Prof. Muhongo asema kuwa hii habari ya 16% Share kwenye Madini huenda tumeliwa!

Aulizwe Kabudi na kina Mwendazake walioileta 😁😁

Japo Sina uhakika Kwa anachosema Kwa sababu unaposema hatuingii kwenye Management na wakati Huwa zinaundwa kampuni tanzu Zenye uwakilishi wa Serikali kwenye Management inaleta mkanganyo..

Nimemsikia Dotto akisema tutakuwa na uwakilishi kwenye management ya kampuni tanzu Kwa level zote.
Wala usipate shida.sheria ya makampuni IPO wazi mwenye share/hisa nyingi ndivyo mwenye voting power nukta..Mgawo/dividend hutolewa baada ya faida halisi kulipa Kodi za Serikali,hapa kama faida baada kulipa Kodi ni Tsh 100 Serikali itapata Tsh 16\=nukta..kama kampuni itapata hasara hakuna mgawo.hatutoboi maana ni rahisi kuonyesha kampuni imepata hasara,ukiiflate bei za capital asset itaaffect profit na allowable expenses pia.usipotaja mapato,au taja kidogo .tuna vijana wamesoma viziri ni wakati Sasa majukumu haya kupewa vijana,tuwaamini tuwape vijana

/=
 
Je kama hao wanahisa na serikali zao ndiyo wanaagiza management ndiyo itunyonye unategemea watatoa taarifa sahihi kwako 'mliwaji'/muibiwaji?

Suala la kuwa na informants wetu kwenye ngazi zote za kampuni hizi halikwepeki!
Heshima mkuu 'TUJITEGEMEE'.

Hapana.
"Wanahisa na serikali zao hawawezi kuwa ndio wanaagiza management ndiyo itunyonye..."
Kukataa wazo hilo siyo kuwakingia kifua kwamba hatupigwi katika muundo mzima wa wizi wa mali zetu kunakofanywa na watu hao.

Huko pia kuna machizi kama tulivyo nao huku kwetu. Si unakumbuka ile isu ya Rada ya Uingereza wakati ule wa Mkapa? Machizi kama Linda Walker' wa huko walilishikia bango jambo hilo hadi tukapata chenji yetu!

Ninakubaliana kuhusu swala la kuwa na watu wetu katika ngazi zote katika kampuni. Hili lingetakiwa kuwa takwa muhimu katika mikataba yote.
Lakini si unajua jinsi tunavyolainishwa? Tuanaambiwa tuna "unfriendly investment environment."
Tukisha ambiwa tu hivyo, tunaachia kila kitu.

Pili, hata tunapo kubaliwa kuwa na hao 'informer unaowasema, hawa wazalendo utawapata wapi? Natumaini unaelewa ninacholenga hapa.'
 
Tumepigwa hiyo project tungeweza kufanya kwa pesa zetu wenyewe.

Mimi naomba Rais aombwe asiingie mkataba mwingine Tena wa maskini maana sidhani kama ana weza kuhimili figisu za majambazi ya Rasilimali Toka nchi za magharibi.
 
Punguza utoto, hivi unajua TPDC ilipewa 20% ya hisa kwenye kuchimba gesi ya mnazi bay. Sasa JPM anakuja na 16% mnashangilia? Mbona nchi Ina wajinga wengi. Umeambiwa Tanzanite one tuna zaidi ya hiyo asilimia 16% Sasa kivipi Tena JPM kaboresha. Yale Yale tu zaidi tumerudi chini.

Hata Gesi ilichimbwa kwa ubia, na ndio hapo tuna 20% nani aliyekudanganya subsidiaries au joint venture zimeanza na JPM?. Mbaya zaidi kawapa 84% zote huku hatuna hata board member ndio upuuzi gani huo?
Elewe tofauti Hisa na Gawio.
JPM 16% GawioKampuni likipata faida- Taifa Bila kuweka mtaji kampuni likipata faida na lisipopata faida Taifa halina cha kupoteza
JK Mtaji 20% pesa ya Watanzania-Joint Venture. Kampuni likipata faida Taifa linapata Gawio la 20% mtaji lililowekeza na ikitokea hasara Pesa ya Taifa inapungua kwa % hiyo ya hasara. Ok
 
Haisaidii kivipi wakati ndio unaweza husika kwenye maamuzi. Na sio menejimenti Bali Bodi Ili hata investment decisions, Transfer pricing, Capital flights zote utaziona zinavyo flow so utalinda maslahi ya taifa.

