Prof. Tibaijuka: Nijiuzulu kwa lipi?

Prof. Tibaijuka: Nijiuzulu kwa lipi?

jibu ni dogo sana,kama unaelewa vizuri sana utaelewa kuwa shule huwa hazikopesheki,anakopeshwa mdhamini mkuu au mtu binafsi au mwenye shule,ni vigumu sana kuuza shule kama ikikosa kurudisha deni ikiwa imekopa bank,ndio maana wanataka mdhamini kwa bank zinazo jielewa ili iwe rahisi kuuza assets zake akishindwa kulipa deni,ndivo ilivo kuwa kwa shule ya barbro,yeye alikopa pesa kama mdhamini mkuu kujenga mabweni,na ruge alisha mwaidi kitambo kuchangia shule ivo akatoa sehemu ya mchango ili deni lipunguzwe


by the way wala hapa hoja sio kama kwanini pesa zimewekwa kwenye account ya waziri,suala ni kuwa je pesa imewafikia walengwa??

Vyombo vinavyo husika wafanye utafiti wao na wathibitishe hilo

Una akili nyingi sana.....:confused2::confused2:
 
Yani mama Tibaijuka sioni kosa lake kabisa. Wengi hapa tunachangia kwa hisia tu. Tumeambiwa Ruge kashalipia kodi. Pesa kamuwekea kwenye account yake its not an issue hata angeipeleka kwenye account ya shule bado hiyo account mwenye mamlaka ya mwisho ni mama Anna hili jambo lipo ki binafsi sana.
 
Amesema haoni kosa kutafuta mchango wa shule. Yeye alipokea fedha toka kwa Ruge ambaye na kodi alilipa amehoji kama ni fedha haramu inakuwaje TRA wamechukua mpaka kodi yake zaidi ya billion 30. Anasubiri mamlaka ya uteuzi ipime na kuamua. Haoni haja ya kujiuzulu. Amesema hayo akihojiwa na BBC

Huyu ni Prof. gani huyu, TRA wenyewe wamekiri kampuni ni fake hivyo hata hiyo hela iliyochukuliwa ni fake ndiyo maana kamati inataka hela zote zirudi zikiwemo zilizochukuliwa na TRA kama kodi? hivi jamani huyu ni prof wa ukweli????
 
Jamani hizo shule si ni za mtu binafsi? Ile si mali ya serikali. Yaani mali yangu afu nyie ndo mkae muamue na kupanga jinsi ya ku allocate pesa zangu? Haiingii akilini sana sana ni kushauri tu ila sio eti mkae muanze kupanga wakati mwenye neno la mwisho nipo haiwezekani

Mbona nasikia Babro wanafunzi bado wanalipishwa 5m/ kwa mwaka? Mbona hawajapata unafuu baada ya kupokea 1.6b/? Na bado misaada ya fedha toka Sweden inayoingia shuleni hapo
 
Amesema haoni kosa kutafuta mchango wa shule. Yeye alipokea fedha toka kwa Ruge ambaye na kodi alilipa amehoji kama ni fedha haramu inakuwaje TRA wamechukua mpaka kodi yake zaidi ya billion 30. Anasubiri mamlaka ya uteuzi ipime na kuamua. Haoni haja ya kujiuzulu. Amesema hayo akihojiwa na BBC

Professor una haki kabisa ya kukataa kujiuzuru maana wewe ulipokea pesa safi. Watu wanaokuhukumu wewe wanashindwa kuangalia tatizo lilipotokea. Tatizo ni la kimfumo na code of conduct ambalo lilighubika uamishwaji wa pesa za escrow bila kodi kama ipo. Aliyekupa hizo pesa hata repoti ya CAG haisemi wala PAC kama alikuwa na any influence ya transactions from BOT to PAP. Wewe uliomba msaada wa shule na wanahoji ni kwanini iliingia kwa account yako wakaulize board ya shule na waulize kama pesa hazikufika. Badala ya kuweka effort kwenye kuwasaka waliochukua pesa kwa rumbesa na maboksi toka STANBIC wanaaganaika waliopewa pesa na JR naona hapo kuna tatizo kubwa sana abalo haliwezi kusaidia kuweka mifumo yetu imara
 
