Prof. Kitila Mkumbo - Achangia Mtaala Mpya wa Elimu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,890
939

MBUNGE PROF. KITILA MKUMBO - MAARIFA YAPATIKANE KWA LUGHA MBILI & LUGHA ISIWE KIKWAZO KWENYE KUPATA ELIMU

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam Mhe. Prof. Kitila Mkumbo akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema ni muhimu maarifa yapatikane kwa lugha ya kingereza na Kiswahili na lugha isiwe kikwazo kwenye kupata Elimu katika mtaala mpya wa Elimu unaokuja.

"Namshukuru Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuniahidi kuleta Chuo cha VETA kwenye Jimbo la Ubungo hususani Kata ya Makuburi ambayo ina idadi kubwa ya viwanda maana pale tuna kiwanda cha pili kwa ukubwa cha kutengeneza Nguo na kinaajiri watu zaidi ya 4000 na EPZA kubwa kuliko zote Tanzania" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo

"Naunga mkono Sera inavyopendekeza kwamba lugha mbili zinatumika kufundisha Kiswahili kwenye ngazi ya chini na kingereza kwenye ngazi inayofuata. Mjadala huu tunaweza kujadili kwa kuzingatia Uzalendo wa Lugha, Utamaduni na Kuangalia Taaluma (Kupanua wigo kwa vijana na hali halisi)" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo

"Hali halisi ni makosa kudhani kingereza ni lugha ya wakoloni, waingereza wapo Milioni 67 lakini Duniani tuna watu Bilioni moja wanaotumia kingereza kama lugha ya kwanza. Kingereza kuwa lugha ya wakoloni kiliisha siku nyingi ndiyo maana kuna Kingereza cha West Africa, South Africa, Kenya, Canadian ni kuonyesha kuwa Kingereza kwenye lugha ya kikoloni kilishatoka zamani" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo

"Asilimia 53 ya Tovuti (Website) zote Duniani zinatumia lugha ya kingereza. Lugha zinazofuata ni chini ya Asilimia 10. Kichina ni asilimia 2, Kifaransa ni asilimia 4, Kirusi ni asilimia 6, Kijerumani ni asilimia 6, Kihispaniola ni asilimia 5 na Kireno ni asilimia 3. Lugha ya kingereza inaendelea kuwa lugha ya Taaluma na Biashara Duniani" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo

"Nchi 10 zenye mfumo bora wa Elimu Afrika; Seychelles ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡จ, Mauritius ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡บ, Afrika Kusini, Botswana ๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ผ, Kenya ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช, CapeVede na Namibia ๐Ÿ‡ณ๐Ÿ‡ฆ nchi 7 zinatumia Kingereza kama lugha ya kufundishia na nchi tatu zinatumia kiarabu kufundishia hizi Algeria ๐Ÿ‡ฉ๐Ÿ‡ฟ, Tunisia ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ณ na Egypt ๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡ฌ " - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo

"Africa zinazosemekana kwa ubora wa Elimu ni Seychelles ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡จ na Mauritius ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡บ na zinafana na Tanzania ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ kwasababu wao wana lugha yao. Seychelles na Mauritius lugha yao ya Kitaifa ni Klior lakini lugha yao ya kufundishia ni Kingereza lakini ndiyo nchi ambazo tunazungumza zina ubora katika Elimu" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo

"Nchi 47 Duniani zinatumia Kingereza kama lugha ya kufundishia. Nchi 143 Duniani Kingereza ni somo la lazima. Takwimu za matokeo ya darasa la saba miaka 3 iliyopita ambayo tunatumia Kiswahili, Dar es Salaam shule 50 za juu zote zinatumia Kingereza kama lugha ya kufundishia ikiwemo Shule ya Msingi Olympio ya Serikali ambayo ni moja ya Shule za Serikali zinazotumia Kingereza" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo

"Hatuwezi kulaumu Kingereza kama ndiyo chanzo cha wanafunzi kushindwa kwasababu Shule za Msingi tunatumia Kiswahili lakini tafuta Shule 50 bora utakuta ni ambazo zinatumia kingereza" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo

"Tunapoandaa Mitaala tunaangalia sababu nyingi ambayo moja ya Msingi kuizingatia ni Matakwa ya Wazazi (Wazazi wanataka nini). Kabla Shule binafsi hazijapamba moto Tanzania, Watanzania wa Kati walikuwa wanapeleka watoto wao Kenya ๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช na Uganda ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ, walikuwa hawafuati Elimu walikuwa wanafuata Kingereza" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo

