Bei za dawa za mitishamba zaidi kupaa.

Mavindozii

JF-Expert Member
Oct 20, 2012
2,111
2,759
Hello Wana JF, naomba kuuliza kwa nini hizi bei za mitishamba bei zake ni kuanzia 150,000 kuendelea ? Kule Facebook ukiingia huko utakuta kuna matangazo mengi sana kuhusu dawa za kienyeji na bei zake zinatisha wakuu , nilichojifunza watoa dawa wengi wa dawa za kienyeji ni matapeli wa kutupwa , na sisi wenyewe ni wajinga sana , unakuta mtu anaumwa UTI au bawaziri badala ya kwenda hospital wananunua hizi dawa zaa kienyeji, kutibu UTI kwa dawa za pharmacy haizidi 12000na unapona , nenda sasa kwa kienyeji utasikia 250000 ,what the heck, Ninachoamini mganga au tibabu wa kienyeji anayetibu dawa zake ni kuanzia 5000 ,10000 , wengine anakupa dawa ukipona unamletea zawadi kama shukrani.Kuna mmoja hapa ARUSHA ameniambia anatibu Kisukari kwa nusu milioni.Tunaangamia kwa kukosa maarifa ,hamna cha mzizi mbichi ,mbaya zaidi wanakuambia acha dawa zako za hospitals,utakuta ,kwa kuua FIGO na haya matakataka ya kienyeji,
 
Back
Top Bottom