Prof. Shivji Aukosoa Mchakato wa Katiba Mpya!- Aliponda Bunge la Katiba!. Watch ITV/TBC-1!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,556
2,000
Salaam,

Kwa wenye access na ITV, Watch ITV now, Prof. Issa Shivji, anashusha mhadhara kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya.

Kwa wale ambao mtakikosa kipindi hiki leo saa hizi hapa ITV, angalieni TBC-1 kesho saa 1:30 usiku.

Please Watch.

Pasco.

NB. Vipindi hivi vitakujia kila siku saa 1:30 TBC-1 na ITV siku za Alhamisi na Ijumaa saa 1: 00 usiku.

UP DATE
Sehemu ya pili ya mada ya Prof. Shiji na Mchakato wa Katiba Mpya kinaendelea ITV saa hizi na kitakuwepo TBC-1 saa 1:30. Leo Prof. Shivji anajibu maswali ya washiriki.
Karibuni tuendelee.

Prof. Shivji anasema msingi mkuu wa katiba ni "dira ya kitaifa ". Anasema huwezi kuingia kwenye mchakato wa katiba mpya bila kuwa na dira ya kitaifa. Mchakato wa kukusanya maoni ulitakiwa utanguliwe kwanza na "mjadala wa kitaifa kuweke dira", ndipo sasa tutengeneza katiba inayoweka dhima ya kuitekeleza hiyo dira!.

Amesema, pamoja na mchakato huu wa katiba kuanza bila dira rasmi, lakini kwa vile baadhi wajumbe wa kamati hiyo ni watu we mitazamo tofauti tofauti na kuna wenye misimamo thabiti, hivyo japo tumeanza bila dira, lakini bado tunaweza kupata katiba nzuri kama mbele ya safari tutajadili dira ya taifa na ikaingizwa!.

Ameitaja misingi mikuu minne ya katiba nzuri, ikianzia na uhuru, haki, usawa na udugu au ujamaa.
Uhuru: Huu ni uhuru wa mtu binafsi, lengo zima la uhuru limejengwa kwenye misingi ya haki za binaadamu, maada ya dhana ya uhuru, pia ni uhuru wa nchi, uhuru wa taifa, uhuru wa jamii!. Kama nchi haiko huru, then watu wake hawawezi kuwa huru!. Japo taifa limepata uhuru wa nchi, yaani independence, lakini taifa hilo likawa halijajikomboa kiuchumi, "libarated", huwezi kujidai eti una uhuru!. Zaidi ya nchi kupata uhuru, ili nchi iwe na uhuru wa kweli lazima watu wake wawe huru na taifa liwe na uwezo wa kuichumi wa kujitegemea, wawe economically libarated!. Huwezi kudai uko huru huku ni masikini wa kutupwa na huku rasilimali za nchi yako zina nyonwa na kufyonzwa na mapepari na mabeberu.


Nchi zinataka uhuru
Mataifa yanataka ukombozi
Watu wanataka uhuru na mapinduzi ya kiuchumi!.


Prof. Shivji amezungumzia haki, nimemkosa, sasa anazungumzia usawa "equality before law", watu wote ni sawa, tajiri, masikini, mwanamke mwanaume, mkubwa mdogo, walala heri na walala hoi wote wako sawa mbele ya sheria.


Anatoa hadithi ya kesi ya Martha Wejja, usawa huo unategemea, dira ndio ilitakiwa iamue kuhusu hii misingi

Katiba bora ni ile katiba ambayo chimbuko lake litatoka chini kwa wananchi kwenda juu kwa watawala, katiba hii tuyoitengeneza sasa, misingi yake imetoka juu kwa watawala na kuletwa chini kwa wananchi!.

Amesisitiza dira inatengezwa kwa mjadala wa kitaifa, ili dira hiyo iwe imetokana na wananchi watu muhimu kabisa wa kwanza ni wananchi na sio viongozi. Kabla ya kuandaa katiba kwanza ni lazima watu waulizwe wanataka kujenga taifa la namna gani, baada ya kujua tunataka nini, ndipo tunaunda tume, kuandaa katiba ya kuitekeza dhima ya hiyo dira!.


Prof. Shivji anasema amemuuliza M/Kiti wa Tume ua Katiba, Jaji Warioba, hayo maoni tunayoyakusanya, ni maoni ya kutengeneza katiba ya kutekeleza nini?, Jaji Warioba hana jibu!, hivyo tunatengeneza katiba mpya kwa kufuata dira, dhima na misingi ya katiba ya zamani kwa sababu Tanzania kama taifa, hatujawahi kukaa chini na kujitafakari, tunataka nini!.

