Prof. Safari: Kuna haja ya kufungua kesi kuhoji uhalali wa Wabunge 19 wa Viti Maalum CHADEMA

Watz tuna roho za kwa nini sana kisa wao wamekosa ubunge ndo wanamua wote wakose dah,

Wanasiasa ndo ajira zao ubunge wacheni watumikie ajira
 
Shida yote ya nini?

Kama ni uanachama tayari wamewavua.

Na kama nafasi za ubunge Chadema haizitaki Sasa mapambano hayo ya kila siku kwa ajili ya nn?
nadhani Chadema hawataki chama kitumike katika uhalali wao; yaani wasijiite wabunge viti maalumu kutoka chadema
 
CDM tabu yote hii ya nini?? Maamuzi yenu ni kwamba mmeshawavua uanachama, kwanini mnateseka ?
Wananchi wameshawashitukia kwa taarifa yenu
Ni heri mkubali tu mapema raia waanze kuzoea kulikoni mje mkubali mwishoni na vidonda havitapona (muwaruhusu hao covid19 sababu mlikubaliana wenyewe,msicheze na akili zetu)
Akili zenu nyie CCM zitoke wapi CHADEMA wachezee hamna kitu vichwani mwenu. Wabunge wa Viti Maalum hawana majimbo kwa hiyo wanawakilisha Vyama na wanachama wao. Vile Viti 19 ni vya CHADEMA na hao Covid-19 siyo wanachama tena wamefukuzwa kwa hiyo Viti ni wazi na wakuvijaza ni CHADEMA na wakujaza wako wengi tu kwenye Chama. Viti haviwezi kujazwa na CCM na wajinga hao walijua hilo ndo maana walitumia mbinu chafu bila kufuata taratibu wakawaapisha gereji wanachama wa CHADEMA wengine wakitolewa mahabusu usiku wa manane wengine wakiwa Mahakamani kwa kesi za kubambikiziwa. Hivi sasa Viti vyote 19 viko wazi na visipojazwa na CHADEMA vitabaki wazi mpaka Uchaguzi ujao kwa hiyo Prof. Safari anasema kweli kuwa tafsiri ya mahakama inahitajika kusafisha bali ya hewa ili Viti vipate Wabunge halali.
 
Tatzo cdm wanaamini sana katika lugha chafu na zenye kuashiria ugomvi pasipo kufikiri kwa kina nakujua nini unajibu. Any way kwataarifa yako mdee hawezi kufukuzwa kama wengi wanyonge mnavyodhani,hapo wana cheza na akili yenu kwa mbinu eti "wakate rufaa". Kama huelewi subiri maamuzi ya rufaa.
Mwezi wa pili usishangae kuwaona covid19 bungeni😂😂😂😂
Akili zenu nyie CCM zitoke wapi CHADEMA wacheze hamna kitu kichwani. Wabunge wa Viti Maalum hawana majimbo kwa hiyo wanawakilisha Vyama na wanachama wao. Vile Viti 19 ni vya CHADEMA na hao Covid-19 siyo wanachama tena wamefukuzwa kwa hiyo Viti ni wazi na wakuvijaza ni CHADEMA na qakujaza wako wengi tu. Viti haviwezi kujazwa na CCM na wajinga hao wanajua hilo ndo maana walitumia mbinu chafu bila kufuata taratibu ya wakawaapisha gereji wanachama wa CHADEMA wengine wakitolewa mahabusu usiku. Hivi sasa Viti viko wazi na visipojazwa na CHADEMA vitabaki wazi mpaka Uchaguzi ujao kwa hiyo Prof. Safari anasema kweli kuwa tafsiri ya mahakama inahitajika kusafisha bali ya hewa ili Viti vipate Wabunge halali.
 
Profesa Safari, aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa Chadema kuanzia 2014 hadi 2019, alisema kuna haja ya kufungua kesi kupata tafsiri kama Mdee na wenzake bado ni wabunge halali baada ya Kamati Kuu ya Chadema kuwavua uanachama.

“Mahakama ndiyo ina haki ya kutafsiri,” alisema.
Unaona hawa watu wanavyotumika kuendelea kukihujumu CHADEMA?

Sasa huyu katumwa kufanya kazi maalum. Kuwashawishi CHADEMA huku akijua mahakama hiyo itakataa kwamba hao wanachama hawakufukuzwa!
Maajabu ya nchi sasa ndiyo haya. Profesa anatafuta kuhalalisha ubunge wa akina Halima Mdee kupitia mahakamani.

Maana yake ni kwamba CHADEMA hawana uwezo wa kuwafukuza wanachama wao hawa bila mahakama kuhalalisha!
 
