Prof. Mukandala: Meli ya MV Bukoba ilifanya kazi Tanzania kwa miaka 17 bila kusajiliwa na haikupaswa kuletwa nchini

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,517
8,451
Aliyewahi kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Rwekaza Mukandala amezitaja sababu mbalimbali zilizosababisha kuzama kwa meli ya Mv Bukoba kwa kurejea maandiko, hotuba, tafiti, hukumu za kesi zilizohusu sakata hilo.

Profesa Mukandala ameyasema hayo leo Jumanne Mei 21, 2024 akitoa muhadhara wa kiprofesa UDSM ikiwa ni miaka 28 tangu meli hiyo izame jijini Mwanza. Katika maelezo yake, amesema meli hiyo ilifanya kazi miaka 17 nchini pasina kusajiliwa na wala haikupaswa kuletwa nchini.

Profesa Mukandala anatoa muhadhara wa kiprofesa kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma ikiwa ni baada ya miaka 45 tangu muhadhara wa mwisho wenye hadhi hiyo ufanyike.

MWANANCHI

Poa Soma Mhadhara wa Uprofesa: Machungu ya MV Bukoba, Dola na soko
 
Mtu mweusi hatenganishwi na makando-Kandi. Mnashida gani lakini?
IMG_5624.jpeg
 
Maprofesa wachumia tumbo kama Mukandala na wenzake ambao wakipewa vijisent na ccm tu wanapindisha tafiti watakavyo hawawezi kuaminika nje ya fence ya udsm.

Elimu ya kimangharibi haijaisaidia Afrika wala kuwafanya wasomi wetu kuwa na tija kwa jamii.

Hawa Maprofesa sampuli ya Mkandala, Kabudi na wenzake wana faida kwa matumbo yao, familia zao na ccm tu.

Hatujamsahau Mkandala wa REDET na yule wa juzi wa kurekebisha sheria za uchaguzi.

Hawa ni useless profesa
 
Una dharau sana.

Ushindwe.

Mwafrika ni kila kitu.

Hatahivyo hayo makando kando si tumejifunza kutoka kwa Wazungu? Najua utabisha lakini zingatia tokea ukoloni na njia zao za kutubadilisha tufanane na wao. Sasa tumekuwa hivyo, ni shida nayo!🤔😭😭😭😭😭

Just like always;Muzungu pipo!🙌🏾
 
Una dharau sana.

Ushindwe.

Mwafrika ni kila kitu.

Hatahivyo hayo makando kando si tumejifunza kutoka kwa Wazungu? Najua utabisha lakini zingatia tokea ukoloni na njia zao za kutubadilisha tufanane na wao. Sasa tumekuwa hivyo, ni shida nayo!🤔😭😭😭😭😭

Just like always;Muzungu pipo!🙌🏾
Unajua historia ya ukoloni wewe? Au historia ya uzwazwa wa mwafrika umeanza kipindi cha ukoloni? Si mlibadilisha watumwa kwa nguo? Chumvi? Kioo? nk.

Punguzeni makando-kando

Mnaumiza watu wengi.
 
Unajua historia ya ukoloni wewe?
Wewe yako ni ipi
Au historia ya uzwazwa wa mwafrika umeanza kipindi cha ukoloni?
Uzwazwa ndio nini? Wewe unawajua Neanderthrals? Sisi waafrika-Tena bila ya kumumunya Homo Sapiens wametoka hapa kwetu bongo. Tanzania- Wakiwa na Akili kuliko hao Neanderthrals. Take note.
Si mlibadilisha watumwa kwa nguo? Chumvi? Kioo? nk.
Chini ya mtutu wa Bunduki. Unaijua Maxim gun wewe?
Punguzeni makando-kando
Ndio nimesema, tumejifunza kutoka kwa Wazungu. Na hilo unabisha?
Mnaumiza watu wengi.
Kabla ya Wazungu tulikuwa hatupigani risasi, wakaje na maxim gun na magobole, hizo ndizo tulibadilishana nao. Ukumbuke wakati wazungu wanakuja walitukuta na sisi Waafrika tulkuwa na vita vita kama zile za Ulaya na Asia.

Hivyobasi ilikuwa ni win win situation. Wanaondoka na Chumvi, tunabakiwa na Silaha.

Sasa hasira za nini? Hivi hujui Wazungu waliwaumiza Waafrika. Ama na hilo unataka kufunika?
 
Aliyewahi kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Rwekaza Mukandala amezitaja sababu mbalimbali zilizosababisha kuzama kwa meli ya Mv Bukoba kwa kurejea maandiko, hotuba, tafiti, hukumu za kesi zilizohusu sakata hilo.

