Profesa Kabudi: Kikwete na Mkapa haifai kuwataja kwenye kashfa sababu tunatunza heshima yao

Hata mimi naunga mkono hoja. Tusiwajadili Marais wetu wastaafu na hata aliyeko madarakani. Urais ni taasisi sio kitu cha kuchezea. Full stop.
Lakini, tunaweza kuwajadili makamu, PM, Spika, Naibu spika, na mawaziri wooote pamoja na wabunge woote. Mkitaka kumjadili Dr Kikwete, mjadilini alioyafanya akiwa waziri kuleeeee. Mkitaka kumjadili Dr Mkapa, mjadilini aliyoyafanya kuleee kabla ya uraisi.
Mkitaka kumjadili Dr John, mjadilini kuleeee sio leo. Leo tunampongeza kwa kuwa mzalendo wa kuthubutu kutufungua macho tukaona tunavyo ibiwa.
Ushauri, Ili tusijewaingiza kwenye msaragambo huu, tuachane na kutafutana, iundwe tume, iwachunguze kwa siri, iwakamatie kile cha juu walichotuibia, wakirejeshe hazina kuu, na wasiruhusiwe kulalamika. Jiulize, ni nini maana ya tume ya utumishi na maadili ya viongozi?? Watu huenda kuapa nini? Watu huenda ku declare nini pale? Ati naingia uwaziri na shs 100 na nyumba nusu sijamalizia kupaua. Ukitoka na nyumba 100 baada tu ya uwaziri wa miaka 5 si lazima uulizwe??
Najiuliza, nyiye mliotuaminisha kuwa mtawachunguza hawa viongozi, mlikuwa wapi?? Nyiye nanyi ni majipu. Mwafaa mtumbuliwe. Nisiseme mengi, yale ya bwana yulee DAB na magari ya kifahari na viwanja 120 miji mbali mbali aliyovitaja Mh Musukuma yameishia wapi?? Hicho kitengo ni jipu lililoiva mno.
 
NDIYO MAANA UKUTI VIONGOZI WETU WANAONGELEA HAKI. MAANA HAKI AICHAGUI MASKINI WALA TAJILI MTUMWA WALA KIONGOZI. WOTE MASHETANI TU NA SHETANI ATOI SHETANI. TOKA LINI MTENDA DHAMBI AKAWA NA HESHIMA?
 
Njaa haijawahi kumuacha msomi yeyote yule wa kiwango cha PhD/Professor salama.

It is a big shame kwa hawa wanaojiita wasomi. Hivi mtu ameboronga na kulitia taifa hasara , hata kama kuna mazuri alifanya, Je kuna tatizo gani akinywa kikombe cha babu kwa ujinga wa kuliingiza taifa katika hasara? Kwanini wanatetea ujinga?

Who is Mkapa, who is kikwete by the way? hao nao si watu tu kama wengine? Ngozi nyeusi ni shida sana katika hii dunia. Wanapenda sana kuabudu au kuabudiwa kama miungu watu! Shame!

Sasa kama ndio hivyo, hii sinema na ifike mwisho. Tuseme hivi: "YALIYOPITA SI NDWELE TUGANGE YAJAYO". Hapa nina maana asiguswe mtu yeyote kuanzia Rais mtaafu mpaka watendaji wengine wote maana hakuna tija kuwahukumu sisimizi halafu ma-Don yanaachwa kwa sababu zipi hasa?

Huo ni ujinga wa kiwango cha lami kabisa.
 
