Profesa Kabudi: Kikwete na Mkapa haifai kuwataja kwenye kashfa sababu tunatunza heshima yao

Hizi tume na kamati tunazounda ni upumbavu mtupu. Mkimuita Maswi au Mruma akasema alitumwa na Waziri, Waziri nae akaja akasema alitumwa na Mkapa/Kikwete mtasemaje? Tuanze kwanza kwa kuondoa kinga ya Marais wastaafu kwenye baadhi ya mambo (uhujumu uchumi etc) ili adabu iwepo. Otherwise tutapigwa tu kila iitwapo leo.
Aliyesaini ndo anawajibika. Akituonesha saini ya Rais kwenye Mkataba tutamwachia, la kama ni longolongo inakula kwa mtia saini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Prof ajue kuwa wananchi hawana tatizo kabisa na hao viongozi wastaafu. Viongozi siyo malaika; hufanya makosa. Busara katika uongozi ni pamoja na kusahihisha hayo makosa bila kudhalilisha viongozi waliofanya hayo makosa. Kwa hiyo wenye tatizo kubwa ni viongozi wa sasa walioamua kwanza, kufanya uchunguzi kwenye jambo ambalo kusema kweli halikuhitaji uchunguzi kwani kila kitu kilikuwa kinafahamika. Pili, kutangazia umma mubashara taarifa ya uchunguzi na hivyo kuwavua nguo hadharani hao viongozi. Sasa, baada ya kuwavua nguo, inawezekana kweli kuzuia watu wasiwatazame?
 
Watu walizunguka dunia kujitafutia wawekezaji na wakaja nao mwisho unakuja na hoja kama hii unategemea upate jibu gani kama sio kuwatusi watu uliowatea hoja husika. Ninaamini huwa zama hubadika na kubadilika kwa kuna majibu mengi yatatokea mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli siyo vizuri kuwataja viongozi wastaafu kwa lengo la kuwatunzia heshima.Maana hata mikataba waliingia kwa heshima,na wabunge wetu wale wa ndiyo nao walipitisha kwa heshima,na sasa heshima iwe mbele kwa wote.Kwa msingi huu maendeleo yatachelewa sana TZ.Maana kila atakaye ingia anauwezo wa kupiga ishu kwa kujuwa hatapata matatizo kisheria.Tutumie critical thinking.
 
Ni Kabudi huyu ninayemfahamu? Hivi CCM Kuna laana gani inamaliza vichwa vya watu kiasi hiki?
Mwafrika hata akisoma hawezi kuacha upumbavu wake.Haya aliyaongea aliyewahi kuwa rais wa Afrika kusini bwana P. Botta.
 
Heshima hujijenga kulingana na matendo ya mtu, haishinikizwi. Historia ikakuhukumu kwa kwa kushindwa kutoa hata chozi kwa kukereka moyoni kama unaogopa kusema kusema au kunyosha kidole. Busara kuyapuuza walioyafanya na tusonge mbele lakini tusiwanyime haki yao ya kuwakumbuka kama marais walioiangusha nchi ktk vipindi vyao.
 
Ndio maana nilipinga kata kata alipoteuliwa waziri ikawekwa hapa biography yake ya kienyeji inasema alikuwa genious wa sheria UD.

Miezi miwili baadae ikagundulika kwamba cheti cha Form 4 hana, mtihani wa bar exam ambao kila wakili ameufanya huyu hakufanya, na law school hajafanya. Hana umahiri wa sheria kihiiivyo...

Haelewi checks and balances on co-equal branches, haelewi equal protection under the law, haelewi nothing...
 
Back
Top Bottom