Prof. Mayunga Nkunya kwa hili Unatuchanganya kabisa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Mayunga Nkunya kwa hili Unatuchanganya kabisa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Katikomile, Feb 12, 2010.

 1. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Katika lile sakata la mafisadi wa elimu Tanzania, nashindwa kuelewa hasa kazi ya tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) ni nini?

  Jana Prof. Mayunga, boss wa Tanzania Commission for Universities, amesema eti wao hawawezi kusema vile vyeti vya waheshimiwa ni feki ama sio kwa sababu hawajapelekewa wakaviona. Hapo ndo napata homa ya matumbo kabisa!!!!!!!!!!!

  Hivi si ndio hao hao TCU wanatuimbia kila siku kwamba tukipata chuo cha nje kutaka kusoma ni bora uwaone wao kwanza wakushauri kama chuo hicho ni accredited or not?

  Sasa mwanaharakati Msemakweli katika kitabu chake si kataja hivyo vyuo, na kwenye website ya bunge si kuna qualification za hao waheshimiwa na hivyo vyuo vyao?

  Je, TCU hawaoni kama wamekwisharahisishiwa kazi?

  AU NDO STYLE YA FUNIKA KOMBE?????????
   
 2. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Prof Mayunga amechoka sana anaogopa kuwa wa kwanza kumfunga Paka kengele
   
 3. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 667
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Prof. Mayunga Nkunya ni mmoja ya wasomi dhaifu na waoga sana. Elimu aliyopata haijampa uhuru kamili, anawaogopa sana wanasiasa kwani anaamini ndiyo wanaomfadhili kwa kumpa vyeo uchwara. Kuna wasomi wa aina mbili, wapo waliokombolewa na elimu yao,ambao wao vyeo uchwara siyo priority na kila siku wanasema ukweli tu.

  Wapo wasomi dhaifu, waoga, opportunist na walafi ambao hawawezi kuusimamia ukweli. Wao kila kukicha wanafanya kazi kwa matakwa ya wanasiasa. Kama wasomi wangetekeleza wajibu wao kulingana na taaluma zao basi nchi hii ingeenda. Lakini wasomi wa hapa kwetu ni waoga sana kuhoji na kusema ukweli.


  Suala la vyuo visivyotambulika halina kificho tena hapa nchini. Mzumbe tayari wamefuta kwenye prospectus zao qualification ambazo baadhi ya lecturers waliandikiwa kuwa wanazo. Msemakweli (kama jina lake) kachukua hatua zaidi kwa kuwaanika hawa watu na kuweka rekodi sahihi ili hata kizazi kijacho kijue kuwa ukifanya mambo ya elimu biashara utakutikana na masahibu kama haya. Kuna baadhi ya watanzania walikuwa either wanataka kusoma vyuo hivi au tayari wako wanasoma katika vyuo hivi nadhani watajifunza jambo.

  Elimu lazima iheshimiwe na kila mtanzania. Kuna watu wanachukua four years kufanya PHD kwa shida kweli kumbe kuna wengine wananunua tu. Isifike mahali pesa ikawa mbadala wa elimu. Kila kitu kina umuhimu wake.

  Argument za Profesa zilikuwa dhaifu sana. Msemakweli kabla ya kuandika kijitabu chake alifanya research na katika moja ya kazi zake alipata taarifa TCU kuwa vyuo hivyo havina accrediation. Sasa alichokosea kisheria ni nini?

  MAkongoro Mahanga kama kweli ameenda mahakamani anataka kuaibika. Makongoro ana elimu yake nzuri tu,sijui kwanini aliingia kwenye mtego wa vyuo bandia.
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,916
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Prof. Nkunya ni mchovu sana ktk maamuzi na hata akiwa pale UDSM alikuwa akiyumbishwa na wanasiasa. Kwa hili ananendelea kujifedheesha mbele ya umma.

  Kama anasema Ndugu Msema kweli kakosea je, TCU walikuwa wapi siku zote hizo? Na je, TCU inafanya nini mpaka wananchi waingilie kati kujaribu kupambana na mafisadi wa elimu?

  Mimi nilitegemea kuwa TCU ingewachunguza watuhumiwa akina Mahanga, nchimbi na wengine, lakini cha ajabu TCU iko kimya tu kwa kuwaogopa eti ni mawaziri.

  It's time now prof Nkunya uachie ngazi hapo TCU umeshindwa.
   
 5. w

  wasp JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Prof. Nkunya Mayunga, a simple advise for you. You have totally underperformed as an Executive Director of TCU because you are coward of facing headon politicians who have forged their academic qualifications. You better go back to UDSM and teach.
   
 6. O

  Omumura JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama kuna profesa hopeless kwa sasa nchi hii ni pamoja na Mayunga nkunya, huyu jamaa ameaminiwa akapewa hicho cheo uchwara eti cha kuhakiki degree, alikuwa wapi siku zote mpaka Msema kweli atokee na kumwumbua?tena angalijua asiongee kitu kwa sasa, anawaonea aibu hao mafisadi wanaoiba kutwa kucha pesa za walipa kodi wa nchi hii kwa kwenda nje kusoma degree haramu huku watoto wa maskini wakikamatika vilivo kutoka kwa maprof wa kibongo. Mayunga nkunya asiongee kwa sasa lolote, kama ana nguvu aanze kwa kubatilisha degree feki za Mary nagu, Kamala, Emanuel nchimbi, Dialo na wengine wengi tu wamejaa, aache kupoteza lengo la sivo atalaaniwa na watanzania!
   