Hata mimi naunga mkono hoja. Tusiwajadili Marais wetu wastaafu na hata aliyeko madarakani. Urais ni taasisi sio kitu cha kuchezea. Full stop.
Lakini, tunaweza kuwajadili makamu, PM, Spika, Naibu spika, na mawaziri wooote pamoja na wabunge woote. Mkitaka kumjadili Dr Kikwete, mjadilini alioyafanya akiwa waziri kuleeeee. Mkitaka kumjadili Dr Mkapa, mjadilini aliyoyafanya kuleee kabla ya uraisi.
Mkitaka kumjadili Dr John, mjadilini kuleeee sio leo. Leo tunampongeza kwa kuwa mzalendo wa kuthubutu kutufungua macho tukaona tunavyo ibiwa.
Ushauri, Ili tusijewaingiza kwenye msaragambo huu, tuachane na kutafutana, iundwe tume, iwachunguze kwa siri, iwakamatie kile cha juu walichotuibia, wakirejeshe hazina kuu, na wasiruhusiwe kulalamika. Jiulize, ni nini maana ya tume ya utumishi na maadili ya viongozi?? Watu huenda kuapa nini? Watu huenda ku declare nini pale? Ati naingia uwaziri na shs 100 na nyumba nusu sijamalizia kupaua. Ukitoka na nyumba 100 baada tu ya uwaziri wa miaka 5 si lazima uulizwe??
Najiuliza, nyiye mliotuaminisha kuwa mtawachunguza hawa viongozi, mlikuwa wapi?? Nyiye nanyi ni majipu. Mwafaa mtumbuliwe. Nisiseme mengi, yale ya bwana yulee DAB na magari ya kifahari na viwanja 120 miji mbali mbali aliyovitaja Mh Musukuma yameishia wapi?? Hicho kitengo ni jipu lililoiva mno.
JK ndiye alisaini leseni ya Bulyanhulu akiwa waziri unalijua hili?
 
walio tajwa kwenye ripoti ya prof

wanajulikana kwa majina yao sasa

wanataka kuhalalisha ufisadi wao

kwa kuwachomekea viongozi wetu

wastaafu ili tushindwe

kuwashughulikia kamwe hatukubali!!

walio tajwa ktk ripoti washugulikiwe kwa mujibu wa sheria ili iwe funzo kwa watakao jaribu kuhujumu mali yetu!!

tukiwa chekea na kuwaonea aibu wale walio tajwa ktk ripoti mambo haya yatajirudia tena.

wanataka kujificha ktk migongo ya marais wetu wapendwa wastaafu ili wakwepe kushugulikiwa hatukubali!!
 
Kama ni hivyo, na mimi nautaka "Urahisi" aka Urais. basi. Business as usual.

Waziri wa Sheria Prof. Plamagamba Kabudi amesema haifai kuwataja marais Mkapa na Kikwete kwa kuwa heshima yao inatunzwa kwa kuwa wamekuwa wakuu wa nchi, wakuu wa serikali na maamiri wajeshi wakuu na heshima hiyo inafaa kutunzwa kikatiba, kisheria, kimaadili, kiutamaduni na kiutu na ndio maana hata ripoti haijawataja sehemu hata moja

Hivyo haifai kuacha kujadili mambo yaliyo mbele yetu na kuwajadili wakuu hawa wastaafu

Heshima? Wezi wana heshima gani!!!! Wakati wanaiba wewe bundi walikuheshimu? To a ukuda hapa, umesoma sheria za njaaaa! Shutup!!!!
 
Acheni hizo, rais wa brazil aliondolewa madarakani na kufunguliwa mashitaka, juzijuzi rais wa south korea ameondolewa madarakani kawekwa rumande na tumemwona kapigwa pingu pamoja na kwamba ni mwanamke, hivi sasa kuna mjadala wa kumwondoa trump madarakani. Ina maana viongozi wa hayo mataifa makubwa niliyotaja wenyewe hawastahili heshima ila wa kwetu pekee ndo heshima yao imepanda hadi mawinguni. Kwa mentality hizi hakuna anayestahili kushtakiwa kwani wote waliotajwa ni wale wenye title za uheshimiwa
 
Hapo huyo Kabudi kachemka.

Ni kana kwamba anakubali hao wawili waliboronga kwenye hiyo mikataba lakini wanayafagilia mauchafu yao chini ya busati kwa kisingizio cha kuwatunzia heshima.

Mtu kama huyu 'kaka msomi' ungedhani labda ana sophistication ya kutosha kuweza walau kuweka spin yenye akili kuhusu hao marais na huo ushiriki wao lakini wapi.

Bure kabisa.
 
JK ndiye alisaini leseni ya Bulyanhulu akiwa waziri unalijua hili?

Nasi tumeamriwa sio kuombwa kuwa tusiwajadili Marais waliokwisha pita. Ukimjadili kama waziri wa nishati sawa. Hujiulizi kwamba kwa nini kalamu ziliteleza kwenye ripoti zote za makinikia?? Zilipotaka kuandika majina yao, hata kwa mfano tu kalamu zote ziliteleza. Acha kumjadili kwa afya yako.
 
Kwa hiyo hao wengine ndio heshima yao mnaivunja? Ipo siku nao heshima yao itavunjwa kwa nguvu na wananchi wenyewe.
 
Back
Top Bottom