Prof. Safari: Kuna haja ya kufungua kesi kuhoji uhalali wa Wabunge 19 wa Viti Maalum CHADEMA

... sio suala la wao kuongelea lolote kuhusu Chadema bali kutambulishwa kama wanachama wa Chadema. Kumbuka kwenye ile press yao baada ya kuvuliwa uanachama walijitambulisha wakiwa na mavazi rasmi ya Chadema; mmeshavuliwa uanachama attire za Chadema za nini tena?
Sasa na nyie ubunge si hamuutaki basi waacheni tu

Au kwa vile act wameenda basi na nyie Mnaanza kuhangaika
 
Nauliza aliye toa kibali cha wao kumpa Supika yule ninani?

Jee ndiyo njia shihii ya kutumika
Jee kikao cha kupendekeza majina kilikuwa halali?
 
Wakili wa kujitegemea, Profesa Abdallah Safari ameishauri CHADEMA kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya uhalali wa ubunge wa makada 19 wa chama hicho walioadhibiwa baada ya kwenda kuapa kuwa wabunge wa viti maalum na kutotokea mbele ya Kamati Kuu kujieleza.

Wanachama hao, ambao ni pamoja na mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Bawacha), Halima Mdee waliapishwa Novemba 24 wakati kukiwa na utata wa barua iliyopelekwa Tume ya Uchaguzi (NEC) kuhusu uteuzi wa wabunge wa viti maalum, baada ya katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika kusema hakuiandika wala Kamati Kuu haikukutana kupitisha orodha.

Kitendo hicho kiliifanya Chadema iwate mbele ya Kamati Kuu kujielezas, lakini wote hawakutokea na hivyo chombo hicho kufikia hatua ya kuwavua uanachama, lakini Spika Job Ndugai alisema hatatambua uamuzi huo aliodai wa kuonea wanawake baada ya kuhukumiwa bila ya kusikilizwa.

Nafasi za viti maalum ni za vyama ambavyo hupata zaidi ya asilimia tano ya kura za wabunge, tofauti na za ubunge wa jimbo ambazo hupatikana kutokana na vyama humdhamini mgombea.

“Kama wataenda bungeni, njia pekee ni kuomba tafsiri ya mahakama ili chombo hiki kiseme katika mazingira haya ibara ya 71 (1) f hawa ni wanachama halali,” alisema Profesa Safari, ambaye amebobea katika sheria.

Ibara hiyo ya katiba inasema mtu atapoteza ubunge iwapo “ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge”.

Profesa Safari, aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa Chadema kuanzia 2014 hadi 2019, alisema kuna haja ya kufungua kesi kupata tafsiri kama Mdee na wenzake bado ni wabunge halali baada ya Kamati Kuu ya Chadema kuwavua uanachama.

“Mahakama ndiyo ina haki ya kutafsiri,” alisema.

Profesa Safari alisema suala la Mdee na wenzake kufukuzwa Chadema lipo wazi kwa mujibu wa ibara ya 71 (1) (f) ya Katiba ya jamhuri ya Muungano inayoeleza kuhusu mbunge kufukuzwa uanachama na pia sifa za kugombea zinazoelezwa katika ibara 67 (1)b, inayotaka mgombea ubunge apendekezwe na chama chake.

“Dhana ya kuwa na chama ni muhimu. Ukishatimuliwa huwezi ukakingikiwa kifua na mtu yeyote. Bahati nzuri matukio yametokea mara nyingi sana. Wakati wa Tanu walifukuzwa kina Anangisye, halafu wabunge wa CUF walitimuliwa. Mara nyingi tu (haya yanatokea),” alisema Safari.

Pia alielezwa kushangazwa na kitendo cha Spika kuwatetea makada hao akihoji wameanza urafiki lini.
Ni ushahuri mzuri, lakini kama CDM watataka kwenda mahakamani basi wakuwashtaki ni Halima na kundi lake kwa kutumia jina la chama hali ya kuwa si wanachama. Na Halima alilikiri hilo wakati alipo ulizwa maswali, aliweka wazi kwamba yeye na kundi lake (waliofukuzwa) ni wanachama wa hiyari na wako katika mchakato wa kukata rufaa.
Kulishtaki bunge ama spika wa bunge nikupoteza muda, kwa sababu hivyo vifungu vya katiba viko wazi sana havihitaji tafsiri ya mahakama. Kinacho endelea hapa ni utawala wa kimabavu badala ya uongozi chini ya katiba na sheria.
Kwa kumalizia tu niseme kwamba kesi hii si ya CDM tena, bali ni ya kila mtanzania kwa sababu katiba inayokanyagwa hapa si katiba ya CDM bali ni katiba ya JMT.
CDM walishafanya maamuzi kwa mujibu wa katiba yao.
JMT nayo ifanye maamuzi kwa mujibu wa katiba.

Lakini je ni nani wa kumfunga paka kengele?
 
Back
Top Bottom