaponunua mafuta. Hayo ndiyo tutegemee toka Puma Energy (Tanzania).
Mkuu labda huna habari, serikali ya tz ina hisa kubwa kwenye hyo puma. Hao jamaa bila shaka walitaka unyoshe mkono au hawajui kama kazi ya kituo kama hicho ni pamoja majumu kama hayo. Shame on them
 
Forum statistics

Threads 1,294,738
Members 498,025
Posts 31,186,504
Top