Miongoni mwa mambo yanayonifanya nishindwe kumwelewa kabisa Prof. Muhongo ni tabia yake ya kutumia kiwango chake cha elimu na CV yake kama utetezi badala ya kujadili hoja inayokuwa mezani. Mara nyingi badala ya kujadili jambo husika, hukimbilia kueleza CV yake na sehemu alizofanya kazi na ni jinsi gani anaheshimika duniani. Hata walipomwambia alishiriki kuwezesha pesa zilizokuwa kwenye account ya escrow kuibiwa kwa kufanya udalali, aliishia kusoma CV yake badala ya kujadili tuhuma. Kwenye mkutano mmoja wa wadau wa mafuta uliofanyika Mlimani City ambapo alifanya presentation, aliishia kutumia fursa hiyo kuonesha ni jinsi gani anaijua miamba kwa kuorodhesha makorokoro ambayo kimsingi hayakuhitajika mahali pale. Nafikiri alijiaminisha kwamba akitishia watu na usomi, watamwogopa. Hataulizwa maswali mengi. Nimefikia hitimisho lifuatalo: Prof. Muhongo hana uhakika na usomi wake. He feels insecure. Hivyo, he constantly see the need to remind people how educated he is for fear that people have forgotten. Hiyo si sifa ya msomi (as in intellectual). Wahenga walisema, "A tiger does not shout its tigritude, it acts". Huoneshi usomi wako kwa kusoma CV yako hadharani kila unapopata fursa/kupiga kelele kuwakumbusha watu kuhusu CV yako. Ukifanya matendo ya kisomi watu watahitimisha kuwa wewe ni msomi (kama ndio kitu unajali maishani, kuonekana msomi).