Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,589
- 1,681
Watanzania wengi wamenyweshwa propaganda kuwa nchi imeenedelea mno chini ya CCM, na kwamba bad0 tunachanja mbuga! Maskini! Baada ya CCM kuwanyang'anya lugha ya pili, Kiingereza, ambayo angalau wangeweza kufuatilia masuala ya Kimataifa na jinsi maisha yalivyo kwa wengine, uwezekano pekee wa kuyajua hayo ni kwa kusafiri nje.
Lakini hata kusafiri nje aghalabu kunataka elimu, lugha, fedha na mawasiliano, si wengi wenye bahati hiyo. Matokeo yake raia wengi wa Tanzania ni mbumbumbu wa mambo muhimu, isipokuwa mpira, tena wa miguu tu! Bahati njema siku hizi kuna TV ambazo, more and more, Watanzania wanapata uwezo wa kununua. Ndiyo hapa mtu mwenyewe anaweza kugundua uhalisia wa kuchelewa kwetu.
Katika vita vya sasa baina ya Israeli na Hamas, kitu kilich0nistaajabisha ni hospitali za Gazza. Kipande hicho cha ardhi kilichozuiwa aina yoyote ya maendeleo na Waisraeli, hata kuingiza chuma ni marufuku....kina hospitali nzuri, zenye vifaa kuliko hospitali yoyote Tanzania!
Tena wana hata Ambulance nyingi, safi, zinaz0fanya kazi! Najua, kuna watu watasema, 'ah, lakini hao ni Waarabu wanapewa pesa na wenzao!' Si kweli, Tanzania inapokea mara sita fedha za msaada kuliko Gazza! Tofauti ni kuwa kwa Gaza hicho kidg kinachopatikana chatumiwa kwa lengo lake, bas!