I guess ulimaanisha Mwanyika? Huyo alikua muajiriwa wa Barrick wenyewe. Hapa tunaongelea Serikali kuwepo kwenye vikao vya maamuzi. Yes tutaibiwa ila at least tutakua na taarifa kuliko Sasa ambapo hata wakiunderestimate Mapato hakuna anayejua zaidi tunapewa mgao wa 16% kazi imeisha.
Heshima mkuu 'zitto junior'; lakini pamoja na kuelewa umahiri wako katika mswala ya namna hii, sijauona umahiri huo niliozoea kuuona katika mchango wako huu hapa.
Nadhani kulikuwa na kitu, msukumo pembeni uliokufanya uweke tu maneno haya hata bila ya kuongeza uzito wowote kwenye utatuzi wa swala husika.

Huo mstari wa kwanza, ukitaka kufanya hivyo, unatishiwa nyau, kwamba utakosa wawekezaji kwa kutokuwa na mazingira rafiki, na hili unalijua wazi maana yake ni nini!

Uko sahihi, nilikuwa na maana ya 'Mwanyka', asante kwa kunikumbusha kuhusu hilo, na pia ninakubaliana na wewe kwamba alikuwa ni mwajiriwa tu.
Lakini maana yake hasa ilikuwa ni ipi kumwajiri mtu kama huyo? Kuwatia usingizi wanaopigwa waone kwamba wanaye mtu wao huko huko ndani.

Mkuu 'zitto junior', kwenye maswala kama haya, kila mara nina'defer' kwa watu kama wewe, ili muweze kutufungua akili zaidi katika maeneo haya.
Nimejaribu kukumbuka mifano katika nchi za kiafrika ambazo tungeweza kusema kwamba pengine wanazo nafuu zaidi kuliko sisi kwenye maswala kama haya, lakini sioni mfano wa kuuleta hapa; labda Botwana na Namibia?

Lakini kwa hivi karibuni, akili zangu zimeaelekea zaidi Arabuni, Qatar, UAE, Saudi Arabia n.k., ambako kwa ufahamu wangu mdogo naona kama wao waliweza kuwa na utaratibu wa kuhakikisha kwamba mali zao zimetumika kubadili hali zao za maisha.
Sasa hapo ndipo ninajiuliza, wao walifanyaje?

Nimalize kwa kusema kwamba, hata sisi siyo kwamba hatukujaribu, kwa sababu ninajua Mwalimu Nyerere alinuia nasi tufaidike na raslimali hizi, kuna mambo yaliyofanyika iwe hivyo, lakini ilishindikana kwa kupigwa vita na hao hao wanaotupiga.

Ninaomba mkuu, ukitulizana vizuri, ninajua utaleta jambo zito zaidi kwenye mada kama hii kuliko hayo uliyoweka hapo juu.
 
Yaani wewe unadhani kwamba Kampuni za Madini zinapotupiga serikali zao hazijui au hazibariki hizo ishu kwa mlango wa nyuma?.
Hao lao moja!. Ni jukumu letu kujibeba, kujisimamia!
Ninakubaliana nawe kuhusu "sisi kujibeba", hilo halina mjadala. Mjadala ni sisi tukijibeba vipi huku hao tutakaowaweka huko watutetee hali zetu ndio hao hao watakaotumiwa na hao hao kutunyonga; au umesahau hili mkuu 'Missile'?

Hivi unaposikia hizi habari za "Mazingira ya Uwekezaji" kuwa rafiki au kutokuwa rafiki, wewe unadhani maana yake ni nini hasa?

Kuna haya mambo ya "Uwazi", tunayohimizwa sana sisi tuyazingatie, lakini wao hayawahusu?

Tunachokosa sisi ni kitu gani?
Kwa vile ninaheshimu sana uwezo wako wa fikra, ngoja nikuelekeze kwa mfano mzuri kuhusu swala hilo, juu ya tunachokosa sisi. Mfano wenyewe ni wa Rais Kagame na timu yake katika kampeni zake za kuwatia aibu hao hao tunaowalalamikia hapa. Kampeni ya swala la mauaji ya Kimbari yaliyotokea Rwanda.

