Profesa Kabudi amtembelea Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, wasema uchaguzi umekwisha sasa kazi tu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
Waziri wa foreign affairs Prof Kabudi na watendaji wakuu wa wizara yake wamekutana na makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar maalim Seif na kukubaliana kuchapa kazi kwa pamoja.

Maalim Seif amesema uchaguzi umekwisha aliyepata kapata na aliyekosa amekosa cha muhimu ni watanzania kuungana pamoja katika kujiletea maendeleo.

Naye Prof Kabudi ameihakikishia Serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar kuipa kila aina ya ushirikiano itakaohitaji ikiwemo kuutangaza utalii wa Zanzibar kimataifa.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Tunabadilishana tu, wengine wapo Serikalini wengine wapiga pesa ya ruzuku na yote ni kwa mujibu wa Katiba.
 
Hili ni jambo jema kabisa. Shida kubwa ni kuwa 'walioshinda" wamejifunza nini katika uchaguzi uliopita?Wana majuto na nia njema ya kurekebisha mambo au wanatafiti mbinu ingine kali zaidi ya kushinda hata pale wasiposhinda?

Kwa Prof.Kabudi najua wazi kuwa si mwana diplomasia lakini inabidi ajifunze diplomasia hasa kutokana na haya matangazo ya mara kwa mara kutoka kwa mabeberu.

Kabudi amsaidie Rais na ianelekea wakati Nyerere anaanzisha azimio la Arusha Rais wetu alikuwa shule ya msingi na wakati Azimio la Arusha linafeli Rais wetu alikuwa akifundisha somo gumu sana la Chemistry (hakuwahi kupata muda wa kusoma mambo ya penguin).

Serikali kuingia kufanya biashara ni kosa la kujirudia na serikali kutaka kumiliki njia kuu za uchumi tunarudi kule kule.
Hapa ni kwetu!!
 
Hili ni jambo jema kabisa.Shida kubwa ni kuwa 'walioshinda" wamejifunza nini katika uchaguzi uliopita?Wana majuto na nia njema ya kurekebisha mambo au wanatafiti mbinu ingine kali zaidi ya kushinda hata pale wasiposhinda?..
Nimekuelewa bwashee lakini serikali haifanyi biashara kwa sababu hailipi kodi bali wanawezesha muuzaji na mnunuzi kukutana katikati.
 
Waziri wa foreign affairs Prof Kabudi na watendaji wakuu wa wizara yake wamekutana na makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar maalim Seif na kukubaliana kuchapa kazi kwa pamoja.

Maalim Seif amesema uchaguzi umekwisha aliyepata kapata na aliyekosa amekosa cha muhimu ni watanzania kuungana pamoja katika kujiletea maendeleo.

Naye Prof Kabudi ameihakikishia serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar kuipa kila aina ya ushirikiano itakaohitaji ikiwemo kuutangaza utalii wa Zanzibar kimataifa.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
... USHIRIANO HUO KWIYO!!
 
Prof Kabudi ni mwalimu " mkuu " wa Tundu Lisu!
Ilikuwaje akaokotwa Jalalani? akajiita wa kutoka Jalalani? You might be well informed of this!
University Mwalimu ni "instructor".. siyo kama primary. University education is in the books
 
Hatuna sababu ya kugombea fito.
Tujenge taifa letu bila kujali makando kando ya kisiasa.
Yaliyopita si ndwele tuagange yajayo
 
Back
Top Bottom