No wonder kuna kiongozi aliulizwa "chanzo cha umasikini wa Tanzania ni nini", akasema "hajui kwa nini Tanzania ni masikini!.

Katiba yetu hii iliyopo ina contradiction na dhima yetu kama taifa. Katiba bado inasema Tanzania ni nchi ya wakulima na wafanyakazi inayofuata misingi ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, huku in reality, Tanzania ya leo sio tena ni nchi ya wakulima na wafanyakazi, bali sasa ni nchi ya wenye nacho na wasio nacho, na tunafuata misingi ya upapari na soko huria!.

UP DATE
Sehemu ya tatu ya mada ya Prof. Shiji na Mchakato wa Katiba Mpya kinaendelea ITV saa hizi na kitakuwepo TBC-1 saa 1:30. Leo Prof. Shivji anajibu maswali ya washiriki.
Karibuni tuendelee.
Prof. Shivji ameanza na ukosoaji wa Tume ya Katiba, akasema Tume za katiba ziko supposed to be a "professional body" ilihitaji watu professionals wa fani mbalimbali, hazikuhitaji uwakilishi, kwenye kukusanya maoni, uwakilishi wa nini?. Amesema, uwakilishi, anahitajika kwenye Bunge la Katiba. Pia ameuliza kwa nchi masikini kama Tanzania, wajumbe 30 wa tume ya kukusanya maoni, "wote hao wa nini?!.

Prof. Shivji pia amekosoa Bunge la Katiba litakaloitishwa, amesema sheria iliyopo inawataja wabunge wote bunge la JMT, na wajumbe wote wa BLW automatically wanakuwa ni wajumbe wa bunge la katiba, akasema "wabunge hawa ni wawakilishi wa wananchi kwa mujibu wa katiba iliyopo, sasa nani kawatuma wajumbe hawa kuwa wawakilishi wa wananchi katika Bunge la Katiba?!. Wabunge wote na wawakilishi wote wamechaguliwa kutoka vyama vya siasa. Jee Watanzania wasio wanachama wa chama chochote cha siasa, watawakilishwa na nani?!,

Prof. Shivji amesema Bunge la Katiba ni bunge maalum kwa kazi maalum!, Wabunge wa bunge la sasa, hawakupaswa kuwa wajumbe wa bunge la katiba automatically.


Kwa msiojua, katika uundaji wa katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, wabunge wa Bunge la JM ya Tanzania tuu ndio walijitransform na kujigeuza wajumbe wa Constituent assembly, na Bunge la JMT likajiugeuza kuwa Bunge la Katiba, likaipitisha katiba ile within 45 minutes!.

Ali katiba ipate uhalali kikatiba, katiba hiyo inabidi ipitishwe na akidi ya theluthi mbili za wajumbe, hivyo akatoa angalizo, kuwa kitendo cha kuwatumia wabunge wote na wawakilishi wote, ukujumlisha idadi ya wabunge wote na wajumbe wote wa BLW katika ujumla wao, wabunge wa chama kimoja peke yao, tayari wanafikia theluthi mbili za kupitisha katiba mpya!, hivyo katiba yoyote itakayopendekezwa, hata iwe mbovu vipi, ni lazima tuu itapita tuu!.

Prof. Shivji amesema this is a good chance kwa Watanzania kupata katiba bora, ila tusiharakishe, bora tuchelewe mchakato lakini tupate katiba bora yenye uhalali wa kikatiba na uhalali wa kisheria.
We not only need a good constitution, but a constitution which has the constitutionality of a good constitution!-Prof. Shivji.
Pasco
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,556
2,000
Shivji anasema msingi mkuu wa katiba ni "dira", huwezi kuingia kwenye mchakato wa katiba mpya bila dira. Mchakato wa kukusanya maoni ulitakiwa utanguliwe na "mjadala wa kitaifa kuweke dira", ndipo sasa tutengeneza katiba inayoendana na hiyo dira!.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,556
2,000
Amesema, pamoja na mchakato kuanza bila dira rasmi, lakini wajumbe wa kamati hiyo wana mitazamo, hivyo japo hatuna dira, lakini pia tunaweza kupata katiba nzuri!.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,556
2,000
Ameitaja misingi mikuu minne ya katiba nzuri, ikianzia na uhuru, haki, usawa, udugu na ujamaa.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,556
2,000
Uhuru: Huu ni uhuru wa mtu binafsi, lengo zima la uhuru limejengwa kwenye misingi ya haki za binaadamu, maada ya dhana ya uhuru, pia ni uhuru wa nchi, uhuru wa taifa, uhuru wa jamii!. Kama nchi haiko huru, then watu wake hawawezi kuwa huru!. Japo taifa limepata uhuru wa nchi, yaa independence, lakini taifa hilo likawa halijajikomboa "libarated", huwezi kujidai eti una uhuru!. Zaidi ya nchi kupata uhuru, ili mchi iwe na uhuru wa kweli lazima wawe libarated!. Huwezi kudai uko huru huku unanyonywa na mapepari.

