Mikataba ya hovyo; Je, Magufuli anawalinda Mkapa na Kikwete au anajilinda yeye!

Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,092
2,000
Baada ya kuapishwa tarehe 4/11/2015, cha kwanza alichowaahidi viongozi wakuu wastaafu ni kuendelea kuishi kwa amani na kuwataka walale usingizi mwororo bila kujali kelele za aliowaita wapinzani wakorofi.

Hiyo ilikuwa ni kabla ya sakata la madini na juzi tena kawahakikishia kutokuwa na hofu kwa waliyoyatenda na kwamba hataruhusu heshima yao waliyoijenga wakiwa madarakani kuharibiwa na wananchi wakorofi.

Na kweli imetokea. Wananchi wamepigwa marufuku kuyataja majina mawili Mkapa na Kikwete na kuwahusisha na mikataba yoyote ile inayolalamikiwa kama huu wa madini na badala yake walioagizwa kusign mikataba ndio washughulikiwe.

Na kweli imetokea. Waziri wake Mwakyembe tayari kafungia gazeti moja kwa miaka miwili kwa kosa tu la kuchapisha picha za Mkapa na Kikwete kwenye kurasa zinazoongelea mikataba hiyo iliyoitia taifa hasara.

Si hivyo tu. Adui wa taifa hili kwa sasa ni wale waliokuwa wanalalamikia hii mikataba kwamba ni ya hovyo na ya kifisadi. Anayeongoza kwa hili ni Mh. Tundu Lissu aliyeanza kupigia kelele hii mikataba toka miaka ya 1990s.

Je nini hasa ni lengo la Rais John Pombe Magufuli? Hata kwa akili kidogo ilitegemewa kwamba wahusika wangeshughulikiwa bila kujali nafasi zao katika jamii kwa kulisababishia taifa hasara ya mabilioni kwa miaka mingi.

Ilitegemewa kwamba ili kufanikisha hili hatua zingechukuliwa kuhakikisha hakuna mhusika anayekwepa kuwajibishwa kwa sababu tu kuna mwanya unaoweza kutumika kuzuia wengine wao kushughulikiwa kisheria.

Bila kumung'unya maneno au kupepesa macho, wahusika wakuu wa sakata hili na mengine mengi ni CCM na serikali yake. Hakuna namna mwanachama au kiongozi wa CCM anapona kwenye hili na hasa viongozi wake wakuu.

Je nini kinachowalinda hawa wasaliti wakuu wa taifa? Magufuli anajua, mimi najua na Mtanzania yeyote anajua...kikwazo ama kisiki ni sheria mama, Katiba, ambayo inacho kipengelele kinachowalinda wezi wakuu wa taifa letu.

Katiba inamlinda Mkapa, katiba inamlinda Kikwete na Katiba inamlinda na itaendelea kumlinda Rais, Jemadari Mkuu na Mtendaji Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Tanzania. Mpaka tutakapoking'oa kisiki kinachowalinda hatutafanikiwa.

Rais John Pombe Magufuli, kama wewe ni jasiri na una nia thabiti ya kupigana hii vita, kwa nini unasita kutumia silaha pekee ya maangamizi, silaha inayopatikana ndani Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba kama itapitishwa?

Je unawalinda watangulizi wako au unajilinda wewe siku za usoni? Ili kuondoa utata huu moja, kwa niaba ya CCM waombe radhi Watanzania na pili, malizia mchakato wa Katiba mpya bila kuchelewa.
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
39,665
2,000
Mtu wa kawaida anaweza fikiri Magufuli anavyo apa kuwalinda kina JK na Mkapa
basi kweli 'anawapenda na anataka kuwalinda'

Ukweli ni kuwa JK na Mkapa wana mizizi mirefu kwenye CCM

wao wawili wakiamua huyu Magufuli 'aondoke'
anaondoka bila ubishi..na Magufuli anajua hilo

So hadharani anaahidi 'kuwalinda' huku anajua anachowaahidi ni
'kutowagusa' ili na yeye 'wamuache' afanye anavyotaka...
 
AirTanzania

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
1,139
2,000
CCM ni Kichaka cha Wagawa Rasilimali za Tanzania kwa mataifa ya Ulaya na America. CCM wanaendesha nchi kwa kiki ya kulindana. Sanaa juu ya Sanaa
 
AirTanzania

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
1,139
2,000
Mtu wa kawaida anaweza fikiri Magufuli anavyo apa kuwalinda kina JK na Mkapa
basi kweli 'anawapenda na anataka kuwalinda'

Ukweli ni kuwa JK na Mkapa wana mizizi mirefu kwenye CCM

wao wawili wakiamua huyu Magufuli 'aondoke'
anaondoka bila ubishi..na Magufuli anajua hilo

So hadharani anaahidi 'kuwalinda' huku anajua anachowaahidi ni
'kutowagusa' ili na yeye 'wamuache' afanye anavyotaka...
Hiyo inaitwa nilinde nikulinde au kwa kiswahili fasaha nifute tongo nikufute matako
 
Dan Zwangendaba

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
2,398
2,000
Mimi naamini spirit hii ya kuunda kamati za uchunguzi wa mambo ya kitaifa yaliyopita itaendelezwa kwa kuundwa kwa kamati ya uuzaji wa Nyumba za Serikali.
 
