Prof. Mbarawa: Treni za SGR ni za mwendo wa kawaida (siyo mwendokasi)

Mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa amesema treni ya SGR itatumia saa moja na nusu kutoka DAR mpk Moro na itatumia msaa 3 kutoka DAR mpk Dodoma.

Ndipo waziri wa uchukuzi prof. Makame Mbarawa akasema "naomba wananchi waelewe hii treni siyo ya high speed kama zile za China na South Korea. Na hata ujenzi wa reli yake ni tofauti na hii ya kwetu ".

Source: ITV habari.

My take; Naona kama tumebadllishiwa gia angani. Mbona mwanzo tuliambiwa itakuwa treni ya mwendo kasi? Kama Dar mpk Moro ni saa moja na nusu, kuna haja gani ya kuitumia? Si ni bora watu waendelee kutumia IST ama Vitz zao tu?
Jana nimebahatika kuiona ikikatisha mitaa ya shaurimoyo kwa speed ile mi natangulia kufika Moro nikiwa na baiskeli yangu..
 
Bado ni nafuu sana kutumia masaa 3 kwasababu Dar - Dodoma kwa Bus ni masaa 9 kwahiyo kuna unafuu sana
Hawa kenge hawalioni hili kabisa kama kuna unafuu...wao wako negative tu. Wapande IST zao tu afu watumie saa 1 kufika Dodoma ili waridhike
 
Bongo bhana na mabasi ya mwendo kasi hili jina libadilishwe mwendokasi gani mwisho 60km/h!
 
Hakuna nchi Afrika yenye uwezo wa kumiliki high speed train.
Hizi ni medium speed na sio high
 
Wamewanyima wananchi wa Dar Haki ya kukutana kwa kuwatenganishia uzio wa sengenge pasipo sababu utadhani treni itapita Kila baada ya dakika tatu
 
Tafsiri ya uwekezaji huo mkubwa imebebwa na dhana ya mwendo kasi ili kuokoa muda na kuchochea ukuaji kwa uchumi
Na hili ndio ilikuwa vision and mission ya huo mradi, na sio haya tunayosikia sasa hivi. Kweli hii nchi bila mabadiriko ya kichama, watu wapya kuunda serikali maendeleo ya kweli tutabaki kuyasikia kwa majirani tu miaka nenda rudi.
 
Nakubaliana na wewe kabisa, isipokuwa wakati mwingine unajikuna pale unapoweza. Kwa hali ya ya uchumi wa nchi, ambao bado unategemea huruma za wahisani na mikopo, inabidi tupange na kuchagua kipi cha kufanya sasa hivi na kipi kifanywe baadae.

Haiwezekani nchi ijiingize kwenye mega economic development projects zaidi ya sita, ambazo zinagharimu trillion of shillngs, na ambazo tunategemea kukoapa na kupewa na wafadhili, halafu tutegemee kupata World class results. Binafsi, sidhani kama that is possible hata kidogo.
Hebu angalia hii miradi ya maendeleo ambayo nchi iliamua kuianzisha kwa ajili ya maendeleo ya nchi:
-SGR
-Mwalimu Nyerere Hydro Electric Dam
-Daraja la Busisi/ Kigongo
- Tanzania/ Uganda pipeline kutoka Tanga
-Kuna miradi kibao ya mwendo kasi inaendela hapo Bandari Salam.
-Kuna lile daraja kule kwa matajiri, Msasani Peninsula
- Nasikia Kuna project nyinge ya kutandaza Cable wire kule Mt. Kilimanjaro kwa ajili ya utilii.

Hii yote ni miradi mikubwa sana Na yenye gharama. Bila kuweka kipaumbele, kuna baadhi ya miradi tutabambikiwa tu au itakamilishwa below standard. Kuna msemo kwenye lugha ya wakoloni , unasema, "Don't bite off more than you can chew". Na ndicho tunachofanya.

Binafsi naona ni vizuri turidhike na kile tunachoweza kumudu.
Shida ni kwamba hatupendi kutumia PPP kutoka private sector. Kila kitu ni cash wakati miradi ya PPP mwekezaji atajenga na kurudisha pesa yake hata ikiwa miaka 20, 30 n.k
 
Mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa amesema treni ya SGR itatumia saa moja na nusu kutoka DAR mpk Moro na itatumia msaa 3 kutoka DAR mpk Dodoma.

Ndipo waziri wa uchukuzi prof. Makame Mbarawa akasema "naomba wananchi waelewe hii treni siyo ya high speed kama zile za China na South Korea. Na hata ujenzi wa reli yake ni tofauti na hii ya kwetu ".

Source: ITV habari.

My take; Naona kama tumebadllishiwa gia angani. Mbona mwanzo tuliambiwa itakuwa treni ya mwendo kasi? Kama Dar mpk Moro ni saa moja na nusu, kuna haja gani ya kuitumia? Si ni bora watu waendelee kutumia IST ama Vitz zao tu?
Ndio Mana wenye mabus wananunua kila siku mnk walisha nuza kuwa gari Moshi hyo hataweza kukimbizana. Na mabus
 
Hiyo tofauti ya ujenzi kati ya reli za China na Korea na hii reli yetu ya SGR ni ipi?

