Propaganda za wapinzani zimepungua JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Propaganda za wapinzani zimepungua JF

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Masaka, Jun 11, 2008.

 1. M

  Masaka JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 437
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona sasa watoa propaganda wa chadema na wapinzani wengine wametulia na kupunguza propaganda zao hapa jf. Inaonekana members wenye kazi ya propaganda na uzushi wameishiwa. kazi inayofanywa na ccm wakiongozwa na kamanda wao Kikwete imeonekana kushika kasi hasa baada ya bajeti mpya kutoka na sasa watu hawana cha kusema.

  Wabunge wa ccm wameanza kushughulikia matatizo kidogokidogo ndani ya chama na sasa mambo yamekuwa safi na yanategemewa kuwa safi zaidi kwenye hili bunge.

  Watoa propaganda nao wameanza kujichimbia na wengine hata hawatokezi tena hapa. Balance hii ambayo wengine tumekuwa tunaiomba hapa naona sasa imepatikana na kadri Kikwete anavyoendelea kufanya kazi nzuri ya kuleta maendeleo ya nchi basi mengi mazuri yatakuja.

  kidumu chama cha mapinduzi.
   
 2. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kazi gani ya Kikwete? Wizi na procastination?

  Bajeti gani? Huko kufanyia mchezo wa kuigiza msaada unakuita bajeti?
   
 3. tgeofrey

  tgeofrey JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2008
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 526
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni ujinga kutegemea watu waharibu ili utoe umbeya unatakiwa uombe mabaya yasifanyike.

  Tumaini
   
 4. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Uombe umuombe nani?
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,768
  Likes Received: 83,104
  Trophy Points: 280
  Achana na dhana potofu! Wanachama wa CHADEMA hapa ni wachache mno! Wengi tuna mapenzi na nchi yetu na kuhuzunishwa na mwelekeo wake ambao kila kukicha maisha yanazidi kuwa magumu kwa Watanzania walio wengi wakati mafisadi wachache wanakuwa matajiri wa kupindukia kwa kuiba rasilimali za Watanzania na makusanyo yao ya kodi na kisha kujijengea majumba ya kifahari ndani na nje ya nchi na kununua magari ya kifahari.

  Hivi ni wanachama wangapi unaowafahamu hapa JF ambao pia wana uanachama wa CHADEMA? Acha kubwabwaja kaka!! kama huna la kusema bora ukae kimya kuliko kuja na dhana potofu. Watanzania tuna haki ya kukilaumu chama kilicho madarakani na hata vyama vya upinzani na hapa JF yote hayo yanafanyika, siyo lazima tuwe wanachama wa chadema ili kukiromea chama cha mafisadi.

  Usiwe unabwabwaja kama Kasuku kwa kupewa mistari ya kuandika hapa JF na wewe kuiandika kama ulivyopewa bila kuhoji chochote. Jifunze tabia ya kuchanganua mambo na kujiuliza maswali kabla ya kuimba kama kasuku.
   
 6. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ulichokisema hapo hakina mantiki!

  Kama unasema vilio vya vya upinzani vimepungua kwa sababu CCM na Kikwete wameanza kufanya kazi, ina maana waliyokuwa wanayasema hayakuwa propaganda. Na hapo hapo ina maana unakubali CCM na Kikwete walikuwa wachovu. Unaona usivyo make sense? Watu wengine vipi jamani?
   
 7. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  duh ! mod kaamua kuifanyia MBOWEISM hii thread !! ukiona kitu ambacho ni kizuri kwa serikali na watu wakaanza kukiponda na thread ikahamishwa ili wapinzani wasione jema lolote, hiyo huitwa MBOWEISM !!
   
 8. M

  Masaka JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 437
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhh, kwa kweli sijui kama ni wanachama wa chadema ni wachache hapa JF na kama hili ni kweli basi nafurahi sana kujua kuwa wana chadema hapa JF ni wachache sana. Ni vizuri pia lakini kujua kuwa wana ccm tumeongezeka hapa na balance imepatikana.

  Tujenge nchi sasa na tuache majungu.
   
 9. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Naona tuna Crusaders hapa.
   
Loading...