Nchi zinataka uhuru
Mataifa yanataka ukombozi
Watu wanataka mapinduzi!.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,556
2,000
Amnezungumzia haki, nimemkosa, sasa anazungumzia usawa "equality before law", watu wote ni sawa, tajiri, masikini, mwanamke mwanaume, mkubwa mdogo, walala heri na walala hoi wote wako sawa mbele ya sheria.

Anatoa hadithi ya kesi ya Martha Wejja, uswa huo unategemea, dira ndio ilitakiwa iamue kuhusu hii misingi

Katiba bora ni ile katiba ambayo chimbuko lake litatoka chini kwa wananchi kwenda juu kwa watawala, katiba hii tuyaitengeneza sasa, misingi imetoka juu kwa watawala na kuletwa chini kwa wananchi!.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,556
2,000
Kipindi kimemalizika kwa ITV, kitaendelea kesho saa 1:00 usiku. Kwa wale wenye access na TBC, kipindi kitaanza saa !:30. Kwa TBC, kipindi kitakuwa kila siku saa 1:30 usiku.
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,254
2,000
Ndio sababu hawakumuweka kwenye tume ya katiba maana angemkosoa live hata Warioba na ToR alizopewa azishikilie!!kile kichwa ni balaa!!!
 
Dec 11, 2010
3,321
0
Kipindi kimemalizika kwa ITV, kitaendelea kesho saa 1:00 usiku. Kwa wale wenye access na TBC, kipindi kitaanza saa !:30. Kwa TBC, kipindi kitakuwa kila siku saa 1:30 usiku.

Mkuu Pasco.
Samahani naomba uhakiki upya muda wa kipindi hicho maana kwa muda huu wa saa moja na nusu kuna kipindi pekee ambacho huwa nakiangalia tbc1 (ze comedy) kwa ITV nako nimeangalia punde nimekuta ni Isidingo. Samahani naomba muongozo.
 
Last edited by a moderator:

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,556
2,000
Kasema angependa taifa liwe na dira gani kwa sasa?
Amesisitiza dira inatengezwa kwa mjadala wa kitaifa, ili dira hiyo iwe imetokana na wananchi. Kabla ya kuandaa katiba kwanza ni lazima watu waulizwe wanataka kujenga taifa la namna gani, baada ya kujua tunataka nini, ndipo tunaunda tume, kuandaa katiba ya kuitekeza hiyo dira!.

Amesema amemuuliza M/Kiti wa Tume, hayo maoni tunayoyakusanya, ni maoni ya kutengeneza katiba ya kutekeleza nini?, Warioba hana jibu, hivyo tunatengeneza katiba mpya kwa kufuata dira na misingi ya katiba ya zamani kwa sababu Tanzania kama taifa, hatujawahi kukaa chini na kujitafakari, tunataka nini?.

No wonder kuna kiongozi aliulizwa "chanzo cha umasikini wa Tanzania ni nini", akasema "hajui kwa nini Tanzania ni masikini!.

Katiba yetu bado inasema Tanzania ni nchi ya wakulima na wafanyakazi inayofuata misingi ya siasa ya ujamaa na kujitegemea, huku in reality, Tanzania ya leo sio ya wakulima na wafanyakazi na tunafuata misingi ya upapari na soko huria!.
P.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,556
2,000
Mkuu Pasco.
Samahani naomba uhakiki upya muda wa kipindi hicho maana kwa muda huu wa saa moja na nusu kuna kipindi pekee ambacho huwa nakiangalia tbc1 (ze comedy) kwa ITV nako nimeangalia punde nimekuta ni Isidingo. Samahani naomba muongozo.
Mohamed Mtoi, ITV ni saa 1:00-1:30, TBC ilikuwa iwe Saa 1:30 mpaka 2:00 every day isipokuwa Alhamisi, sorry. Kesho anzia ITV Saa 1 na TBC saa 1:30.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom