Naomba nikuweke sawa kidogo kwani kuna mambo umeyasahau kidogo.
Tanganyika na Znz zimeungana kimkataba na sio kikatiba. Kuna mambo yamo katika mkataba huo nayo ndio mambo ya muungano. Suala la ardhi na makazi si suala la Muungano na ndio maana Znz kuna waziri wa wizara hiyo na Bara yupo.
Kumbuka kuwa Mamlaka ya Tibaijuka mwisho wake ni Chumbe akiwa Znz hana mamlaka yoyote ukilinganisha na waziri wa mambo ya nje au mambo ya ndani. hawa wana malka kote kote.
Kumbuka vile vile Znz ni nchi kamili yenye mamlaka kamili na hilo limebainishwa katika katiba ya Znz. Kwa msingi huo Katiba hiyo hiyo imeanisha eneo la Znz kiufasaha kabisa. sasa kwa ombi hilo la Tibaijuka ni lazima katiba ya Znz itabidi ibadilike kwa kuongeza eneo la milki yake au kupunguza miliki yake na hapo ili kubadilisha kipengele hicho cha katiba lazima BLW litahusika vilivyo kwani wao ndio wtunzi wa sheria za Znz na mambo yote yaliyo nje ya muungano.
Kumbuka kuwa katika Picha walopiga kule UN wakti wanawakilisha alikuweo Tibaijuka, balozi wa Tz katika UN, Mbunge wa Mafia na Katibu wa wizara kutoka Znz. Kwa mantiki hiyo inaonekana wazi Prof Tibaijuka alipata baraka zote za Bunge la Muungano dio maana akachukua muwakilishi wa Bunge.
Sasa upande wa BLW hawakuwa na taarifa zozote ongezeka hilo officially na aliku husishwa kwa lolote lile kitu ambacho Jussa amehoji. Ikumbukwe kuwa maombi haya yakifanikiwa lazima BLW litahusishwa katika kupitisha sheria za ongezeko la eneo la miliki la Znz.
sasa labda tujiulize.
Je Znz itaongezewa kiasi gani katika hicho kilicho ombwa? hilo ni suala ambalo limegubikwa na utata mkubwa na alijabainishwa katika mkataba au mbi hilo.
Lakini pia lazima ufahamu kuwa Tz na Znz zote zinaongozwa na Rules of Law. Na mihimili yote mikuu inajipambanua yaani Serikali, Bunge na Mahakama bila kuingilia katika utendaji kazi wake. Kila muhimili unajitegemea.
Limeanza baraza la wawakilishi kuhoji Serikali ya Znz kisha uzi utafuata. Kwani majibu ya Serikali ndio yatatoa mwangaza kwa sakata hilo. Lakin all in all Tibaijuka lazima ajiuzuru hapo.
Kwani mtiririko wa jambo hili unakuwa sawa kabisa na ule wa Tz kujiunga na OIC.