Tunatakiwa kuwa 'vigilant' namna ile ili hawa wezi wa mali zetu wajue kwamba tunajua ushenzi wao wanaotufanyia sisi.
Lakini hatuwezi kufanya hivyio kwa sababu tupo kwenye mashindano ya kujipendkeza kwao ili tupate 'favour' zao.
 
JPM 16% GawioKampuni likipata faida- Taifa Bila kuweka mtaji kampuni likipata faida na lisipopata faida Taifa halina cha kupoteza
Gawio kivipi sisi tumeambiwa ni hisa 16% zinaitwa Free Carried Interest kama sikosei. Tena Kabudi amesema ni non-dillutable. Ina maana ikiwa faida ama hasara ni ratio ya 16%
JK Mtaji 20% pesa ya Watanzania-Joint Venture. Kampuni likipata faida Taifa linapata Gawio la 20% mtaji lililowekeza na ikitokea hasara Pesa ya Taifa inapungua kwa % hiyo ya hasara. Ok
Sawa tutaweka operating costs lakini hata returns tunapata 20%. Hoja hapa ilikua shares na ndio nasema tuliwahi kuwa na zaidi ya 20% why Sasa tukipata 16% tunaona ni hatua kubwa?
 
Mama anaupiga mwingi sana na anatoa mirija ya kupiga mwingi watu wasipate tabu kipindi cha uchaguzi
 
Kwani tunapigwa kwa sababu hatujui au tunapigwa kwa sababu wasimamizi wetu wanapata chochote kutokana na kupigwa kwetu ?
Mimi nadhani kwa ujumla wetu hatujui, tungejua tungepiga kelele nyingi sana za "MWIZIIII", hata hao wanaotumiwa katika kufanikisha kazi hiyo wangekataa kutumika kutuibia.
Tungekuwa na ufahamu jinsi mali yetu inavyozolewa, hao wanaotumika wangejua kuwa tutawaadabisha.

Kwa vile, kwa ujumla wetu kama wananchi hatujui kinachofanyika, hawa hawa tuliowaweka huko ndio wanaotumika kutuhadaa na kutulaza akili kuwa tunafaidika na hii mikataba mibovu.
 
Tuache kulaumu wawekezaji kwa matatizo yetu wenyewe.

Control ya shirika inaweza patikana kwa njia mbili
(i) kupitia 51% shares and above
(ii) au katiba inayoruhusu mtu fulani/taasisi ata kama shares ndogo kuwa na control ya management

Kwa ivyo kuwaachia wao wajiendeshee hayo mashirika wanavyoamua bila ya kufahamu kinachoendelea huko (kama kweli huo ndio utaratibu) ni uzembe wetu wa kijitakia.

Serikali za mabeberu don’t care kuhusu faida za haya mashirika kwa sana, wao wanasaidia kwenye kupata access ya resources ambazo muhimu kwa uchumi wao. Hapo ndio kwenye maslahi ya mapana ya security za kiuchumi.

Mradi wamepigana kampuni yao kupata hizo resources, swala la kuingia mkataba mmbovu ni sisi wenyewe.

Hela wanazopata nje ya nchi hazikatwi kodi huko kwao (hiyo itakuwa ni double taxation) kama ishalipiwa kodi nchi husika labda tuwe tumesamehe. Again huo tena ni uzembe wetu.

Otherwise hela iliyolipiwa kodi nje ya nchi kwa biashara ambazo zipo registered kwenye nchi nyingi za ulaya, inawekwa kwenye income statement kuonyesha tu mapato ya shirika kwa mwaka.

Mfano ndani ya nchi shirika limetengeneza faida ya 100m hiyo ndio itatozwa kodi. Cha kuzingatia malipo ya kodi yana utaratibu tofauti kwa biashara ndogo zinaweza pewa mpaka miezi tisa baada ya kufunga hesabu za mwaka ndio walipe.

Wakati biashara kubwa unaanza kulipa kati kati ya mwaka wa biashara na kila miezi mitatu baada ya hapo (accrual). So ideal kila mtu angependa kuwa biashara ndogo.

Wanaweza sema labda biashara kubwa ni zile zenye mapato kuanzia 130 million. Kwa mtaji huo kama unatengeneza 100m we ni biashara ndogo.

However kuna kigezo kingine pia kinazingatiwa je una dividend income kutokana na biashara zingine nje ya nchi, if yes hiyo hela unajumlisha. Let’s say umetengeneza 50m from Tanzania ambayo umelipa kodi huko.

Hiyo dividend huko kwao utajimlisha na 100m ambapo utakuwa biashara kubwa (umevuka 130m threshold) japo utalipa kodi in accruals ila ni kwa hiyo 100m tu. Hiyo ndio interest ya serikali zao awafaidiki moja kwa moja na hayo mapato nje ya nchi.

Na kuweza kuongopa kwenye vitabu vyao ni ngumu kwa labda uwe sio company, lakini wewe either private or public company hela uliyopata nje ya nchi itajulikana tu na kuna auditor anaekuja kuwakagua kuhakikisha hakuna janja janja kwa shareholders.

Madhira tunayopata ya mikataba mibovu ni mainly incompetence zetu wenyewe kuingia hiyo mikataba.
 
Kuwa na adabu kijana, Mnyika alipata 1.7 pale Tambaza form 4 na Advance alipata 2. Chuo amesoma UDSM ilikua BBA evening program ila alitimuliwa akiwa mwaka wa tatu sababu ya mgomo.

So usiongee utumbo usiofahamu
Toka lini Manyika akawa Mnyika,
 
Unacho sema ni kweli kabisa…..ki ukweli hata akae mtu kwenye management bado tutaliwa tu kuwa tumejaa tamaa na ubinafsi….
Kweli ndugu yangu, Botswana wamefanikiwa sana Kwa kuhakikisha kuwa madini yanasaidia nchi Kwa mikataba yenye tija....bt Tz kaazi kwelikweli.
 
Kwani tunapigwa kwa sababu hatujui au tunapigwa kwa sababu wasimamizi wetu wanapata chochote kutokana na kupigwa kwetu ?
Ndio maana yake ila watu wanajaribu kudanganya kwamba bado hatujui after 60 years !!
 
Gawio kivipi sisi tumeambiwa ni hisa 16% zinaitwa Free Carried Interest kama sikosei. Tena Kabudi amesema ni non-dillutable. Ina maana ikiwa faida ama hasara ni ratio ya 16%

Sawa tutaweka operating costs lakini hata returns tunapata 20%. Hoja hapa ilikua shares na ndio nasema tuliwahi kuwa na zaidi ya 20% why Sasa tukipata 16% tunaona ni hatua kubwa?
Mkuu 16 % free carried share maana yake ni kuwa tunamiliki 16 % ya kampuni inayochimba bila sisi kulipa hatasent tano isipokuwa kwa sababu tu madini na mgodi viko kwetu.
 
Kweli ndugu yangu, Botswana wamefanikiwa sana Kwa kuhakikisha kuwa madini yanasaidia nchi Kwa mikataba yenye tija....bt Tz kaazi kwelikweli.
Mkuu kusema UONGO ni dhambi- Botswana wanamiliki hisa za kulipia za makampuni yanayochimba. Angalia Botswana ilivyowekeza


KampuniWenye hisaMadini
Debswana Diamond LTDSerikali ya Botswana (50%) De Beers (50%)Almasi, makaa ya mawe, shaba na nikeli
Bamangwato Concession ltdSerikali ya Botswana (30%)
Anglo american (30%)
Wengine (40%)
Nikeli na kobati
Tati Nickel Mining Co.Serikali ya Botswana (15%)
Canadian Lionore Mining International (41%)
Anglo American (43%)
Wengine (1%)
Nikeli na kobati
 
Mkuu 16 % free carried share maana yake ni kuwa tunamiliki 16 % ya kampuni inayochimba bila sisi kulipa hatasent tano isipokuwa kwa sababu tu madini na mgodi viko kwetu.
"...kwa sababu tu madini viko kwetu"?

Hii ni mali yetu.
Hii siyo mali ya mwekezaji toka huko nje.

Haya madini "Mwekezaji" hatumuuzii kwa bei ya ughunduzi wake wala bei(gharama) za uchimbaji wakena uendeshaji wa kampuni yake.

Hapa ndipo tunapoanzia makosa, kuona kana kwamba hiyo siyo mali yetu.
 
Back
Top Bottom