Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,884
Hivi sababu zilizotufanya tukatae "dual citizenship' hapo awali zime'expire' (zimeisha muda wake) ama bado?
Hivi kama unaipenda nchi yako....kwa nini unaahaa kutafuta nchi uraia wa nchi nyingine...hivi mnajua kwa nini nchi zilizoendelea zinapenda dual citizenship...? Raia wake karibu wote wanaouwezo wakukabliana na yeyote kiuchumi nakadhalika,Tanzania tuna rasilimali nyingi watanzania wengi hawawezi kukabiliana kiuchumi na yeyote...kitendo cha kuruhusu dual citizenship..maana yake sasa hata Mmarekani , mchina ana haki ya kuomba uraia hapa na kupewa huku akiendela kuwa mchina....mmarekani ki-uraia. Naye atataka fursa sawa na mtanzania hoehae (ambao tuko wengi) katika nyanja za kiuchumi...hivyo yeye kwakuwa anao uwezo wakiuchumi atafaidika zaidi na rasilima zetu kuliko wenyeji wa nchi hii. Ili litatudidimiza kabisa...tukubali kuwa na Dual citizenship tukishajiridhisha kuwa Watanzania karibu wote sasa wanao uwezo wakukabiliana na raia yeyote yule hapa Ulimwenguni katika ushindani wa kiuchumi...
Kwa ufupi, Tanzania, hatujawa tayari kuwa na Dual Citizenship...kwa sababu nilizozitoa hapo juu.
....."hivyo kwakuwa yeye ana uwezo wa kiuchumi utatudidimiza...."
Unamaanisha nini!?
Na huo uwezo wa Watanzania kukabiliana na raia yeyote wa kigeni una maanisha nini?
Ngoja nikupe mtazamo wangu.
Kwanza;
Kinachoombwa hapa, ni sheria iwaruhusu Wa Tanzania wanaoishi nje wasipoteze uraia wao kwakuwa tu wamepata haki za uraia huko waliko!
Pili;
Watanzania hawa waliopata sifa za kupata uraia huko nje, wengi "wapo tayari kukabiliana" na changamoto zinazoletwa na raia wasio wazawa lakini wanapata Uraia wa Tanzania bila kuathiri uraia wa nchi walizotoka.
#MosKwito !