jibu ni dogo sana,kama unaelewa vizuri sana utaelewa kuwa shule huwa hazikopesheki,anakopeshwa mdhamini mkuu au mtu binafsi au mwenye shule,ni vigumu sana kuuza shule kama ikikosa kurudisha deni ikiwa imekopa bank,ndio maana wanataka mdhamini kwa bank zinazo jielewa ili iwe rahisi kuuza assets zake akishindwa kulipa deni,ndivo ilivo kuwa kwa shule ya barbro,yeye alikopa pesa kama mdhamini mkuu kujenga mabweni,na ruge alisha mwaidi kitambo kuchangia shule ivo akatoa sehemu ya mchango ili deni lipunguzwe


by the way wala hapa hoja sio kama kwanini pesa zimewekwa kwenye account ya waziri,suala ni kuwa je pesa imewafikia walengwa??

Vyombo vinavyo husika wafanye utafiti wao na wathibitishe hilo
Na mimi naweza kusema imefika au haijafika kwa walengwa hapo serikali haina cha kuhusika nacho ile ni private institutions na inaendeshwa na mtu binafsi. Pesa hazijatoka serikalini zimetoka kwa mtu. Laiti ingekuwa ni serikali ndo imezitoa kungekuwa na haja ya kutafuta hilo jibu kwamba imefika au la. Hii issue iko so personal
 
wasipo jiuzuru basi bunge la feb 2015 tunahamasisha kura ya kutokuwa na imani na rais na si pinda tenda tuwashikishe adabu hawa wezi wakubwa
 
amesema haoni kosa kutafuta mchango wa shule. Yeye alipokea fedha toka kwa ruge ambaye na kodi alilipa amehoji kama ni fedha haramu inakuwaje tra wamechukua mpaka kodi yake zaidi ya billion 30. Anasubiri mamlaka ya uteuzi ipime na kuamua. Haoni haja ya kujiuzulu. Amesema hayo akihojiwa na bbc

wakati unacheza hako kamchezo kachafu ulikuwa unaruka na kukata miuno kwa furaha . Sasa umeshtukiwa unang'aka wee subiri panga likufikie ili ukakate miuno vizuri kwenye hizo shule zako.
 
Mama huyu anamajanga sana hadi naona kumbe ilikuwa sawa kwa serikali kipindi kile cha mkapa kuzuia usajili was BAWATA taasisi aliyokuwa mwenyekiti. Watakuwa walijua huyu mama ni mpigaji. Uwaziri si urithi wake. Aondoke. Mradi wa kigamboni ataumaliza kama ni hivyo
 
viongozi wa bongo ni wabishi sana kuwajibika wakishapata madaraka...
Madaraka matamu hasa kwa nchi kama ya Tanzania ambapo watu tumekuwa waoga sana. Pia ugumu huu wa watu kujiuzuru kuna viashiria vingi sana kuhusiana na mamlaka ya uteuzi ikiwemo
  1. Mamlaka ya uteuzi ni dhaifu
  2. Mamlaka ya uteuzi ina pata mgao katika ufisadi huu, hivyo wateuliwa wanajua kabisa mteuzi hawezi kuwawajibisha kwa sababu ni mshiriki wa uchafu huo
  3. wateuliwa wanajua madudu mengi zaidi ya mamlaka ya uteuzi, na mamlaka ya uteuzi inajua hilo na hivyo kusita kutengua uteuzi
  4. Uteuzi haukuzingatia maadili, msingi wa uteuzi ni kujuana, udini, ushoga, uhawara na pengine au shinikizo kutoka makundi yenye nguvu za kifisadi
  5. Ili kulinda siri na maslahi ya mamlaka ya uteuzi ni lazima hao wateuliwa waendelee kushikilia ofisi ili asiingie mtu mwingine na kuibua maovu zaidi.
kwangu mimi juu ya hili naweza hata andika kitabu
 