Nampongeza Safari kwa uadilifu wake, ingawa hakuna mahakama ya kushindana na mhimili wa serikali au bunge now.Ni kupoteza muda tu
Kama ni mwadilifu kama unavyodhani, basi ujue hapa anatumika kuhujumu chama alichowahi kuwa mwanachama wake.

Ushauri anaotoa hapa hauonyeshi uadilifu wowote. Huyu anatumika tu sasa kuendelea kukihujumu CHADEMA. Ni ushauri wa kipuuzi sana aliotoa.
 
CDM tabu yote hii ya nini?? Maamuzi yenu ni kwamba mmeshawavua uanachama, kwanini mnateseka ?
Wananchi wameshawashitukia kwa taarifa yenu
Ni heri mkubali tu mapema raia waanze kuzoea kulikoni mje mkubali mwishoni na vidonda havitapona (muwaruhusu hao covid19 sababu mlikubaliana wenyewe,msicheze na akili zetu)
Mkuu unadhani ni sahihi kwa asiye Mwanachama was CHADEMA kuendelea kubaki Bungeni Kwa kofia ya Chama ambacho hakimtambui?

Kama shida ni Ubunge si wawape tu huo Ubunge Kwa namna zao wao na siyo kulazimisha kutumia jina la CHADEMA?
 
hapana mkuu, lakini wakikata rufaa watarejeshewa uanachama wao as it was at first.so wataendelea kuwa wabunge kwa mwavuli wa cdm,believe or not but truthy will remain truthy🤔🤔
 
Shida yote ya nini?

Kama ni uanachama tayari wamewavua.

Na kama nafasi za ubunge Chadema haizitaki Sasa mapambano hayo ya kila siku kwa ajili ya nn?
... kuna shida! Umeshavuliwa uanachama halafu unajitambulisha kwa jina la chama kilichokuvua uanachama; sio sahihi. Chadema hawana shida na ubunge wao; kisichotakiwa ni wao kujitambulisha kama wanachama wa Chadema. Membe alivuliwa uanachama wa CCM na ukakoma muda ule ule; vivyo hivyo kwa Sofia Simba, na wengine wengi!
 
Kama ni mwadilifu kama unavyodhani, basi ujue hapa anatumika kuhujumu chama alichowahi kuwa mwanachama wake.

Ushauri anaotoa hapa hauonyeshi uadilifu wowote. Huyu anatumika tu sasa kuendelea kukihujumu CHADEMA. Ni ushauri wa kipuuzi sana aliotoa.
"...chama alichowahi kuwa Mwanachama wake".

Kwani amekihama?!!
 
Mkuu unadhani ni sahihi kwa asiye Mwanachama was CHADEMA kuendelea kubaki Bungeni Kwa kofia ya Chama ambacho hakimtambui?

Kama shida ni Ubunge si wawape tu huo Ubunge Kwa namna zao wao na siyo kulazimisha kutumia jina la CHADEMA?
... exactly; kinachogomba ni kung'ang'ania ubunge kwa chama ambacho sio wanachama tena. Kama vipi wawape ubunge kwa utaratibu mwingine na sio kuilazimishia Chadema. Waende CCM wakapewe hivyo viti maalumu kutokea huko; very simple.
 
Wale siyo wanachama wa CHADEMA mpaka sasa hivyo hakuna sababu ya kupoteza muda kwenda mahakamani
.... kuna umuhimu huo; kuiomba mahakama iwazuie kujitambulisha kwa namna yoyote na Chadema. Huo ubunge hauna issue, waendelee nao ila marufuku kujiita wanachama wa Chadema.
 
"...chama alichowahi kuwa Mwanachama wake".

Kwani amekihama?!!
Nilidhani hivyo. Wewe unajua bado ni mwanachama wa chama hicho?
Hata kama "hakukihama" na kujiunga na chama kingine, nilidhani alishakoma kuwa mwanachama wa CHADEMA.
 
Nilidhani hivyo. Wewe unajua bado ni mwanachama wa chama hicho?
Hata kama "hakukihama" na kujiunga na chama kingine, nilidhani alishakoma kuwa mwanachama wa CHADEMA.
....kumbe kwenu CHADEMA mtu akiwa si kiongozi Tena anakuwa amekihama eee?!!

Huyo bado ni CHADEMA kindakindaki....

Mtu huna taarifa sahihi halafu unaanza kubwabwaja kuwa wakili "anatumiwa"...
Hakika mko na ILLUSION Sana....
 
Hapa unaonyesha upumbavu wako. Umeniona nikiwa CHADEMA?
Nilikujibu nikidhani kichwani zimo kumbe ni mmoja wa walewale wanaoshinda hapa JF ili mradi waende chooni?

Usitafute kuendelea kujibizana na mimi, huwa sina muda na wapuuzi wa aina yenu.
 
Back
Top Bottom