Profesa Shivji: Mkataba wa Bandari unaegamia zaidi upande mmoja na hauna ukomo wa muda. Hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD

IMG_7772.jpeg

Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) ni mkataba kati ya nchi na nchi kuhusu uwekezaji, na mkataba unasema ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ni aina ya mikataba ya uwekezaji

Katika mkataba huu wa bandari kuna mambo mawili, jambo la kwanza, mkataba unahusu ushirikiano wa kiuchumi lakini sio ushirikiano wa kiujumla bali ni katika eneo la bandari za bahari na bandari za maziwa. Na jambo la pili ni kwamba mwekezaji ameshatambulika

Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa.

Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidiplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)

Chanzo: Jambo Tv
 
Machafuko tu bro. Siku zote huwa nasema hapa bila kuumauma maneno.
Acha uzwazwa mzee. Bora amani ya kijinga kuliko haki yenye fujo.

Watu million 60 huwezi kufanya decision ya kuwafurahisha wote.

Hujifunzi nchi zilizokimbilia kwenye machafuko sasa hvi zinaishije?

Narudia acha uzwazwa aisee.

Yaan mkataba ambao direct impact yake haimfikii hata mtoto wako ndio ufanye nchi iingie kwenye machafuko ambayo yataleta direct impact kwa watoto wako?, tumieni akili basi
 
Subiri KUFURUSHWA hapo ikulu ukachimbe MIHOGOOH.
 
Acha uzwazwa mzee. Bora amani ya kijinga kuliko haki yenye fujo.

Watu million 60 huwezi kufanya decision ya kuwafurahisha wote.

Hujifunzi nchi zilizokimbilia kwenye machafuko sasa hvi zinaishije?

Narudia acha uzwazwa aisee.

Yaan mkataba ambao direct impact yake haimfikii hata mtoto wako ndio ufanye nchi iingie kwenye machafuko ambayo yataleta direct impact kwa watoto wako?, tumieni akili basi
Unafikiria kizamani sana yaani Kijima!
 
k
Hii nchi inahitaji mambo fulani yatokee ili Raia na nchi yao wapone.
kabisa maana hili suala la bandari kuna viongozi wamewageuza wananchi mazuzu imagine mpaka mwanasheria wa serikali bwana feleshi katetea ujinga huu leo lakini watu wanazidi kuibuka na kusema mkataba ni fanfwa haufai Mungu aingilie kati maana kuna wachache wanaangalia matumbo yao tu
 
Kweli nimeamini huwezi mwelewesha shekh utamu wa nyama choma na bia. Hii serikali haielewi kuwa sisi watanzania ni maskini na sifa ya maskini ni kufatilia mali za urithi. Sasa nyie mnataka kuuza bandari alafu pesa mgawane nyie na vizazi vyenu vyote hapa duniani hata mkifa mna hamu ya kuwa reincarneted kwenye familia zenu ili muendelee kuwa matajiri ndiyo mana akifa mtu anazaliwa mtu kwenye familia zenu?
 
Back
Top Bottom