"Utafiti katika ya mwaka 2015-2017 tuliuliza Wazazi, ungetaka watoto wako wafundishwe na lugha gani, Asilimia 63, Wazazi 6 mpaka 7 kati ya 10 walisema wanataka watoto wao wafundishwe kwa kingereza kuanzia Awali mpaka Chuo Kikuu. Utafiti wa mwaka 2022 unaonesha ni asilimia 70" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo

"Lugha ni nyenzo muhimu sana kwenye suala la Elimu. Ni muhimu watoto na walimu watumie lugha ambayo wanaijua lakini lugha huzaliwi nayo lugha unaipata kwenye mazingira. Tanzania kuna tatizo kubwa la lugha ya kingereza na Kiswahili " - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo

"Jambo la Msingi, hutatui tatizo kwa kulikimbia, unalitatua kwa kulikabili. Tuna changamoto kubwa sana ya walimu kwenye somo la kingereza kwa idadi na ubora wao. Nchi zingine walikiri tatizo na wakaamua kufungulia milango" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo

"Tufungulie mipaka miaka 5 mpaka 10 waje walimu wa Kingereza kutoka ndani ya nchi za Afrika, wakati tunawapelekea Kiswahili tunakaribisha walimu wa kingereza, ndani ya Miaka 5 mpaka 10 tatizo hili litakuwa limeisha. Tuwekeze sana kwenye walimu wa somo la kingereza" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo

"Tunakipenda Kiswahili chetu, watoto wa kitanzania lazima wawe na kingereza kizuri na Kiswahili kizuri. Kitabu kitakuwa kwa lugha ya Kiswahili na kingereza na mitihani atapewa ya lugha ili ajibie lugha anayoweza kujibia. Muhimu ni kwamba maarifa yapatikane kwa lugha mbili Kiswahili na kingereza, na lugha isiwe kikwazo kwenye kupata Elimu" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo
 
Attachments

  • FTjOLI-WQAAKrX1.jpg
    FTjOLI-WQAAKrX1.jpg
    52.1 KB · Views: 11
Sitaki kuamini mpaka leo lugha ya kufundishia na kujifunzia inapewa promotion ambayo haipo

Lugha ni medium tu, kinachotutesa ni ulimbukeni wetu wazazi na watanzania wengi

Nani kasema ili maarifa yawe maarifa au yawafikiwe wanafunzi ni lazima yake kwa lugha fulani?

Maarifa sio static wala sio inelastic wala sio rigid

Laiti kama mtaala wetu ungeweza kuwajengea kiu, shauku, hamu, nia au kusudi maalumu kwa wanafunzi kutafuta maarifa mapya lugha is nothing!!
 
Akili za Watumwa bana daaah! Yaani kweli Profesa mzima unakwenda bungeni kusema ni LUGHA gani bora kufundishia?
Unatoa mfano wa kukoloniwa tena kwa fahari bila aibu ilihali Tanzania imetumia Kiingereza toka Mkoloni na ipo chini kielimu, ni Historia gani mnatumia?

Haya hao China na India wasiotumia Kiingereza je wao wako wapi? Ati Seychelles na Mauritius wana Elimu ya juu kwa sababu ya Kiingereza! For real? Sio Mitaala ya Elimu bali ni lugha ya Kiingereza! Kwa nini basi sisi Kenya, Uganda, Nigeria hatupo top?

Jamani ndugu zangu wapo watu wanazungumza Kiingereza safi na kafika darasa la saba!. Hao kina Hamornize wanaweza hata kuzungumza vema Kiingereza kuliko Profesa wa UDSM kwa nini?

Kiingereza ni LUGHA sio ELIMU. Ulaya ni nchi ngapi zinafundisha masomo kwa Kiingereza? Je kwa nini wenye Kiingereza chenyewe hao Uingereza nchi yao haiongozi kwa elimu bora Ulaya?

Kitila kanisikitisha sana kutoa mifano ya ajabu ajabu kama hii..
 
Ni sawa kuwa na lugha yoyote na pia kuwafundisha watoto.lugha za ziada kama kichina, kifaransa, kijerumani ili mradi mtoto azijue lugha za kimataifa pia

Lakini tusiishie kuwafundisha lugha tu bali hayo masomo yawe na tija kwa mtoto
Aelewe anasoma nini na hicho alichosoma anaweza kufanya lolote la maana kutokana na elimu hiyo?

Wanapokuwa maabara wasiishie kumpasua tu chura au sungura bali watafute na mengine

Wenzetu sixth form wanatengeneza dawa za tiba kwenye maabara zao na baadae zinauzika pharmacy zao na duniani pia
Sasa sisi ana PhD hata meza haweza kutengeneza
 
Ulaya kila nchi wanafundisha watoto wao kwa Lugha zao.wenyewe. Kwa nini wasifundishie kwa Kiingereza? Lakini nenda mtaani utakuta wapo wanaozungumza kiingereza maana Kiingereza ni LUGHA.

Unamfundisha mtoto kwa lugha ya kigeni Kiingereza ili iweje? Maana hoja kubwa ya Elimu ni kwamba iwe na manufaa kwake na jamii.

Sasa umemfundisha mtoto kwa kiingereza kenda kuwa bwana Shamba kule kijijini ambako asilimia 99 hawajui Kiingereza inakuwaje? Au lengo ni mtoto aweze kwenda Ulaya akafanye kazi au sijui atafute ajira katika mashirika ya nje? Nini malengo ya matumizi ya lugha ya kigeni haswa?

Wakenya wanatushindwa sii kwa sababu ya Elimu bali nidhamu ya kazi na kujiamini! Fundisheni Kiingereza kama lugha ya ziada kama wanavyojifunza huku Ujarumani Ufaransa, Sweden, China, India na kadhalika.
 
Akili za Watumwa bana daaah! Yaani kweli Profesa mzima unakwenda bungeni kusema ni LUGHA gani bora kutundishia?
Unatoa mfano wa kukoloniwa tena kwa fahari bila aibu ilihali Tanzania imetumia Kiingereza toka Mkoloni na ipo chini kielimu, ni Historia gani mnatumia?

Haya hao China na India wasiotumia Kiingereza je wao wako wapi? Ati Seychelles na Mauritius wana Elimu ya juu kwa sababu ya Kiingereza! For real? Sio Mitaala ya Elimu bali ni lugha ya Kiingereza! Kwa nini basi sisi Kenya, Uganda, Nigeria hatupo top?

Jamani ndigu zangu wapo watu wanazungumza Kiingereza safi na kafika darasa la saba!. Hao kina Hamornize wanaweza hata kuzungumza vema Kiingereza kuliko profesa wa UDSM gani?

Kiingereza ni LUGHA sio ELIMU. Ulaya ni nchi ngapi zinafundisha masomo kwa Kiingereza? Je kwa nini wenye Kiingereza chenyewe hao Uingereza nchi yao haiongozi kwa elimu bora Ulaya?

Kitila kanisikitisha sana kutoa mifano ya ajabu ajabu kama hii..

Ndio maana tunataka Kiswahili kitumike, maana athari ya kingereza imejidhihirisha kwa kauli za Kitila mwenyewe.
Kama hayo ni mawazo ya Profesa, hakuna haja ya kujiuliza mara mbili kufumua huu mfumo wa Elimu.

Profesa anashindwa kutofautisha Kiingereza kama Lugha ya Kufundishia Tz na Kiingereza kama Lugha kuu ya Mawasiliano duniani.

Nani kamdanganya ili uwasiliane na dunia kuhusu Historian yako ni lazima ufundishwe kwa Kiingereza?

Hawa wameshikiwa akili, na zimefichwa mbali nao. Hapo wako empty kichwani.
 
Akili za Watumwa bana daaah! Yaani kweli Profesa mzima unakwenda bungeni kusema ni LUGHA gani bora kufundishia?
Unatoa mfano wa kukoloniwa tena kwa fahari bila aibu ilihali Tanzania imetumia Kiingereza toka Mkoloni na ipo chini kielimu, ni Historia gani mnatumia?

Haya hao China na India wasiotumia Kiingereza je wao wako wapi? Ati Seychelles na Mauritius wana Elimu ya juu kwa sababu ya Kiingereza! For real? Sio Mitaala ya Elimu bali ni lugha ya Kiingereza! Kwa nini basi sisi Kenya, Uganda, Nigeria hatupo top?

Jamani ndugu zangu wapo watu wanazungumza Kiingereza safi na kafika darasa la saba!. Hao kina Hamornize wanaweza hata kuzungumza vema Kiingereza kuliko Profesa wa UDSM kwa nini?

Kiingereza ni LUGHA sio ELIMU. Ulaya ni nchi ngapi zinafundisha masomo kwa Kiingereza? Je kwa nini wenye Kiingereza chenyewe hao Uingereza nchi yao haiongozi kwa elimu bora Ulaya?

Kitila kanisikitisha sana kutoa mifano ya ajabu ajabu kama hii..
Mwenzio katoa data ku-back up hoja zake toa za kwako tulinganishe.
 
Data zipi unataka? Wachina na Wahindi wanafundisha kwa Kiingereza? Hawa nao mbona walitawaliwa na Muingereza kama sisi.lakini hawatumii Kiingereza kufindishia.

Sasa imekuwaje wao wanaongoza kwa elimu bora duniani baada ya kuachana na Kiingereza. Halafu mifano alotumia Kitila ni nchi maskini kama sisi, ambazo bado maskini msijiulize kwa nini bado maskini kama Elimu nzuri wanayo lakini bado ni maskini?
Unaupimaje Ubora wa Elimu kwa lugha ilotumika unatumia vigezo gani?

Unatumiaje mfano wa Maskini mwenzako ambaye kwa miaka 60 katumia elimu hiyo na bado maskini?. Kwa nini asitumie nchi zilizoendelea maana Elimu ni msingi wa maendeleo ya nchi. Kweli Seychelles ni model wa kufuatwa na sisi?

Ya kuambiwa Changanya na zako. Kitila mtu wangu sana lakini katika hili sikubaliani naye..
 
Sitaki kuamini mpaka leo lugha ya kufundishia na kujifunzia inapewa promotion ambayo haipo

Lugha ni medium tu, kinachotutesa ni ulimbukeni wetu wazazi na watanzania wengi

Nani kasema ili maarifa yawe maarifa au yawafikiwe wanafunzi ni lazima yake kwa lugha fulani?

Maarifa sio static wala sio inelastic wala sio rigid

Laiti kama mtaala wetu ungeweza kuwajengea kiu, shauku, hamu, nia au kusudi maalumu kwa wanafunzi kutafuta maarifa mapya lugha is nothing!!
Tatizo lilianza kwa Nyerere alipopokea nchi
 
Kabisa, halafu ati mifano yake Seychelles, nchi ambayo mpaka leo kama imetawaliwa na Wafaransa, hawana lugha yao. Kiuchumi ni mbovu kuliko maelezo.
 
Mimi nachagua upande wa Prof. Kitila Mkumbo sababu naziona athari za mfumo wetu wa kiswahili elimu ya msingi kisha elimu ya upili na ya juu watu wanapata shida.
Upataji wa maarifa kupitia elimu ya darasani unapaswa uwe rahisi na kwa mtiririko sahihi. Nenda shule za upili (secondary) uone watoto waliosoma elimu ya msingi kwa kiswahili wanavyopata shida kuelewa vitu kwa kiingereza. pengine vingine ni marudio tu ya walichosoma kwa kiswahili.
Kuna shule toka Januari hadi Machi wanapambana na english course tu.

Tunatakiwa kuchagua lugha moja toka elimu ya awali hadi elimu ya juu. Si lazima iwe kiingereza. Huu mfumo wa sasa unachangia watu kuwa na elimu ya kukariri vitu bila kupata maarifa kwa usahihi na kwa undani.
 
Mh Kitila na viongozi wote wa elimu wanao husika na mtaala muelewe kuwa wananchi hawana shida na lugha yoyote kutumiwa kama lugha ya kufundishia na kujifunzia malalamiko yao yamekuwa wazi siku zote na hata rejea ya tafiti alizozitoa zinayo majibu ambayo ni haya;

1. Shida kubwa ni pale mtoto anapofundishwa kwa kiswahili s/msingi na akienda sekondari anafundishwa kwa lugha ya kiingereza jambo ambalo kwa zaidi ya 75% ndicho chanzo kikubwa cha kufanya vibaa kidato cha nne. Tafiti nyingi zinathibitisha hili.

2. UAMUZI UPI SAHIHI?
Wananchi wanatamani kuona maamuzi sahihi ya maoni yao na tafiti za wataalam kwamba "Ama tuamue kutumia kiswahili kuanzia awali hadi chuo kikuu na kiingereza libaki kuwa somo" au "kiingereza kiwe lugha ya kufundishia kuanzia awali hadi chuo kikuu na kiswahili liwe somo la lazima".

Huu Ndio uamuzi mgumu lakini ulio sahihi. Shule zote ziwe na mfumo mmoja ziwe za serikali au binafsi.