Amesema haoni kosa kutafuta mchango wa shule. Yeye alipokea fedha toka kwa Ruge ambaye na kodi alilipa amehoji kama ni fedha haramu inakuwaje TRA wamechukua mpaka kodi yake zaidi ya billion 30. Anasubiri mamlaka ya uteuzi ipime na kuamua. Haoni haja ya kujiuzulu. Amesema hayo akihojiwa na BBC
Uwaziri si ajira ni cheo cha kisiasa na kuwajibika si lazima uwe umetenda kosa, moral.......... Aibu gani na Uprofessa wako, ubingwa kimataifa ung'ang'anie Uwaziri wa ardhi leo. Aibu Prof acha kutuabisha sisi Wahaya. waachie huo uwaziri wao.
 
Mbona nasikia Babro wanafunzi bado wanalipishwa 5m/ kwa mwaka? Mbona hawajapata unafuu baada ya kupokea 1.6b/? Na bado misaada ya fedha toka Sweden inayoingia shuleni hapo
Sasa mkuu hayo ni mambo personal. Suala la uendeshaji wa shule yake iwe gharama sijui misaada hapo hamna namna ambayo anaweza hukumiwa labda uchaguzi tu. Na kinachotuchanganya tunachukulia 1.6 b ni pesa nyingi sana. Ni nyingi kweli lakini kwa matumizi ya shule tena zaidi ya moja ni matumizi ya kawaida. Hata mimi sikubaliani naye ada yake na huduma anayotoa lakini hili jambo liko too personal
 
Amesema haoni kosa kutafuta mchango wa shule.

Yeye alipokea fedha toka kwa Ruge ambaye na kodi alilipa amehoji kama ni fedha haramu inakuwaje TRA wamechukua mpaka kodi yake zaidi ya billion 30.

Anasubiri mamlaka ya uteuzi ipime na kuamua. Haoni haja ya kujiuzulu.

Amesema hayo akihojiwa na BBC

MAAZIMIO YA BUNGE KUHUSU HOJA YA TAARIFA MAALUM YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI MAALUM KUHUSIANA NA MIAMALA ILIYOFANYIKA KATIKA AKAUNTI YA ‘ESCROW' YA TEGETA PAMOJA NA UMILIKI WA KAMPUNI YA IPTL
_____________________________________

1. KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuhusu Ukaguzi Maalum wa Malipo yaliyofanyika katika Akaunti ya Escrow ya Tegeta uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (‘CAG') pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (‘TAKUKURU') imeonesha kwamba kwamba Harbinder Singh Sethi, James Rugemalira (VIP), Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Waziri wa Nishati na Madini, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (‘TANESCO') walihusika kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha kufanyika miamala haramu ya fedha za Akaunti ya Escrow ya Tegeta kwenda kwa makampuni ya Pan African Power Solutions Ltd. (‘PAP'), na VIP Engineering & Marketing (‘VIP');

KWA KUWA, kwa sababu ya kuhusika kwa watu hao na miamala iliyofanyika kwenye Akaunti ya Escrow imeliingizia Taifa hasara ya mabilioni ya fedha za umma zinazotokana na kutokulipwa kwa kodi mbali mbali za Serikali na kushindwa kwa TANESCO kukokotoa upya kiwango cha malipo ya gharama za uwekezaji (‘capacity charges') wa IPTL;

KWA KUWA, mabilioni ya fedha yaliyotolewa kwenye Akaunti ya Escrow yametumika kuwapa kile kinachoonekana kuwa ni rushwa baadhi ya viongozi na maafisa wa serikali kama vile Mawaziri, Majaji, Wabunge, Wenyeviti wa Kamati za Bunge, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi.

