Prof. Safari: Kwenye usafiri wa umma, wazungu husoma vitabu na magazeti, watanzania wanatafuna mahindi ya kuchoma na mayai ya kuchemsha

sababu ya uwepo wa uislamu tanzagiza ndiyo maana labda hali iko hivyo, wazungu ni Christian au wana chimbuko la ukristo atleast …
Iran na Turkiye na Malaysia na Indonesia ni nchi za kiislam ila zina wasomi wakubwa duniani.
Point yako ya kipumbavu,usiingize udini haufai.
 
Issue si kununua, kusoma.

Unafanya nini ukiwa kwenye usafiri wa umma?

Kwa kuwa issue ni kusoma, unaweza kutembea na kitabu hard copy au soft copy ili kila upatapo nafasi usome badala ya kupiga soga.
Hukuwa na ulazima wa kunijibu kwa sababu hujanielewa
 
Hizo basi za Umma zenye convenience ya kusoma au hata mtu kupata fikra za kusomea kwenye hilo basi zinatoka wapi..., kabla haujafungua kurasa unaambiwa sogea tukae....

Kama ni suala la safari ndefu kitabu ni lazima...., mara nyingine mtu hauchukui kitabu ili usome bali jirani yako asikupigishe story zisizo na mwisho hivyo unajifanya busy kwenye usomaji... Pia usisahau hata chakula ni utalii sasa kama upo kwenye basi masaa ya kutosha alafu unafika Dodoma kwenye Zabibu utakuwa haulitendei haki tumbo lako kupata kitu from the Source..., Au kwa waliopanda treni Kuku wa Salanda....
 
Kichwa cha habari kizuri ila tu umeharibu ulipo anza kukichambua, sasa mambo ya meya yanatoka wapi ktk headline yako. Acha ufisiemu kwanza ndio urudi kukielezea alichosema professor.
 
Huyu Prof kwakuwa wazungu mabasi yao yanasimama kwenye take away basi zile burger, hot dogs na can za cocacola siyo vyakula?

Labda wazungu wamestaarabika hawana fujo kama za Wasukuma wa Maswa wakiwa watatu kwenye bus utatamani ushuke au unaweza kusamehe nauli yako, halafu hawakai pamoja, mmoja mbele, mmoja katika na mwingine siti ya nyuma halafu wanataka wapige story zao kwa kilugha. Shubaamiti.
Mzungu anaustaarabu mzuri sana, mkiwa mnasubiria usafiri wa umma mnapanga foleni na anaingia mmojammoja haijalishi babu kijana au mtoto, ukikuta mtoto amekaa hata kama umemzidi umri subiri gari lingine.. hapo kariakoo kama unakuja tegeta siku moja bado kidogo nikanyagwe skio na mtu aliyeingilia dirishani kwenye usafiri huo wa umma..
 
Nimefuatilia interview ya Prof. Safari aliyofanya majuzi, pamoja na mengine, nimeondoka na nukuu hiyo kwamba watanzania hawana utamaduni wa kusoma, kwe ye usafiri wa umma wanashindana kula.

Hii ni kweli kabisa, ni kama tuna mzimu wenye njaa ya kula, basi likisimama ni mbio madirishani au hotelini kufakamia menu, baada ya hapo matumbo ndiii kama Meya wa stendi ya zamani kabla ya ile ya JPM.

Upande basi moja na waha au wasukuma, wanatembea na stoku ya viazi na karanga walivyochemsha jana, au ugali na dagaa.
Huo usafiri haukuruhusu hata kusoma kwa mbanano huo
 
Profesa Safari anajua hiace za Moshi mjini - Machame? Pale mbele wanapotakiwa kukaa abiria na dereva huwa wanakaa abiria watatu na dereva. Hilo gazeti unasomaje? Au coaster za Arusha - Moshi ambapo lazima majibizano kati ya abiria na kondakfa kuhusu nauli yatokee huku dereva naye akiingilia kati. Utakuta hapo ndo mko kwenye kona kali daraja la mto Kikavu ila dereva anatazama nyuma kupambana na abiria kuhusu nauli.
 
Nimefuatilia interview ya Prof. Safari aliyofanya majuzi, pamoja na mengine, nimeondoka na nukuu hiyo kwamba watanzania hawana utamaduni wa kusoma, kwe ye usafiri wa umma wanashindana kula.

Hii ni kweli kabisa, ni kama tuna mzimu wenye njaa ya kula, basi likisimama ni mbio madirishani au hotelini kufakamia menu, baada ya hapo matumbo ndiii kama Meya wa stendi ya zamani kabla ya ile ya JPM.

Upande basi moja na waha au wasukuma, wanatembea na stoku ya viazi na karanga walivyochemsha jana, au ugali na dagaa.
.......Wajapani wanalala
 
Prof siku atest apande na mavitabu yake ataona mziki
Mule ndani 😄

Ova
 
Iran na Turkiye na Malaysia na Indonesia ni nchi za kiislam ila zina wasomi wakubwa duniani.
Point yako ya kipumbavu,usiingize udini haufai.

mbona hakuzitolea mfano hizo nchi za kiislamu huyo profesa? isitoshe kwani udini una shida gani?
 
Back
Top Bottom