Deo

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
1,218
1,250
Nadhani ni mgao mpya unahitajika, mkwara wa nguvu halafu hisa/mgao kilele kwishney
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,092
2,000
Mzee wangu Mag3 hapo kwenye title una maana ya Mkapa na JK? Maana Ben ndo huyo huyo
Oh dear, nilitaka kuandika Mkapa na Kikwete! Samahani, sijui mods watasaidia hapa! Inatakiwa isomeke:

Mikataba ya hovyo, je Magufuli anawalinda Mkapa na Kikwete au anajilinda yeye?

NB: Tafadhali mods saidia kurekebisha title: Cookie, Active
Mkapa ndiyo nani Ben ndiyo nani?

Upunguani huo.
Typo, ni Mkapa na Kikwete...mathalan katajwa kipenzi chako, roho itakuwa inauma aise.
 
Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
10,381
2,000
Mtu wa kawaida anaweza fikiri Magufuli anavyo apa kuwalinda kina JK na Mkapa
basi kweli 'anawapenda na anataka kuwalinda'

Ukweli ni kuwa JK na Mkapa wana mizizi mirefu kwenye CCM

wao wawili wakiamua huyu Magufuli 'aondoke'
anaondoka bila ubishi..na Magufuli anajua hilo

So hadharani anaahidi 'kuwalinda' huku anajua anachowaahidi ni
'kutowagusa' ili na yeye 'wamuache' afanye anavyotaka...
Ndio maana huwa tunasema Kwa Tanzania rais waliopita ndio wanaamua nani awe rais-upigaji wa kura ni kuidhinisha maamuzi tu
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,092
2,000
Na ndo maana huwa hata kujisumbua kujibu kitu hawajisumbui
wanajua mnae muona ana nguvu hana lolote
Nguvu aliyo nayo Magufuli ni wa kuwashughulikia wapinzani tu kwa kuwatumia wahuni kama Bashite na Gambo, mbele ya Kikwete au Mkapa, he is nothing. Mtu yeyote ndani ya CCM angeweza kuokotwa akafanya anayoyafanya Magufuli na wajinga wakapiga makofi na vigelegele.

Werevu watauliza kwa nini wahusika wakuu wa mikataba ya wizi hawagusiki, kulikoni? Halafu mataahira ya Tanzania yanadai anao uthubutu, ni uthubutu upi huo? Kama ni uthubutu wa kuwalinda wezi wenzake aliowatumikia wakiwa madarakani miaka yote hiyo, hapo sawa.
 
Bullycheka

JF-Expert Member
Dec 15, 2016
552
500
KAULI MBIU YA VIONGOZI WA KIAFRIKA. NI KULINDANA TU.

WASIPOLINDANA LEO YAWEZEKANA NAWE KESHO YAKAKUKUTA YALIYOMKUTA MWENZAKO

JE,NANI,ATAKULINDA KESHO?
 
M'bang'ang'walu

JF-Expert Member
Jul 18, 2015
633
500
Mtu wa kawaida anaweza fikiri Magufuli anavyo apa kuwalinda kina JK na Mkapa
basi kweli 'anawapenda na anataka kuwalinda'

Ukweli ni kuwa JK na Mkapa wana mizizi mirefu kwenye CCM

wao wawili wakiamua huyu Magufuli 'aondoke'
anaondoka bila ubishi..na Magufuli anajua hilo

So hadharani anaahidi 'kuwalinda' huku anajua anachowaahidi ni
'kutowagusa' ili na yeye 'wamuache' afanye anavyotaka...
Na pia hilo ni sharti kwake kwa hiyo nafasi aliyopewa kwani hao marais wastaafu walichangia kwa kiasi kikubwa yeye kupata hiyo nafasi.
Pia aliongea kwamba tusipende kuwafanyia wenzetu yale ambayo sisi hatupendi kufanyiwa.
Kwa maana nyingine kwa kuwa yeye pia ni raisi mstaafu mtarajiwa anaweka mazingira hata yeye asije kusumbuliwa.
Katika hili afadhali ucheze na yeye mwenyewe anaweza kukusamehe lakini si kwa hawa wastaafu
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,092
2,000
Mtu wa kawaida anaweza fikiri Magufuli anavyo apa kuwalinda kina JK na Mkapa basi kweli 'anawapenda na anataka kuwalinda'
Kinachowaunganisha ni U-CCM tu...tamaa na ulafi.
Ukweli ni kuwa JK na Mkapa wana mizizi mirefu kwenye CCM
Waliomtangulia walikuwa na historia ndani ya CCM, huyu ni limbukeni tu.
wao wawili wakiamua huyu Magufuli 'aondoke'
anaondoka bila ubishi..na Magufuli anajua hilo
Kumbukumbu ya Baba wa Taifa alipoanza kuwazodoa.
So hadharani anaahidi 'kuwalinda' huku anajua anachowaahidi ni
'kutowagusa' ili na yeye 'wamuache' afanye anavyotaka...
Magufuli keshapata na ujanja kupata...kwa nini amwage mchanga kwenye mkate wake!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom