Poise
JF-Expert Member
- May 31, 2016
- 7,633
- 7,902
Huyu si ndie alimtonya yule mkuu wa kitengo cha mizani kule bandarini kuwa wakubwa wanakuja kwa hiyo arekebishe mambo,haiwezekani kila mara awe yeye tu.Muhongo ni muongo kweli ,alipoteuliwa kwa mara ya pili kwenda wizara ileile wengi walipinga ,na sasa matokeo yake sote tumeyaona,kumbadili tabia mtu mzima ni sawa na kumtaka kumkunja kambale mkavu
Hakika ni uyo huyo Muhongo ndiye alitoa siri ya pale TPA kuhusu ziara ya rais ya ghafula usiku uo huo watu wakafunga machine.
Maana siku ile. ndiyo angetumbuliwa, wale jamaa tulipata mtonyo kuwa walifunga zile mashine usiku kucha.
Rais, alisema, "hizi mashine mbona zimefungwa usiku wa kuamkia leo, akasema aaah, walitoa siri kuwa nakuja leo hapa TPA, sawa "
Basi, ukweli ni kwamba watu tuliowaamini na kudhania kuwa watakuwa makini ndiyo ao hao wanatuuza kwa wazungu koko kisha, na wao kujigeuza kuwa kama wazungu pori wakati ni waafrika nywele ngumu.
Kuna ombwe kubwa sana la uongozi na uzalendo miaka hii hapo Tanzania.
Magufuli, anapitia wakati mgumu sana kwa kuwa mzalendo huku timu yake karibia robo tatu (3/4) ni vibaka, manyangau, walafi na wauaji.
Jambo la muhimu kwa sasa, ni sisi wananchi wote tumuunge mkono rais wetu tutashinda.
Maana kila siku hawa wasaidizi wa rais wa hizi wizara zote taasisi takribani zote tunaona walivyo wazandiki, wanafiki, wapiga deal n.k .
Yaani, "Ukiwa nao Wanacheka' ila Ukigeuza Mgongo ni Wauaji"