 7. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Unaona sasa! Kumbe TCU nao walimpa data, it means tayari wanafahamu vyuo hivyo ni feki? wanaona soo kuumbuana?
   
 8. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Tatizo ni kwamba wabunge hao hao ndo wako kwenye kamati mfano ya elimu na ndi hao hao wenye uwezo wa kum-summon Mayunga! Kazi ipo!
   
 9. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 463
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  jamani mbona hata pale UDSM jamaa aliprove failure, we kama kweli yeye ndo chief academic officer badala ya kuangalia maslahi ya wanafunzi kila cku yeye alikuwa wa kwanza kufunga chuo zitokeapo tofauti kati ya serikali na wanafunzi, reason tu waziri kasema chuo kifungwe.

  mimi nashangaa nani kamteua kuwa CEO wa hiyo tume, the guy pamoja na kuwa Prof has got nothing onto his scurs-------scurs are empty
   
 10. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Sasa nimekubali kama anavyosema mwandishi mmoja wa vitabu, Robert Kiyosaki kwamba, kuwa na elimu hata iwe kubwa vipi haimanishi kwamba ndo utakuwa bingwa kutatua challenges!
   
 11. Companero

  Companero Platinum Member

  #11
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,491
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 160
  Arudi chuoni kufundisha - huko ndio kunamfaa mtu unayedai ame"underperformed"?
   
 12. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Huyu Mayunga ni president appointee,kwa hiyo hawezi kumwangusha rais.Mawaziri wenye fake Phd ni kipenzi cha rais!Ndio tatizo la katiba yetu.Kungekuwa na mfumo wa kwamba mawaziri wote wakuwa confirmed na Kamati za Bunge ,tatizo zimejazwa na wana SISIEM.Kamati hizi ni kuangalia CV na kuhoji kwa kina.Kwa mfano Mkulo ana MBA ya kuhoji,Kamati ya Cheyo ilitakiwa kufanya uchunguzi na kusema kuwa je:katika nchi yetu tunatakiwa na waziri wa fedha kuwa na mediocre MBA ?

  Jamani tumekwisha,Msemakweli amechukua bold decision,nimeona kuna thread hapa inamkanda,lakini tuna stupid people hapa JF,ambao wako kwenye system hawataki Ukweli.

  Nilikuwa na thread ya Dr Magufuli kuhoji Phd yake ya miaka 3 ,wakati ni full time Cabinet minister,nimeshangaa kuona watu hawataki kuelewa mantiki .JE NI KWELI SUPERVISOR WAKE ALIKUWA NKUNYA?hebu wanaojua semeni ukweli
   
 13. M

  Mtoto wa jiji Member

  #13
  Feb 12, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yule msomi feki wa Sheria asiyeweza hata kuandika kiswahili na kiingereza vizuri Kainerugaba ameshushuliwa na TCU!

  Kainerugaba, ambaye kazi yake ni ya kiwano cha mtoto was form II, ameambiwa hana competence ya verify vyeti vya watu!

  Hii imekuja baada ya Spika kumsafisha Dr Mathayo.

  Kainerugaba alikurupuka sijui alitumwa na mtandao wa maharamia, mafisadi wanaotaka kuharibia watu kwenye uchaguzi? Nalaumu vyombo vya habari vilivyompa air time huyu mpuuzi.
   
 14. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  asa umetoa mwitiko wako towards the kasheshe lakini nini kilichojiri; binafis cjakupata
   
 15. Kichwa

  Kichwa Senior Member

  #15
  Feb 12, 2010
  Joined: Mar 15, 2007
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wewe ndio unakurupuka acha ushabiki wa kijinga jinga,

  Hembu rudia ulichoandika uone sentence zako zilivyoungwa ungwa.

  tatizo letu watz tunapenda sana kuona makosa kuliko sifa ya mhusika hata kama hayapo.
   
 16. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #16
  Feb 12, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 747
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mbona umekurupuka?.
   
 17. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #17
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,935
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Wahi shule wewe mtoto wa jiji.Acha kulialia.Shauri yako.mtegemea cha nduguye hufa masikini.subiri TCU ikutee badala ya kujikomboa,vijana wanakuja kwa kasi ya ajabu na utashangaa unavyozidiwa kete.
   
 18. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #18
  Feb 12, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  Huo ni mchango wake ametoa kwa taifa wa kwako uko wapi???na hao TCU walikuwa wapi?
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Waw, full comedy hapa.

  1. Kwa hiyo aliyoyasema Msemakweli hayawi na ukweli mpaka yeye mwenyewe awe msomi??

  2. Kwa hiyo kumbe Spika ndio anagawa PhD siku hizi ??
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,018
  Likes Received: 6,831
  Trophy Points: 280
  Jamani nimepatwa na mshtuko na mzee wetu huyu ambae
  watu wengi wanampenda na kumheshimu tangu akiwa
  udsm;nashangaa vipi leo hii awe mstari wa mbele kutetea
  vihiyo wa elimu;je akuhsika kupitisha wanafunzi feki huyu
  akiwa udsm
  nimepatwa na woga hata elimu yake mwenye nafasi atusaidie
  pamoja na kwamba yuko tcu tunaweza kutafuta uhalisi wa
  prof yake
  alunta kontinyua
  vihiyo wa elimu wajitokeze sasa kuhakiki elimu zao
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...