Profesa Kabudi: Kikwete na Mkapa haifai kuwataja kwenye kashfa sababu tunatunza heshima yao

Mnatuboa na mi dandans yenu? What the hell is dandans? Kwani sasa unahitaji dandans uone video? Tafuteni sehemu nyingine za kupata pesa zetu, lakini sio media players.

Waziri wa Sheria Prof. Plamagamba Kabudi amesema haifai kuwataja marais Mkapa na Kikwete kwa kuwa heshima yao inatunzwa kwa kuwa wamekuwa wakuu wa nchi, wakuu wa serikali na maamiri wajeshi wakuu na heshima hiyo inafaa kutunzwa kikatiba, kisheria, kimaadili, kiutamaduni na kiutu na ndio maana hata ripoti haijawataja sehemu hata moja

Hivyo haifai kuacha kujadili mambo yaliyo mbele yetu na kuwajadili wakuu hawa wastaafu

 
Ni Tanzania Pekee raisi ndio yupo juu ya sheria hata kwa uonvu wa aina gani, kabidi bila haya anakingia kifua maovu huku wakituaminisha kua "No one is above the law'"
 
Waziri wa Sheria Prof. Plamagamba Kabudi amesema haifai kuwataja marais Mkapa na Kikwete kwa kuwa heshima yao inatunzwa kwa kuwa wamekuwa wakuu wa nchi, wakuu wa serikali na maamiri wajeshi wakuu na heshima hiyo inafaa kutunzwa kikatiba, kisheria, kimaadili, kiutamaduni na kiutu na ndio maana hata ripoti haijawataja sehemu hata moja

Hivyo haifai kuacha kujadili mambo yaliyo mbele yetu na kuwajadili wakuu hawa wastaafu


Sasa haya mambo yanakosa maana kuyajadili kama waanzilishi na walioshinikiza bunge letu kufikia maamuzi ambayo leo yanaitwa uwizi HAKUNA HAJA KUYAJADILI KWA SABABU TAYARI YAMEKUWA YA KIBAGUZI.

Only in Tz, aliyidhinisha hana hatia bali mtekelezaji
 
Nijuavyo mheshimu anayejiheshimu,heshima pia hujengwa kama Mtu hajajenga kuheshimiwa haiwezekani kuheshimiwa, na heshima haitafutw bali kwa matendo,sasa kama matendo yao yalikuwa ya ovyo tusitegemee Kabudi kuwalazimisha Watu kuwaheshim,Mtu/Watu hawawez kufanya madudu kwa kisingizio cha walikuwa wakuu wa Nchi hivyo waheshimiwa,na ni aibu Mtu mwenye akil timamu na anayejiita mbobez wa sheria kulitamka hilo,anatulazimisha tuamin kuna Watu wapo juu ya sheria.
 
CCM kwa wingi wao na 'uzalendo' pale bungeni,is a high time sasa kudai mabadiriko ya kikatiba,former presidents waondolewe kinga,waungane na wale waliotajwa katika 'mashtaka ya uhujumu uchumi'.
 
Je wao waliwaheshimu watanzania,kwa kiwango cha hasara tuliyopata hawasitahili hata chembe ya heshima.tuliwakabidhi dhamana kusimamia nchi wamejitajirisha na familia zao.watanzania wangapi wamekufa kwa kukosa huduma mbalmbali.na kama hamuwezi kuwaondolea kinga tuacheni tuseme tuandike nafsi zetu zipoe
 
Kabudi amekuwa mjingaeeeh?
Sababu za prof. Hazina mantiki kabisa. Maraisi wastaafu wanalindwa na katiba hivyo hata ukiwataja bado wanalindwa na hakuna cha kufanya. Hivyo prof. Kusema sijui ni maadili au sijui waachwe wapumzike haina mashiko kabisa. Huhitaji kuwa na phd ya sheria kulijua hili. Kama tukifuata ushauri huu ina maana wazee waliofanya makosa ya jinai tuwaache tu kisa si " maadili" kuwatuhumu wazee!
 
Back
Top Bottom