Nina wasiwasi Mbarawa asijekutumia udhaifu wao wa kununua vichwa chakavu vya treni ya SGR, vilivyosababisha spidi iwe ndogo, akahamishia kwenye ujenzi wa reli.

Maana naona siku hizi ni kama kuna mchezo huko serikalini wa kumtupia lawama The late Magufuli kwenye kila kitu.

Wajanja wamekula pesa kwenye ununuzi wa vichwa vya treni, wameachwa hawafanywi chochote na bosi wao, wapo tu wanatamba kwa ukwasi..

Leo malengo ya utengenezaji wa reli ya SGR ili kurahisisha usafiri yameshindwa kufikiwa, lawama inatupiwa njia ya treni!.

Mbona hili jambo halikuwahi kusemwa kabla? sasa kuna maana gani ya kuwa na hiyo reli ya SGR?

Prof. Mbarawa ameonesha incompetence muda mrefu sana kwenye hiyo wizara, ajabu anaachwa tu, na haya ndio matokeo yake.

Kwa kauli hii ya Prof. Mbarawa, sasa hata ujenzi wa JNHPP nao hauna maana, lile bwawa sasa limegeuzwa la kutuondolea ile migao yao ya umeme wanayoitengeneza, yale malengo mahususi ya kuzalisha umeme wa kuendesha treni ya SGR yamekufa.

I doubt kama yupo atakayekuwa tayari kupoteza muda wake atoke Dsm kwenda Morogoro kwa masaa matatu, wamechezea pesa nyingi, wamepoteza muda, wameshindwa kufikia malengo.
Na ndio maaan matajiri wanazid kuzinunua mabus ya safari ndefu walisha nuza harufu za kitapeli
 
Mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa amesema treni ya SGR itatumia saa moja na nusu kutoka DAR mpk Moro na itatumia msaa 3 kutoka DAR mpk Dodoma.

Ndipo waziri wa uchukuzi prof. Makame Mbarawa akasema "naomba wananchi waelewe hii treni siyo ya high speed kama zile za China na South Korea. Na hata ujenzi wa reli yake ni tofauti na hii ya kwetu ".

Source: ITV habari.

My take; Naona kama tumebadllishiwa gia angani. Mbona mwanzo tuliambiwa itakuwa treni ya mwendo kasi? Kama Dar mpk Moro ni saa moja na nusu, kuna haja gani ya kuitumia? Si ni bora watu waendelee kutumia IST ama Vitz zao tu?
About na shabby na wote waliopo bungeni hawaendi kwakuwa wanaumi?wa na shida za watu wao. Hili ndilo linawapeleka bungeni sasa
 
Hiv kutoka Huko DAR kwenu mpaka Moro Kuna vituo vingapi wakuu?
Na kama vituo ni vingi sana kwa spidi hii inatosha
Lakini kama hakuna kituo hapo katikati aaaah ni ndogo sana hiyo spidi
 
Shirika la reli limeandika kuwa umbali kutoka DAR mpk Moro ni km 300 na speed ya treni ni 160 kmph. Kimahesabu ni kwamba treni hiyo itatumia saa 1 na dk 52 (~2 hrs), ukiongeza na saa 1 la kuisimamia na kupakia unapata masaa 3. Huu ni muda sawa na wa mabasi.
 
Aisee!
 
Mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa amesema treni ya SGR itatumia saa moja na nusu kutoka DAR mpk Moro na itatumia msaa 3 kutoka DAR mpk Dodoma.

Ndipo waziri wa uchukuzi prof. Makame Mbarawa akasema "naomba wananchi waelewe hii treni siyo ya high speed kama zile za China na South Korea. Na hata ujenzi wa reli yake ni tofauti na hii ya kwetu ".

Source: ITV habari.

My take; Naona kama tumebadllishiwa gia angani. Mbona mwanzo tuliambiwa itakuwa treni ya mwendo kasi? Kama Dar mpk Moro ni saa moja na nusu, kuna haja gani ya kuitumia? Si ni bora watu waendelee kutumia IST ama Vitz zao tu?

...........................................................................

UPDATES.
Shirika la reli limeandika kuwa umbali kutoka DAR mpk Moro ni km 300 na speed ya treni ni 160 kmph. Kimahesabu ni kwamba treni hiyo itatumia saa 1 na dk 52 (~2 hrs), ukiongeza na saa 1 la kuisimamia na kupakia unapata masaa 3. Huu ni muda sawa na wa mabasi.

Hiyo ni sawa wawe na tran mbili moja direct ambayo haisimi na ile insyosimama kula kituo ambayo itatumia dakika 192.
 
Back
Top Bottom