Profesa BAREGU ndiye kinara wa kupinga dual citizenship

hata siafiki dual citizenship. wenye uraia wa nchi zingine ni watoto wa vigogo ambao wanataka kuwa na uwezo wa kugombea uongozi baada ya kupata mafanikio ugaibuni. hawa si wazalendo hata kidogo lazima tuwaogope kama ukoma.
ndugu yangu hakuna mtoto wa kigogo wala wa kinyamwezi alioko bado diaspora!!wote wamerudi huko kuja kula mali walizoiba baba zao,akae ulaya afanye nn na neema mnazo huko???fanyeni analyis za kutosha kabla ya kutype msg yako.walioko ulaya ni watoto wa wakulima na wafanyakazi wa kawaida na wana uchungu sana na nchi yao Tanzania ila kwa sababu za kiuchumi na kijamii wanashindwa kurudi haraka..wapeni duo citizenship mtawaona!!
 
Mdau Arigold,
sasa kwa kuwa hapa we dare TALK OPENLY nathubutu kumtaja kuwa ni profesa BAREGU sababu zake hazina msingi. kama kweli tuko serious kwa nini tusifanye kama CHINA au ISRAEL au NIGERIA au KENYA au ETHIOPIA tukawatumia hawa diaspora?

Nitaanisha sababu za nchi tajwa kushabikia dual citizenship:

  • Kenya hawana ardhi, maana ardhi inahodhiwa wachache, sera ya kupeleka wa-Kenya nje kuwa diaspora ilianzishwa na ma-settler Kenya baada ya kutwaa ardhi kubwa na kuona Tanganyika ni sehemu ya kuwapeleka waKenya. Mzee Kenyatta pia alipenda kuona waKenya wahamie Tanzania kutokana na sera tata za Mkoloni mweusi wa Kenya na mpaka leo inakuja kwa kubebwa na East African Community Revival. Marehemu Tom Mboya miaka ya 1960 walianzisha Air-lift kubwa kuwapeleka vjjana vyuoni Marekani na Obama ni mtoto wa operesheni hiyo inayosababisha diaspora kubwa ya waKenya USA kuanzia miakaya 1950 mwishoni.

    M
  • Israel wao wana wafanya biashara wakubwa nje kama Mark Rich, Wa-Israeli wamehodhi biashara ya Almasi huko Belgium, Mabenki France, UK , USA n.k kuneemesha uchumi wao. Ku-lobby ndo wenyewe mitaa maarufu jijini Paris, France ina majina kama Ben Gurion mwasisi wa Taifa la Israel Mashariki ya Kati.
  • Ethiopia wana maelfu ya wakimbizi kutokana na Mapinduzi yaliyogoa Mfalme Haile Sellasie mwaka 1974 na hivyo baada ya miaka 40 ughaibuni wamekuwa na uwezo kibiashara, kielimu n.k kusaidia nyumbani.
  • Nigeria, mlolongo wa mapinduzi ya kijeshi miaka ya 1960, 1970 na vita ya Biafra imesababisha kuwa na diaspora kuwa Ulaya na Marekani ifikiayo mamilioni kwa zaidi ya miaka 50 kama Ethiopia.
  • China, raia zake wamehodhi uchumi wa nchi nyingi kama ukienda The Philipines, Malaysia, Singapore n.k hivyo watasadi uchumi wa nyumbani.
Swali Kuu, Je , kuna maelfu ya wa-Tanzania wangapi walioishi ughabuni miaka zaidi ya 30 ambao wameweza kuhodhi ughaibuni biashara kubwa, wameajiriwa ktk taasisi nyeti kuweza ku-lobby (kuiunganishia ulaji) Tanzania, ni wabunge ughaibuni, madaktari, wanasheria mahiri ughaibuni?

Jibu ni kuwa Watazania wengi ni watu wa kawaida hata nyumbani Tanzania hawatambuliki kuwa wanaweza kuleta Mabadiliko Makubwa kwa Haraka hivyo basi muda wa Dual citizenship kuifaidisha Tanzania bado haujafika na suala hili litiwe kapuni labda lirejeshwe kujadiliwa baada ya miaka 50 kupita kuanzia sasa.
 
Mlishakana Tanzania na kuiona takataka mkachagua nchi mlioonabora kwenu endeleeni huko huko wasaliti nyie km mnaipenda Tanzania mukane uraia Wa huko uliko
 
Huyo rais kilaza tu kwa sababu prof mmoja anamyumbisha???