NA KWA KUWA, vitendo vilivyofanywa na watu hawa vinaashiria makosa mbali mbali ya jinai kama vile uzembe, wizi, ubadhirifu, kutakatisha fedha haramu, matumizi mabaya ya madaraka, rushwa na kupokea mali ya wizi;

HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, TAKUKURU, Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya ulinzi na usalama viwachukulie hatua stahiki za kisheria, kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, watu wote waliotajwa na Taarifa Maalum ya Kamati kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya Akaunti ya Escrow, na watu wengine watakaogundulika kuhusika katika vitendo hivyo vya jinai kufuatia uchunguzi mbali mbali unaoendelea;

2. KWA KUWA, vitendo vya kijinai wanavyhohusishwa navyo viongozi wa umma na maafisa wa ngazi za juu serikalini vinakiuka pia maadili ya viongozi wa umma na kuwanyima viongozi na maafisa hao uhalali wa kuendelea kushikilia nafasi za mamlaka katika uongozi wa umma;

HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO wawajibishwe, kwa kuishauri mamlaka yao ya uteuzi kutengua uteuzi wao;
3. KWA KUWA, katika watu walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kashfa ya miamala ya Akaunti ya Escrow wapo pia viongozi wa Kamati za Kudumu za Bunge kama vile Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO;

NA KWA KUWA, Bunge na/au Kamati zake za Kudumu zina uwezo na mamlaka, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, ya kuwawajibisha viongozi hawa wa Kamati kwa kuwavua nyadhifa zao;

HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Kamati husika za Kudumu za Bunge zichukue hatua za haraka, na kwa vyovyote vile kabla ya Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge, kuwavua nyadhifa zao Wenyeviti tajwa wa Kamati husika za Kudumu za Bunge;

4. KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha kwamba katika watu waliotajwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kashfa ya miamala ya Akaunti ya Escrow wapo pia Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania;

KWA KUWA, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (‘Katiba') imeweka utaratibu mahsusi wa kushughulikia nidhamu ya Majaji;

KWA KUWA, utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji kwa mujibu wa Katiba unamtaka Rais kuunda Tume ya Uchunguzi ya Kijaji kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya Majaji;

NA KWA KUWA, utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji kwa mujibu wa Katiba unamruhusu Rais kumsimamisha kazi Jaji au Majaji husika wakati uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea;

HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aunde Tume ya Kijaji ya Uchunguzi kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania;

5. KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha kwamba Stanbic Bank (Tanzania) Ltd. ilishiriki kupokea na kutakatisha fedha zilizotolewa kwa njia haramu kutoka katika Akaunti ya Escrow na kupelekwa katika akaunti zilizofunguliwa na PAP katika benki hiyo;

KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha kwamba akaunti za PAP katika Stanbic Bank Tanzania Ltd. zimekwishafungwa baada ya fedha zote zilizotolewa katika Akaunti ya Escrow kumalizika na Akaunti ya ya VIP katika Mkombozi Commercial Bank imebakiza kiasi fulani cha fedha;

NA KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati inaonesha kwamba kuna uwezekano fedha zilizotolewa kutoka kwenye akaunti za PAP na VIP zilipelekwa katika benki nyingine;

NA KWA KUWA, vitendo vya Stanbic Bank (Tanzania) Ltd., na benki nyingine kupokea na kutakatisha fedha zilizotolewa kwenye Akaunti ya Escrow ni vitendo vya jinai kwa mujibu wa Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu;

HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, mamlaka husika za kifedha na za kiuchunguzi ziitaje Stanbic Bank (Tanzania) Ltd. na benki nyingine yoyote itakayogundulika, kufuatia uchunguzi wa mamlaka za kiuchunguzi, kujihusisha na utakatishaji wa fedha zilizotolewa katika Akaunti ya Escrow, kuwa ni taasisi zenye shaka ya utakatishaji wa fedha haramu (institutions of money laundering concern);

6. KWA KUWA, vitendo vya wizi, ubadhirifu wa mali ya umma, hujuma ya uchumi na ufisadi vimeongezeka, kushamiri na kushirikisha viongozi wa kisiasa na maafisa wa serikali pamoja na wafanya biashara wakubwa;

KWA KUWA, kwa mujibu wa sheria iliyoiunda, TAKUKURU inashughulikia vitendo vya aina zote za rushwa zikiwemo rushwa ndogo ndogo (petty corruption) na rushwa kubwa na ufisadi (grand corruption) na matumizi mabaya ya madaraka;