Profesa Mukandala ameyasema hayo leo Jumanne Mei 21, 2024 akitoa muhadhara wa kiprofesa UDSM ikiwa ni miaka 28 tangu meli hiyo izame jijini Mwanza. Katika maelezo yake, amesema meli hiyo ilifanya kazi miaka 17 nchini pasina kusajiliwa na wala haikupaswa kuletwa nchini.

Profesa Mukandala anatoa muhadhara wa kiprofesa kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma ikiwa ni baada ya miaka 45 tangu muhadhara wa mwisho wenye hadhi hiyo ufanyike.

MWANANCHI

Poa Soma Mhadhara wa Uprofesa: Machungu ya MV Bukoba, Dola na soko

Makubwa haya...mbona hizi tafiti hazikufanyiwa kazi mapema? Halafu nani aliyeleta hiyo meli bila kuisajili? Shida yetu kubwa ni rushwa. Ndio maana hata anayesema hasemi kitu kimenyooka maana inawezekana katika kona na pitapita zake, alisaidiwa kwa mfumo wa aina hiyo hiyo.

Taifa letu sisi sote, tujitafakari. Tuamue tunataka kufika wapi na tuambiane. Ili tusiwe na mtu wa kumlaumu kama mambo yakikataa
 
Huu ndiyo uzwazwa wenu watu weusi. Huku akiwapandishia wananchi kodi, yeye anapanga ziara ya anasa na kudanganya kuwa Marekani imegharamikia ziara hiyo.

Unatumiaje zaidi ya dollar 1,500,000 kukodi private jet kwenda tu Marekani? Bado hoteli na chakula, gharama za Ulinzi, per diem, nk.

Hadi nchi waisani huwa wanatuchangaa. Ila kWa kuwa pesa nyingi wanazotoa ni mikopo, hawana shida.

Mtu mweusi ni hatari sana.
 

Attachments

  • IMG_5625.png
    IMG_5625.png
    1.9 MB · Views: 3
Huu ndiyo uzwazwa wenu watu weusi. Huku akiwapandishia wananchi kodi, yeye anapanga ziara ya anasa na kudanganya kuwa Marekani imegharamikia ziara hiyo.

Unatumiaje zaidi ya dollar 1,500,000 kukodi private jet kwenda tu Marekani? Bado hoteli na chakula, gharama za Ulinzi, per diem, nk.

Hadi nchi waisani huwa wanatuchangaa. Ila kWa kuwa pesa nyingi wanazotoa ni mikopo, hawana shida.

Mtu mweusi ni hatari sana.
Umaskini huku Africa ni wa kutengenezwa na watu wachache .
 
news

Picha: Mpigapicha Wetu
Profesa Rwekaza Mukandala
JANA ilitimu miaka 28 kamili tangu kuzama kwa meli ya Mv Bukoba' katika Ziwa Victoria, Profesa Rwekaza Mukandala akiibua hoja mpya ikiwamo miili ya abiria kuelea kwa muda mfupi kwenye maji kunakotoa ishara walikunywa mafuta kabla ya kufariki dunia.

Vilevile, msomi huyo amesema meli hiyo ilizama kutokana na uzembe, haikusajiliwa licha ya kufanya kazi kwa miaka 17 huku nahodha wa meli hiyo akijiokoa kwanza na kutelekeza abiria wake.

Prof. Mukanadala aliyasema hayo jana, mkoani Dar es Salaam, katika Mhadhara wa Uprofesa uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kuhudhuriwa na wanazuoni pamoja na Mkuu wa chuo hicho, Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Akiwasilisha mada kwa takribani saa moja na nusu, Prof. Mukandala alisema: "Tume ya Jaji Kisanga ilitaja upungufu ya meli. Kati yake, ni meli kuongozwa na manahodha wasio na ujuzi, kujaza mzigo hasa ndizi na abiria zaidi ya 400, mara mbili ya kiwango kilichostahili."

Prof. Mukandala alisema Taasisi ya Maji ya Dermark iliwahi kufanya utafiti na kushauri meli hiyo iwe na matangi yaliyojaa maji muda wote ili kuweka uwiano wenye usawa kutokana na kasoro za meli tangu ilipoundwa na wahandisi wasio na ujuzi.

"Mnusurika maarufu anapinga maelezo kuhusu ubovu wa chombo. Rushwa na uendeshaji duni wa chombo, kutofanyiwa matengenezo kulichangia meli kuzama. Meli hii ilikuwa ikitembea upande na ikiserereka majini," alisema mwanazuoni huyo.

Prof. Mukandala alieleza kuwa inaaminika kwamba binadamu akizama huibuka baada ya siku kadhaa. Lakini mnusurika mmoja alisema wakati anajiokoa alizingirwa na mikungu ya ndizi na miili ya watu. Inawezekana walipigwa na shoti ya umeme au walikunywa mafuta.