Hata hivyo wanaoshadidia uraia wa nchi mbili ni mafisadi ambao wanataka watakapobamwa watakimbilia nchi hiyo nyingine
 
Mlishakana Tanzania na kuiona takataka mkachagua nchi mlioonabora kwenu endeleeni huko huko wasaliti nyie km mnaipenda Tanzania mukane uraia Wa huko uliko

Hivi, una habari Mtanzania aliye na uraia wa Marekani, Uingereza, UAE, Oman etc hata atapoomba tena uraia wa Tanzania ---haumpotezei sifa ya kuwa raia wa nchi hizo?

#MosKwito !
 
Kwa wanao-support dual citizenship, naomba mtutajie hasara za kuwa na Dual citizenship system kwenye nchi.

Na support dual Citizenship, faida ni kubwa kiasi kwamba hakuna hasara kwa nchi, ila nitakupa mfano mdogo sana...

Wewe MtamaMchungu na wengine mnaopinga, nyie si waTanzania? Hebu niorodheshee haki zako za uraia wa JMT katika Nchi ya #Zanzibar .

Na uhakika wengi wenu mwaupinga Uraia wa nchi mbili ingawa wenyewe humu nchini kuna haki za msingi mnazikosa.

#MosKwito !
 
Last edited by a moderator:
Wazungu na wahindi wanaoukuja na kupewa uraia huwa wana ukana uraia wa nchi zao ndio wanapewa uraia wa tanzania...kama unaitamani tanzania kana uraia wa ughaibu upata wa tanzania sidhani kama utanyimwa

Kuukana uraia wa kigeni haukuondoshei haki yako ya Uraia wa nchi hizo ambazo zimeruhusu dual citizenship

#MosKwito !
 
kwa kuzingatia MSLAHI YA TAIFA LETU CHANGA, napinga HOJA ya Kuwa na DUAL CITIZENSHIP , hatuhitaji kwa sasa, hatuwezi kuzihimili changamoto hizo..
 
Changamoto zipi hizo ambazo unahofia wazaliwa wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi watazileta?

#MosKwito !
 
mtoa mada nadhani anaishi nje na ameshapoteza uraia wa tanzania,pole ndugu,kati ya watanzania 49million,ni watanzaia 400 tu watakaokubali hiyo dhana,haina maana kwetu,unataka kuwa mtanzania kana kwanza uraia wako,hatuwezi kuhatarisha usalama wetu na ardhi yetu kirahisi,hata kama kikwete anaunga mkono,ukweli ni kwamba wananchi wengi hawataki na hii ndio demokrasia
 
Kwa hiyo wananchi wengi wakisema Albinos wasipewe ajira tufanye hiyo? Au wananchi wengi wakisema wachaga waporwe mali zao ni sawa hiyo? Hiyo ni mob rule wanaita. Tatizo mnaopinga hii ishu kwa maslahi yenu binafsi mnapotosha jamii. Hii ishu ikijadiliwa kinaga ubaga, na wananchi wakielemishwa sidhani kama wengi watapinga.
 
Nitaanisha sababu za nchi tajwa kushabikia dual citizenship:

  • Kenya hawana ardhi, maana ardhi inahodhiwa wachache, sera ya kupeleka wa-Kenya nje kuwa diaspora ilianzishwa na ma-settler Kenya baada ya kutwaa ardhi kubwa na kuona Tanganyika ni sehemu ya kuwapeleka waKenya. Mzee Kenyatta pia alipenda kuona waKenya wahamie Tanzania kutokana na sera tata za Mkoloni mweusi wa Kenya na mpaka leo inakuja kwa kubebwa na East African Community Revival. Marehemu Tom Mboya miaka ya 1960 walianzisha Air-lift kubwa kuwapeleka vjjana vyuoni Marekani na Obama ni mtoto wa operesheni hiyo inayosababisha diaspora kubwa ya waKenya USA kuanzia miakaya 1950 mwishoni.

