Mkuu Mzee Mwanakijiji, naomba ufike mahali ujikubali kuwa na wewe you are only human na sio super human, hivyo unaweza kufika mahali ukakasirika!. Kwenye maandishi kuna kitu kinaitwa "graphalogy" ambapo msomaji wa andiko anaweza kabisa kuona mwandishi alikuwa kwenye mood gani au state gani wakati anaandika!. Kwa vile tumekaa wote muda mrefu humu, tumefika stage baadhi yetu tunafahamiana kupitia maandishi yetu. Kiukweli pale ulipojibu na kuweka neno "upumbavu", ulijibu kwa hasira, uliporekebishwa, ukanote, ukaliondoa as if mwanzo ulikosea!. Pia unafahamika vizuri katika baadhi ya mijadala, ukizidiwa sana huwa unasusa, its all human!.
Ukiandika kitu with genuine love, kama kwenye love leters, real love inatoka moyoni mwako ina stick kwenye maandishi yako, ikimfikia mlengwa akiisoma barua yako, ile love inamwingia na ana feel good!. Ukiandika umekasirika, zile hasiri zinamfikia mlengwa, na kuna maswali ukiulizwa, megine una ignore kuyajibu just kwa kua ignore, na kuna megine huyajibu kwa kuyasusa!. Its all human!.
Miongoni mwa wafuasi wa CDM humu ndani ya jf miongoni mwao ni ma fanatics kabisa kwao wanaiabudu kama mungu fulani. Ukiendelea kubishana nao, kama sio mvumilivu na mstahimilivu mwenye endurance ya kutosha, unawea kutukana watu humu au kususa kabisa kujibishana nao na sometimes kuisusa jf!.
Kama na mimi pia nimeassume ndivyo sivyo, sorry in advance, I'm only human born to make mistakes!.