NA KWA KUWA, kwa sababu ya majukumu yake mapana kisheria, TAKUKURU inaelekea kuelemewa katika vita ya kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi zinazotishia uhai wa taifa letu kiuchumi, kijamii na kisiasa;

HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Serikali iandae na kuwasilisha Muswada wa marekebisho ya Sheria iliyoiunda TAKUKURU kwa lengo la kuanzisha taasisi mahsusi itakayoshughulikia, kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi zinazotishia uhai wa taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa;

7. KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha jinsi ambavyo TANESCO imekuwa ikitumia mabilioni ya fedha kulipa gharama za umeme unaozalishwa na IPTL na hivyo kuathiri hali ya kifedha ya Shirika hilo;

KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati inaonesha kwamba TANESCO itaendelea kulipa fedha nyingi kwa ajili ya gharama za umeme huo wa IPTL;

HIVYO BASI, Bunge linaazimia kwamba Serikali iangalie uwezekano wa kununua mitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO kwa lengo la kuokoa fedha za Shirika hilo.

8. KWA KUWA, kwa miaka mingi mikataba mibovu ya kuzalisha umeme kati ya TANESCO na makampuni binafsi ya kufua umeme imeisababishia TANESCO hasara ya mabilioni ya fedha na hivyo kutishia uhai wake wa kifedha;

KWA KUWA, Bunge lilikwishaazimia kwamba serikali iwasilishe mikataba husika Bungeni au kwenye Kamati zake kwa lengo la kuliwezesha Bunge kutekeleza vyema wajibu wake wa kuisimamia na kuishauri serikali;

NA KWA KUWA, Serikali haijatekeleza Azimio hilo la Bunge hadi sasa;

HIVYO BASI, Bunge linaazimia kwamba Serikali itekeleze Azimio husika la Bunge mapema iwezekanavyo na kwa vyovyote vile kabla ya kumalizika kwa Mkutano wa Bunge la Bajeti Serikali iwasilishe taarifa ya utekelezaji wa mapitio ya mikataba ya umeme.
 
Amesema haoni kosa kutafuta mchango wa shule. Yeye alipokea fedha toka kwa Ruge ambaye na kodi alilipa amehoji kama ni fedha haramu inakuwaje TRA wamechukua mpaka kodi yake zaidi ya billion 30. Anasubiri mamlaka ya uteuzi ipime na kuamua. Haoni haja ya kujiuzulu. Amesema hayo akihojiwa na BBC

Mbona kwenye hiyo account zilidumu kwa saa48 tu? lete matumizi ya hizo fedha na risiti, kabla mbona ulisema hujuwi zimetoka kwa nani? Rugemalila ulijuwaje tena? kwanini hukutangaza umepokea fedha alokutumia hukumjuwa kabla huyu mama ni mwizi na hatoki
 
Watu kweli wanakazi. Unaamini kweli MTU anaweza kugawa 1.6 billion. Tena baada ya kupata mgawo. Duu kweli tumefika pabaya . ni either taifa limeoza au watu wamehongwa kutetea msimamo wa mama. Hili ni kosa kubwa LA kimaadili kwa waziri unayeshiriki vikao vya cabinet na
 
Amesema haoni kosa kutafuta mchango wa shule.

Yeye alipokea fedha toka kwa Ruge ambaye na kodi alilipa amehoji kama ni fedha haramu inakuwaje TRA wamechukua mpaka kodi yake zaidi ya billion 30.

Anasubiri mamlaka ya uteuzi ipime na kuamua. Haoni haja ya kujiuzulu.

Amesema hayo akihojiwa na BBC

lakini kweli. tra nao wawajibishwe maana wamelamba haramu
 
Ni kama yule alie tuhumiwa kumpa mimba mbunge mwenzie na ikatangazwa kuwa ni personal issue haihusiani na chama (utendaji wake).

Vivyo hivyo huyu mama amepewa pesa kusaidia shule, alie toa pesa amelipa kodi, suala la hiyo pesa imefika kwa wahusika au la halituhusu labda alie toa hizo pesa anaweza akauliza.

Judgement ifanyike bila matumizi ya hisia.
 
Back
Top Bottom