3. Wananchi wamekuwa na malalamiko yenye mlengo wa kibaguzi pale ambapo wanaona watoto wa viongozi wote, matajiri, na baadhi ya watumishi wenye kipato cha Kati na juu wakiwapeleka watoto wao ktk shule za kiingereza na pindi wanapohitimu na kwenda kwenye usaili wa ajira asilimia kubwa ya wale wahitimu waliosoma kwa kiingereza wamekuwa walipata ajira kuliko wahitimu wengi wa Wananchi maskini waliosoma kwa kiswahili ambao hukatwa mapema kwa kushindwa kijieleza kwa lugha ya kiingereza. Nalo hili pia limedhihirishwa ktk tafiti.

4. UGUMU UNATOKA WAPI?
Ukweli unaoogopwa kusemwa na viongozi ktk kufanya uamuzi sahihi ni huu hapa;

(i) Ikiwa shule zote zitakwenda ktk mfumo wa lugha moja ya kufundishia na kujifunzia kwa shule zote binafsi na serikali ni kwamba kutahatarisha soko la shule za binafsi ambazo nyingi ya shule hizo ama zinamilikiwa na viongozi au Wanamiliki hisa ktk shule hizo.

(ii). Bado baadhi ya viongozi wanaona kuwa ushindani wa ajira kwa watoto wao inaweza kuwa hatarini kitaifa na kimataifa.

NAWASILISHA.
 
Mimi nachagua upande wa Prof. Kitila Mkumbo sababu naziona athari za mfumo wetu wa kiswahili elimu ya msingi kisha elimu ya upili na ya juu watu wanapata shida.
Upataji wa maarifa kupitia elimu ya darasani unapaswa uwe rahisi na kwa mtiririko sahihi. Nenda shule za upili (secondary) uone watoto waliosoma elimu ya msingi kwa kiswahili wanavyopata shida kuelewa vitu kwa kiingereza. pengine vingine ni marudio tu ya walichosoma kwa kiswahili.
Kuna shule toka Januari hadi Machi wanapambana na english course tu.

Tunatakiwa kuchagua lugha moja toka elimu ya awali hadi elimu ya juu. Si lazima iwe kiingereza. Huu mfumo wa sasa unachangia watu kuwa na elimu ya kukariri vitu bila kupata maarifa kwa usahihi na kwa undani.
Sasa Mkuu wangu kama unayosema ni kweli, mbona viongozi wetu wote walisoma shule hizo hizo na leo maprofesa au ndio tuseme ni maprofesa wa Uongo?

Binafsi nimesoma elimu ya msingi kwa Kiswahili na tulikuwa na somo la lugha ya kiingereza kuanzia darasa la 5 lakini tofauti ni kwamba mbali na somo hilo binafsi nilijifunza lugha ya kiingereza.

Tatizo la Elimu kwa lugha ya kigeni ndio chanzo cha watoto wengi kushindwa mitihani kwa sababu sio anatihaniwa kwa lugha asiyoijua. Wanapata taabu sekondary kwa sababu ya lugha lakini sio Wajinga.

Mwanafunzi anaweza kujua jibu la swali lakini lugha ikampiga chenga hajui spell ya neno hilo. Kiingereza kina istilahi (terminology) mwanafunzi anashindwa kujua jibu ni lipi hata ukimpa achague a,b,c au d.
Kisha mkuu wangu mtoto wa Kiswahili hata kabla hajaenda Kinda anajua Baba, Mama, Dada, anajua kuhesabu moja mpaka 10 na maana zake. Mwambie mtoto ni embe moja atakupa moja sio mawili kwa sababu anajua moja ni nini?

Leo ukambadilishie luhha ati one, two, three iwe hata darasa la 5 lazima achanganyikiwe kwa sababu anajua one ni moja kwa.matamshi lakini hawezi kuandika ONE pengine ataandika WANI maana sio lugha yake. Jibu sawa lakini kashindwa spelling.

Kifupi, huwezi futa UJINGA kwa lugha. Lengo la Elimu ni kufuta UJINGA au sio? hata Waingereza wwenyewe wapo Wajinga.

La kujiuliza tutawezaje kufuta UJINGA kwa wananchi walio wengi ikiwa hata walimu wenyewe wengi hawajui Kiingereza, hawakizingumzi hata majumbani lakini wote wanazungumza Kiswahili?

Tuanzie hapo.
 