    M
  • Israel wao wana wafanya biashara wakubwa nje kama Mark Rich, Wa-Israeli wamehodhi biashara ya Almasi huko Belgium, Mabenki France, UK , USA n.k kuneemesha uchumi wao. Ku-lobby ndo wenyewe mitaa maarufu jijini Paris, France ina majina kama Ben Gurion mwasisi wa Taifa la Israel Mashariki ya Kati.
  • Ethiopia wana maelfu ya wakimbizi kutokana na Mapinduzi yaliyogoa Mfalme Haile Sellasie mwaka 1974 na hivyo baada ya miaka 40 ughaibuni wamekuwa na uwezo kibiashara, kielimu n.k kusaidia nyumbani.
  • Nigeria, mlolongo wa mapinduzi ya kijeshi miaka ya 1960, 1970 na vita ya Biafra imesababisha kuwa na diaspora kuwa Ulaya na Marekani ifikiayo mamilioni kwa zaidi ya miaka 50 kama Ethiopia.
  • China, raia zake wamehodhi uchumi wa nchi nyingi kama ukienda The Philipines, Malaysia, Singapore n.k hivyo watasadi uchumi wa nyumbani.
Swali Kuu, Je , kuna maelfu ya wa-Tanzania wangapi walioishi ughabuni miaka zaidi ya 30 ambao wameweza kuhodhi ughaibuni biashara kubwa, wameajiriwa ktk taasisi nyeti kuweza ku-lobby (kuiunganishia ulaji) Tanzania, ni wabunge ughaibuni, madaktari, wanasheria mahiri ughaibuni?

Jibu ni kuwa Watazania wengi ni watu wa kawaida hata nyumbani Tanzania hawatambuliki kuwa wanaweza kuleta Mabadiliko Makubwa kwa Haraka hivyo basi muda wa Dual citizenship kuifaidisha Tanzania bado haujafika na suala hili litiwe kapuni labda lirejeshwe kujadiliwa baada ya miaka 50 kupita kuanzia sasa.

Siyo lazima wawe maarufu ndiyo walete mabadiliko. Kama wakifanya kazi na kutuma hela nyumbani (remittances) watasaidia uchumi. Kama mbeba boski anatuma mfano euro 500 (euro 6000 per annum) kila mwezi kwa familia yake kule kijijini, hi si ni hata zaidi ya yule mtalii mzungu anayekuja mara moja kwa mwaka na kulipa airport taxes, na kiingilio cha mbugani? Huyu mbeba boksi si atasomesha mdogo wake shule? Mdogo wake akimaliza shule si atachangia kwenye uchumi akianza kazi?
 
Sio kutuma pesa tu, ile haki ya kuajiriwa Tanzania na kutumia discipline, experience na exposure aloipata nje ya nchi kuboresha uzalishaji ni mchango tosha.

#MosKwito !
 
Nitaanisha sababu za nchi tajwa kushabikia dual citizenship:

  • Kenya hawana ardhi, maana ardhi inahodhiwa wachache, sera ya kupeleka wa-Kenya nje kuwa diaspora ilianzishwa na ma-settler Kenya baada ya kutwaa ardhi kubwa na kuona Tanganyika ni sehemu ya kuwapeleka waKenya. Mzee Kenyatta pia alipenda kuona waKenya wahamie Tanzania kutokana na sera tata za Mkoloni mweusi wa Kenya na mpaka leo inakuja kwa kubebwa na East African Community Revival. Marehemu Tom Mboya miaka ya 1960 walianzisha Air-lift kubwa kuwapeleka vjjana vyuoni Marekani na Obama ni mtoto wa operesheni hiyo inayosababisha diaspora kubwa ya waKenya USA kuanzia miakaya 1950 mwishoni.
    .

habari ndio hiyo,
Naukiangalia CLIP ya kwanza utaona huyo dada analia kuhusu ARDHI.
 
Sio kutuma pesa tu, ile haki ya kuajiriwa Tanzania na kutumia discipline, experience na exposure aloipata nje ya nchi kuboresha uzalishaji ni mchango tosha.

#MosKwito !

Kwani wamekatazwa? mbona wakenya na wazungu, wahindi wa aarabu kibao wameajiriwa huku bongo?
 
Msimsingizie prof baregu, jamani mpinzani wa dual citizenship ni rafiki wa karibu wa jk mwenyewe na mzaliwa wa kanda ya kati-dodoma anayeitwa prof paramagamba kabudi. Alishahojiwa na kipindi cha kiingereza cha cha mzee simbeye cha tbc akasema wazi kuwa yeye ni mpinzani wa hili suala asiyejificha
 
Back
Top Bottom