Alisema pamoja na tukio hilo kutokea, likiwa ni miongoni mwa yaliyo makubwa nchini na kimataifa, baada ya miaka 15, ajali nyingine ya meli ikatokea, Mv Islander ikazama Bahari ya Hindi na kupoteza maisha ya takribani watu 1,000.

Prof. Mukandala alisema meli hiyo ilianza kazi mwaka 1979, ikiwa na kasoro kadhaa ambazo zilifanya isisajiliwe, akiutaja ubeberu kuwa chanzo cha meli kuzama.

"Serikali iliamua kutumia mkopo kununua meli kutoka Serikali ya Ubelgiji iliyoikopesha faranga za Kibelgiji milioni 500 wenye riba ya asilimia 8.3 kwa kipindi cha miaka saba.

"Ununuzi mzuri wa huduma ni ule wa kutangaza kwa ushindani, serikali haikufuata mchakato wa ununuzi uliozoeleka na mkopo ulikuwa wa pingu wenye masharti magumu sana.

"Serikali ya Ubelgiji iliteua kampuni ya ununuzi, kampuni ya MS Belgium Shipping ilikuwa ni kati ya muungano wa kampuni tatu zilizopata zabuni hiyo.

Shirika la Reli (msimamizi wa wakati huo) lilieleza aina ya meli inayohitajika," alisema.

Profesa Mukandala alisema kuwa meli hiyo licha ya kufanyiwa majaribio kadhaa, ilibaki kazini ikiwa na kasoro ingawa hakuna hatua zilizochukuliwa, hivyo kuhatarisha uhai wa wasafiri.

Alisema Shirika la Reli Tanzania halikuwa na muda wa kupitia na kusoma vifungu vya mkataba wa ununuzi. Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wakati huo aliagiza mkataba utiwe saini haraka.

"Inaonesha naye waziri alipewa maagizo na Rais ambaye ana madaraka makubwa, akisema linatekelezwa. Tume ya Jaji Kisanga ilisema masharti yalikuwa magumu sana," alisema.

Prof. Mukandala alisema ujenzi wa meli wa meli ulifanyika Tanzania na watu 63 ambao tume ilibaini hawakuwa na ujuzi chini ya msimamizi mmoja kutoka Ubelgiji.

Alisema kuwa Julai 27, 1979, meli ilikabidhiwa kwa Rais Julius Nyerere na kuanza kazi mwezi uliofuata. Mamlaka zote tatu; dola, Shirika la Reli hazikuchukua hatua baada ya meli kubaini kuwa na kasoro.

"Ili kukabiliana na kasoro hizo, ilibidi ibebe maji katika matangi muda wote. Uokoaji ulikuwa na kasoro wakati ajali ilipotokea.

Hakukuwa na mtaalamu wa uzamiaji hata mmoja, maboya 'kiduchu' licha ya meli kuchukua takriban saa nne. Meli ya Titanic ilizama ndani ya saa tatu lakini watu wengi waliokolewa," alisema.

Prof. Mukandala alisema, "tunajifunza kwamba madaraka ya Rais ni makubwa, kuna haja ya kuwa na mjadala kuwapo Katiba Mpya. Rais Nyerere aliruhusu hili, meli inunuliwe.

"Kuna wakati meli ilijaa maji na kuelemea upande mmoja, lilitolewa tangazo la ununuzi ili kuepusha rushwa katika mchakato wa mradi wowote."

Credit: NIPASHE
 
Huyu ni professor mbwa alikuwa wapi wakati mkapa yuko hai, mbwa wa aina hii ni hatari kwa Taifa
 
Wewe yako ni ipi

Uzwazwa ndio nini? Wewe unawajua Neanderthrals? Sisi waafrika-Tena bila ya kumumunya Homo Sapiens wametoka hapa kwetu bongo. Tanzania- Wakiwa na Akili kuliko hao Neanderthrals. Take note.

Chini ya mtutu wa Bunduki. Unaijua Maxim gun wewe?

Ndio nimesema, tumejifunza kutoka kwa Wazungu. Na hilo unabisha?

Kabla ya Wazungu tulikuwa hatupigani risasi, wakaje na maxim gun na magobole, hizo ndizo tulibadilishana nao. Ukumbuke wakati wazungu wanakuja walitukuta na sisi Waafrika tulkuwa na vita vita kama zile za Ulaya na Asia.

Hivyobasi ilikuwa ni win win situation. Wanaondoka na Chumvi, tunabakiwa na Silaha.

Sasa hasira za nini? Hivi hujui Wazungu waliwaumiza Waafrika. Ama na hilo unataka kufunika?


MIAFRIKA NI MIBWEGE. VILAZA.
 
news

Picha: Mpigapicha Wetu
Profesa Rwekaza Mukandala
JANA ilitimu miaka 28 kamili tangu kuzama kwa meli ya Mv Bukoba' katika Ziwa Victoria, Profesa Rwekaza Mukandala ]
Mhadhara wa Prof. Huyu umenikumbusha mambo yalivyokuwa kipindi cha wakati na baada ya ajali iiyo ya kusikitisha kuwahi kutokea katika ziwa Victoria.

