Prof. Tibaijuka: Nijiuzulu kwa lipi?

Prof. Tibaijuka: Nijiuzulu kwa lipi?

Stanley.

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2011
Posts
659
Reaction score
305
Amesema haoni kosa kutafuta mchango wa shule.

Yeye alipokea fedha toka kwa Ruge ambaye na kodi alilipa amehoji kama ni fedha haramu inakuwaje TRA wamechukua mpaka kodi yake zaidi ya million 30.

Anasubiri mamlaka ya uteuzi ipime na kuamua. Haoni haja ya kujiuzulu.

Amesema hayo akihojiwa na BBC
 
Amesema haoni kosa kutafuta mchango wa shule. Yeye alipokea fedha toka kwa Ruge ambaye na kodi alilipa amehoji kama ni fedha haramu inakuwaje TRA wamechukua mpaka kodi yake zaidi ya billion 30. Anasubiri mamlaka ya uteuzi ipime na kuamua. Haoni haja ya kujiuzulu. Amesema hayo akihojiwa na BBC

Tanzania?..Tanzania ni Nchi ya amani sana mkuu!
 
Wakati unapewa zawadi/mchango huo kama ungekuwa msafi kwanini hukutangaza???? umevunja maadili na WAJIBIKA!!!!!!!!!!!
 
Hapo ndipo wabunge watafahamu kosa walilofanya la kuachia "mamlaka ya uteuzi" kufanya maamuzi! Hafanyi ng'o!
Bunge halina mamlaka zaidi ya hapo walipofikia. Bunge haliwezi kutengua uteuzi wa jaji mkuu, waziri, katibu wa wizara. Halina mamlaka hayo. Bunge LINASHAURI SERIKALI au mamlaka ya uteuzi yaani raisi kuamua kutengua au kutotengua uteuzi wa hao wahusika.
 
viongozi wa bongo ni wabishi sana kuwajibika wakishapata madaraka...

Na safari hii mawaziri wamekomaa mpaka dakika ya mwisho hakuna kuachia ngazi. Huenda wanauhakika na walifanyalo.
 
Bunge halina mamlaka zaidi ya hapo walipofikia. Bunge haliwezi kutengua uteuzi wa jaji mkuu, waziri, katibu wa wizara. Halina mamlaka hayo. Bunge LINASHAURI SERIKALI au mamlaka ya uteuzi yaani raisi kuamua kutengua au kutotengua uteuzi wa hao wahusika.

Vipi Rais hasipotengua si ataingia kwenye mgogoro na bunge.
 
Kwa nini shule yake?kuna mishule ya kata haina hata madawati,leo yako ya ada ya 4.5m.tumia akili wewe mama
 
Binafsi sina imani sana na jk katika suala hili, mpaka leo jk anasubiri nini kutekeleza maamuzi ya bunge? Hawa wahalifu kina muhongo, maswi na huyu tibaijuka bado wanakalia ofisi za umma ilhali wametuhumiwa, hili sio sawa kamwe!
 
Kwani shule haina account bank?kwa nini pesa haikulipwa shule moja kwa moja?alivyozichota alipeleka wapi?aweke ushahidi

Kwani kuna kosa hata kama alipewa yeye?Kwani kuna sheria yoyote inazuia mtu asipewe hela?HUYU ALITANGAZA KUPEWA HII NA ILIKUWA WAZI.NADHANI MAMBO HAYA YANA AJENDA NYINGINE.UKIFANYWA UCHUNGUZI WA KITAALAM NINA UHAKIKA HAWA WATU WALIOGAWIWA FEDHA HAWANA MAKOSA YA WAZI.HV KWA AKILI TU YA KAWAIDA UTAMWONDOAJE GAVANA NA MKURUGENZI WA TANESCO ALAFU UHANGAIKE NA WATU WALIOPEWA HELA AMBAZO BADO KUNA RUMU HAZIKUWA H9O ZA ESCROW.
 
..labda wameshamtisha kwamba wakitimuliwa basi wanaanika uchafu wa Serikali yote hadharani. Ngoja tuone leo kama kutakuwa na tamko kutoka Ikulu.

Back
Top Bottom