Nishereheshe maelezo yangu kwa.kusema hivi. Dunia nzima inatutegemea sisi kuwa Waalimu wa lugha ya Kiswahili badala yake sisi tunakiacha kiswahili kwa sababu tunadhani Lugha ya Kiingereza ndio bora zaidi kufundishia. Ubora upi? wa KIKI mtaani?

Matokeo yake tunazalisha vijana wasiokijua Kiswahili, wanachanganya lugha sijui Kiswangilish mpaka Bungeni imekuwa kawaida! Wakati EA, SADC na nchi za AU wote wanajadili sasa hivi kukifanya Kiswahili kiwe lugha ya Afrika nyie mnadharau utajiri mlojaliwa nao.

Kesho, Kenya wakianza kukitawala mtaanza kusema Wakenya wametuibia, kiswahili ni lugha rasmi ya Tanzania! Siku zote tunachelewa kujielewa mpaka tumefikwa..
 
Hivi kweli tunachagua mfano wa Nchi ya China inayotumia lugha yake kufundishia kujilinganisha na sisi?

Sisi bado tunasaini mikataba ya kilaghai kuwaumiza wananchi.

Tuache ukanjanja kwanza, lugha sio tatizo. Nipo upande wa Kitila (Prof)
 
Lugha ni tatizo ndio maana Mikataka inasainiwa na hao maprofesa kumbe wamepigwa Kiingereza cha ndani.

Ebu niwaulize nyie wachumi mlosoma kwa Kiingereza muwafahamishe vizuri Wananchi ilu waelewe. (Watokane na Ujinga)

Hiyo mikataba: - Unawezaje kupewa asilimia 16 ya mtaji, lakini mtagawana faida 50/50 na mwekezaji?
 
P
Lugha ni tatizo ndio maana Mikataka inasainiwa na hao maprofesa kumbe wamepigwa Kiingereza cha ndani.

Ebu niwaulize nyie wachumi mlosoma kwa Kiingereza muwafahamishe vizuri Wananchi iplu waelewe. (Watokane na Ujinga)

Hiyo mikataba: - Unawezaje kupewa asilimia 16 ya mtaji, lakini mtagawana faida 50/50 na mwekezaji?
prof anasaini kwa agizo la mkuu wa nchi. Hawana cha kujutia. Ndiyo maana Prof Assaad aliwagomea kipindi flani , kufanya kazi za kushikiwa akili.
 
Nimekuuliza swali sikuuliza nani anafanya au alifanya nini? Asad hajawahi kuuliza swali nilouliza.

Mwigulu alisimama bungeni na kusema Trab and Trat kila mtu akacheka maana hawajui alimaanisha nini kumbe njia ya kuwatoa mstarini.

Pale mkutano wa Wafanya biashara wa Kariakoo Mwigulu amechambwa kama nini kwa sababu huyu msomi alofundishwa kwa Kiingereza hajui atawezaje wasaidia Waswahili. Elimu isiyotuondoa katika UJINGA sii ELIMU tunayoitaka.
 
If you cannot defeat them join them!Ukweli utabaki kuwa Ukweli tu kwamba kingereza kinahitajika kuliko kiswahili chetu.Na wasiojua Sababu ya kingereza kuwa na nguvu kuliko lugha zingine,Sababu ni hizi hapa,kwamba ili lugha iwe powerful lazima
1, taifa au mataifa yanayotumia lugha hiyo yawe na uwezo kiuchumi.Sasa linganisha uchumi wa mataifa yanayotumia kiswhili na kingereza kiuchumi(hapa namanisha indigenous country of English) eg Britain and USA
2.The language .must be well researched and documented.Haya angalia vitabu mbali mbali vya kitaluma kama falsafa,utawala,psychology etc vimeandikwa kwa kingereza nenda hata kwenye maktaba zetu za mikoa kama utapata vitabu vya maana vya kiswahili.
3, Pia lazima lugha hiyo utumike zaidi ktk nyanja za sayansi,huwezi kulinganisha kiswahili na kingereza ktk kuelezea issue za kisayansi,japo mtu atapinga kuwa sayansi sio kingereza.kwa kifupi Kuna Sababu nyingi Sana kwa nini kingereza ni powerful kuliko kiswahili.Na hata tupambane vipi hatuwezi kuuondoa Ukweli huu.Ni heri tuamue kuungana nacho tu kwa kukitumia kama lugha ya kufundishia
 
Back
Top Bottom