Prof. Kaeleza mambo mengi kuzunguka ajali hiyo ambayo mengine labda hakukaririwa vyema au yana malengo fulani ambayo yatajulikana kadri muda unavyokwenda.

Mimi ni mhitimu wa darasa la saba b, hivyo mambo ya kisomi nawaachia wenye sifa hizo.

kwa mtazamo wangu mhadhara huu wa prof hasa katika suala la Mv Bukoba una mapungufu na uko sawa na tunayoifanya huku mtaani na kusikiliza wachambuzi wa sasa wa soka kwenye radio zetu, kama bado zina sifa ya kuitwa hivyo.

Nilikuwa Mwnza mjino siku ya ajali na muda mwingi baada ya ajali hiyo na story nyingi za vijiweni zilisambaa kama anavyoeleza prof.

Story kwamba, mmiliki wa vivuko vinavyotoa huduma kati ya mwanza na kamanga, kuzuiliwa kutumia meli zake kuivuta Mv Bukoba ili isizame, mkuu wa mkoa wa wakati huo methew( sina uhakina na jina la kwanza) Luhanga, kuagiza meli kutobolewa ili kuwakoa walioko hai ndani ya meli nk.

Nilihudhuria vikao kadhaa vya kesi ya Mv Bukoba ambapo Jaji Jaxton Mlay wakati akiwaapisha wazee washauri alisisitiza kuwa wasikilize na kutoa maamuzi yao kulingana na kitakachotokea mahakamani na sio walichosikia mitaani.
Kulinganna na Prof. Kuna mambo kadhaa naomba niyaeleze.
1. Meli haikusajiliwa. Hapa kuna utata. Ingawa ni kweli meli ilikuwa na tatizo la uwiano majini. Lakini, IMO ilitoa namba 763611 kwa chombo gani? Hukumu ya jaji Mlay inaeleza Mv Bukoba ilikuwa na Usajili au Prof ana eleza juu ya certficate of sea worthness? Mv Bukoba haikuwa nayo?

2. Nahodha alijiokoa kwanza kabla ya abiria. Sijui kama Prof anafahamu hiyo meli ilipinduka na haikuzama, maana kwenye kuzama taratibu nyingi zinaweza kufuatwa lakini kupinduka ni tendo la ghafla. Sidhani kama amewahi kusikia kuwa kuna abiria walirushwa kutoka kwenye meli hiyo na kujikuta ziwani ambako walijiiokoa kwa mikungu ya ndizi.
Vinginevyo, kwanini hawa wazamiaji wa ndani nje walishindwa kuitoa miili yote ndani Mv Bukoba?

3. Manahodha hawakuwa na ujuzi. Tuchukulie anasema ujuzi wa kazi yao. Shahidi wa kwanza wa upande wa serikali katika kesi hiyo, aliimbia mahakama kuu kuwa, Nahodha Jumanne Rume Mwiru amemfahamu kwa zaidi ya miaka 10 akifanya kazi ya unahodha kwa muda wote huo.

4. Taasisi ya maji ya Denmark ilikagua meli hiyo. Pengine amenukuliwa vibaya. Lakini maelezo rasmi yaliyotolewa mahakamani ni "wataalamu" kutoka Denmark. Hawa wataalamu wa maji ndio waliokagua meli ndio nimewasikia kwa Prof. Kulingana na taarifa za mahakama ambazo kila mmoja anaweza kuzi ona kupitia. Www.tanzlii.org, ukaguzi wa mwisho ulifanywa na kampuni ya Ubelgiji mwezi may 1996 kabla ya ajali na haikutoa taarifa yake.

5. Meli iilikuwa ikiserereka majini. Hii naomba niache hivyo.

6. Meli ilijengwa na watu 63. Hapa sijui alitaka kusema nini. Idadi ya watu inahusikaje? Walikuwa wengi au wachache? Hawakuwa na sifa. Ujenzi wa meli unahusisha watu wangapi na wenye taaluma zipi?

7. Hakuna hatua zilizochukuliwa licha ya meli kubainika kuwa na kasoro. Hapa Prof anajikanganya. Awali anasema kuna wataalamu wa maji waliikagua lakini anabadilika na kusema hakuna hatua zilizochukuliwa.



Samahani kwa kuwachosha na pia nimwombe radhi Prof kuwa haya ndio sisi wa darasa la saba b, tunayafahamu hayo mengine ya kisomi endeleeni ninyi.
 
Msimshangae ,inaonesha walisubiria mwanafunzi wao Tundu lisu awe mwanasiasa na aseme ubovu wakatiba ili waibue hojazaon
 
Back
Top Bottom