Poor Prof ni miongoni mwa wasafi walio litumikia Taifa utumishi uliotukuka
JF,
Na hata Sarungi tena!!!!!
Sasa ni yupi msafi?
hodihodi jamani, twaingia! nimejisomea ripoti na maoni yaliyotolewa naona hapa jamboforums wengi wazushi. kama nikisoma vizuri habari hii ya thisday imejaribu kumhusisha professor na tangold na imeshindikana. hii haikuwa dili lake wala hakuhusika, hebu chekini vizuri alichosema: alikuwa anafuata maagizo ya serikali! sasa mwulizeni nani alikuagiza? ndipo mtapata jibu.
wengine hapa wanaleta umbea eti yule mzee alikuwa anapokea vibahasha airport, hii ni vichekesho! yaani mtumzima kama yule aende airport kila wiki akijua eti hamtamwona? huu ni utoto mlioandika... mweee ngonga hata mimi ni mwenyeji kiasi hapo airport lakini hii sijawahi kuona ulichosema, unaleta uzushi tu. profesor anapita VIP anapokuja airport na hatoki nje alikuwa anatuma wahudumu na hajawahi kupita njia ya kawaida. kama ni mfanyakazi wa airport unajua hata kule duty free shops alikuwa hafiki. acha umbea, mtoto wa kiume! Kama vibahasha siangepokea nyumbani? jamani wengine mnaandika bila kufikiria. alafu wengine mnadandia mkidhani hiyo ndiyo proof ya kuwa si msafi. tukikaa sisi vikao akina mama mnasema ni umbea mkija kwenye vichati vya intaneti mnasema eti mnajadili, ni umbea tu!
huyu mzee mnatafuta kumchafua lakini yatawashinda. mlianza na masuala ya rorya mkaja hapa.. mtafuteni mchawi mwingine maana kama ni tangold, tuna data wengine lakini hatuzimwagi hapa tunasubiri waandishi wazifanyie kazi kwanza. lakini wenye shida na hizi data wanitumie meseji... kama ni umbea na kuchafuliana majina endeleni tuje kuwaumbua!
ngoja niangalie kama kuna umbea mwingine thread nyingine.
He explained that during his two-year spell as defence minister, he never went against government decisions nor ever received any monetary gain from the mine. The ex-minister said he retired from government a poor man, with an outstanding 8m/- debt for the purchase of a government house in Dar es Salaam.
I am being turned into a scapegoat? I was merely implementing government decisions, he said, adding: I am not corrupt?I am a clean man who has always been diligently executing decisions made by the government.
Haya ni maneno yaliyotoka kwenye mdomo wa PROFESA.... ETI yeye ni Bangusilo!
Gus,
This is not personal...ila napenda kujua ni kwa nini unatumia nguvu zako zote, akili zako zote na hata kudiriki kuita watu wambea.... cammon u can do better than that Gus!
Ebu fikiria kama mtu anaweza kutekeleza maamuzi ya serikali bila kuhoji hata kidogo au na yeye analeta zile za Zakhia Meghji za ugeni kwenye wizara???
Yela mashimo, kuhamshwa kwa Kambi ya jeshi Buhemba kwenda Ikoma ili kuupisha mgodi unafikiri ni maamuzi ya kizalendo au kifisadi?? Na je unaelewa kwamba ile kambi iliwekwa kwenye ile Gold reserve makusudi na J. K. Nyerere(RIP) ili kusubiria waTz wawe na uwezo wa kuchimba na kutumia Gold reserve zetu beneficially?
Mi napenda kama una hoja uilete kama hoja sio kwa kebehi.
Sina mengi...
Mzee huyu hela anaijua.....Imechukua muda watu kumshtukia
sasa mnataka kuleta ligi? haya leteni, lakini mjue mi niliingia kwenye huu mjadala najua labda mna data za maana, na niliingia kwa moyo mweupe nikijua kwamba naweza kuongeza na mi data zangu lakini mmebaki kuongea majungu.
kaka lunyungu, nakuona ni mtu mzima sitaki kukuvunjia heshima kwa niyo narudia, majungu tuweke pembeni tuendelee na kile kilichotuleta hapa, ambayo ni suala la meremeta. na hii ni ishu kubwa inayohusu mustakabali wa taifa na si suala la kukisia. ilikuweza kuweka ukweli hadharani inahitaji wote tuwe jasiri maana si ishu ndogo, lakini mtakapochanganya na majungu hata sisi tukiweka hapa data za kuaminika tutaonekana tunaleta majungu na fitna. naomba tuwe imara katika kuhakikisha data zote zinakaa vizuri na zinaamnika.
dmussa, kaka nimekuelewa, na kumradhi kama nimekuwa mkali kwako. wewe unatafuta data au siyo?
kinachogomba hapa ni umbea na fitna na kukosekana kwa dira.
turudi kwenye meremeta na tangold. naomba mjibu maswali haya, na kama mmekosa jibu mkiri kwamba huko mlikokuwa mnaenda siyo, alafu tuwekane sawa;
- meremeta iliundwa lini na nani? wizara? mtu?
- iliundwa kwa lengo gani?
- kampuni ya afrika kusini ilikuwa inapewa majukumu gani?
- kwa nini serikali ya tanzania iliingia ubia na kampuni hii na imeonekana kuwa imebarikiwa na wahusika wote? kumbukeni mradi huu si wa mwaka mmoja tu na haikuanza leo bali tokea zamani.
- kwa nini ubia ulisitishwa?
- pesa za meremeta ziko wapi? hiyo kampuni ya afrika kusini imetokomea wapi?
kwanza naomba majibu alafu tuendelee ili nione kama hapa jamboforums kuna wasomi au la. hoja hujibiwa kwa hoja na si kwa umbea au siyo?