Profesa Kabudi: Kikwete na Mkapa haifai kuwataja kwenye kashfa sababu tunatunza heshima yao

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,940
19,130
Waziri wa Sheria Prof. Plamagamba Kabudi amesema haifai kuwataja marais Mkapa na Kikwete kwa kuwa heshima yao inatunzwa kwa kuwa wamekuwa wakuu wa nchi, wakuu wa serikali na maamiri wajeshi wakuu na heshima hiyo inafaa kutunzwa kikatiba, kisheria, kimaadili, kiutamaduni na kiutu na ndio maana hata ripoti haijawataja sehemu hata moja

Hivyo haifai kuacha kujadili mambo yaliyo mbele yetu na kuwajadili wakuu hawa wastaafu

Teh teh....... Ndio maana wako huru kufanya wanayafanya. Wanajua wakiondoka hata kama wamefanya mabaya kiasi gani hakuna wa kuwasumbua. Yaani binadamu tunamuweka kama "mungu" Tukiamini kuwa hawakosei! Eti wanasema hakuna alie juu ya sheria...ha ha haaaaa. Bila katiba itakayoondoa haya kuwekwa, tutaendelea kuliwa tu. Kila ajae ataunda tume, atapata umaarufu na kisha ataondoka. Hao watuhumiwa wengine wakisema walitumwa na hao wanaostahili kuheshimiwa sana ndio kesi yao imeisha au!!!?
Kama kwenye taasisi, wenyeviti wanatumbuliwa kwa kuwa tu wameenda kinyume na taratibu, kwanini mwenyekiti wa mawaziri apone na kuwekewa kinga!!!!
 
Waziri wa Sheria Prof. Plamagamba Kabudi amesema haifai kuwataja marais Mkapa na Kikwete kwa kuwa heshima yao inatunzwa kwa kuwa wamekuwa wakuu wa nchi, wakuu wa serikali na maamiri wajeshi wakuu na heshima hiyo inafaa kutunzwa kikatiba, kisheria, kimaadili, kiutamaduni na kiutu na ndio maana hata ripoti haijawataja sehemu hata moja

Hivyo haifai kuacha kujadili mambo yaliyo mbele yetu na kuwajadili wakuu hawa wastaafu

Only in Tanzania! Kama wenyewe hawakuitunza heshima hiyo kwa wao kujihusisha na mambo ya kifisadi kinyume na viapo walivyokula, kuna uhalali gani wa kulazimisha heshima kwao kwa mtutu wa bunduki?
 
Okay! Kwahiyo anachosema ni kwamba JK na Mkapa nao wanahusika na wizi huu lakini kutokana na nafasi zao basi haipaswi kuwataja!!!

Anyway, hata ukisoma Ripoti ya 2, Mawaziri wa Nishati wooooooote waliosaini mikataba ya madini wametajwa kwa majina!! Lakini waziri wa nishati aliyesaini mkataba mwaka 1994 hakutajwa kwa jina!! Sana sana amesifiwa ile mbaya jinsi amabavyo ali-struggle kuhakikisha 15% inaenda serikalini kabla hajaja Kigoda na kuipora!!!
 
Maneno ya Professa ni tata bado! Kwamba labda walihusika ila kwa heshima yao wanahifadhiwa?

Nadhani angenena kama Raisi alivyofanya kwamba "Hawajatajwa katika ripoti".
 
Waziri wa Sheria Prof. Plamagamba Kabudi amesema haifai kuwataja marais Mkapa na Kikwete kwa kuwa heshima yao inatunzwa kwa kuwa wamekuwa wakuu wa nchi, wakuu wa serikali na maamiri wajeshi wakuu na heshima hiyo inafaa kutunzwa kikatiba, kisheria, kimaadili, kiutamaduni na kiutu na ndio maana hata ripoti haijawataja sehemu hata moja

Hivyo haifai kuacha kujadili mambo yaliyo mbele yetu na kuwajadili wakuu hawa wastaafu

ma-profesa wetu hawa.
sorry, I mean ma-propesa!

kweli hii ranking kumbe tunastahili....

main-qimg-3709717f6b5938b61eef9aab9f5d3049
 
hao mawaziri wa wanasheria wenyewe vip hawastahili kutunziwa heshima?
 
Duh.....hivi tunarogwa na nani? Na hawa ndio miongoni wasomi waliotukuka kabisa katika nchi yetu.
 
Back
Top Bottom