mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,767
- 7,115
Wana JF,
Tanzania ni nchi yenye wanafunzi wanaosoma masomo mengi na mabovu, kwani hayana malengo thabiti ya kuiweka tanzania katika mikono salama ya sayansi na teknolojia. tangu kuanza kwa masomo ya awali unakuta watoto wanaingizwa kichwani vitu vilivyowazidi na wanakuwa wanavirudia kutokana na kupanda kwao daraja wanapokuwa masomoni. Hakika watanzania tunao mkwamo wa kutoangalia talent za vijana wetu kujua wanaweza nini ndicho tuwafundishe.
Ukiangalia kwa makini, sehemu nyingi ya watu waliosomea veta ndio wanaosukuma gurudumu la maendeleo kuliko waliosoama vyuo vikuu kwani wengi wako na makaburasha wanaangaika kupata ajira za waliopunguzwa serikalini au walikufa, au waliostaafu.
Hawa vijana mpaka wanapata ajira wanakuwa wameshachoka sana, umri unakuwa umewapita, kazi wanazifanya kwa uoga ufanisi hakuna kwa kuwa wanawaza kuwa na vitu walivyovikosa, wakiwa wanaangaikia ajira. ndio maana wengi wanakosa uadirifu wanakuwa wezi kweli kweli.
Tufike hatua kama mtu amepata maksi nzuri badala kwenda form five na Six, aende chuo kikuu chochote na waliopata maksi za kawaida basi waingie veta. kwa wale waliona wamefeli sana wanatakiwa kurudia hili wapate nafasi za veta hawa ndiowarudie mitiani kufuzu kuingia vyuo vya veta.
Hukovetawatakaofaulu vizuri ndio waingie chuo kikuu. hii itasaidia watu wengi kupata ujuzi wa kitu chochote cha kumwingizia riziki hata kama baadaye anataka kazi nyingine, angalalau anakuwa maeishazalisha kitu. hapa lazima tuwe na maendeleo.
Angalia wimbi la bodaboda , kuna mafundi wengi huko kama kungekuwepo mitaala mizuri wengi wangekua mashuleni wakijifunza stadi za kazi, badala yake, hawa ndio wengi wako mhimbili hawa mikono, hawana miguu, wengine wanaugulia kujaa maji vifuani.
Bodaboda ni ajira ya vipo hakuna mbadala. tufike hatua tutumie mawazo ya Profesa Kamzora kwa utafiti wake alioufanya kupitia jamii ya wahindi. Wahindi wengi hawapo mavyuoni wengi hawafiki kidato cha sita, wanacheza na fursa, halafu ndio wanaokuja kuongoza kwenye vitu vya kisayansi kwa sababu wamebobea kwenye masomo machache yenye tija, wanayachagua kwa uwezo walionao sio kwa kulazimika na hali uliyonayo.
======
Prof Kamuzora RAS Kagera:
Tatizo lile lile nililolisema awali. Falsafa ya Elimu yetu ni kuwa watu wanasomea taifa na si kusomea maisha yao. Hivyo, wote mnaingizwa kwenye behewa kuelekea kwenye combinations ambazo Taifa limechagua yaani PCM, PCB, PGM, CBG, CBN, ECA, EGM, HGL, HGE, HGK. Ukikosa nafasi kwenye behewa sasa ndio ukatafute hizo fursa zingine za NACTE na VETA.
Falsafa hii na mfumo huu una athari za kisaikolojia. Kwanza unafanywa watu wakikosa nafasi kwenye behewa la form five wajione kuwa ni watu waliofeli na waliopoteza ndoto za maisha. Pili, inafanya elimu ya NACTE na VETA kuonekana kama ni sitara na hifadhi kwa waliokosa nafasi behewani. Matokeo yake, tunapeleka huko kwenye NACTE na VETA waliopoteza matumaini. Yaani tumegeuza NACTE na VETA kuwa ni elimu mbadala na si chaguo tu kama kwenda form 5.
Katika hili nitapenda kutoa mfano wa jamii ya watanzania wenye asili ya asia. Hivi hawa wanaishiaga wapi? Mbona wengi hawaendi form 5 na hata wanaoenda hawasomi HGL, HGK na HGE bali utawakuta aidha kwenye PCB, PCM na ECA na EGM? Na je mbona huko chuo hawaonekani kwenye vitivo vya Sheria, Sayansi ya Siasa, Sociolojia na Historia na Archaeology? Mbona ni kama hawapo kabisa kwenye Masters degree zinazotolewa na Chuo Kikuu kipendwa cha UDSM na pia hawapatikani kule kwenye Masters za jioni za Mzumbe wala zile za Open University? Lakini mbona pamoja na kutowaona huko kote hatuwaoni mtaani wakipita na bahasha za khaki zenye photocopy za vyeti na barua za kuomba ajira?
Wenzetu hawa walishajinasua siku nyingi katika mtego wa fikra tuliouingia wa kusomeshea watoto kwenda kujaza nafasi za wanaostaafu na kufa katika sekta ya umma. Wenzetu wanajifunza stadi zaidi. Anayetaka uhasibu, akifika form four anajisajili kwenye mitihani ya Bodi za Uhasibu (NBAA na ACCA) anaendelea huko. Wengine watakwenda kujifunza masuala ya kukatisha tiketi za ndege IATA system, wengine watakwenda kujifunza stadi za Hardware na Software Engineering na stadi nyingine nyingine. Wengine watasomea u-pilot, wengine insurances nk. Leo nenda kwenye nursery schools walimu wengi ni watanzania waasia kwa kuwa wanakwenda kusomea fani hiyo. Kwao behewa la form 5 ni moja tu kati ya mabehewa mengine na si behewa takatifu au la wateule.
Wenzangu na sisi tunakwenda na behewa, tunaingia chuo tunapigwa sumu ya DS 101 tunakuwa wanamapinduzi na wachukia mabeberu huku tukisoma archaeology, Sociology, Political Science na Kiswahili mwisho wa siku tunasubiri Sekretariati ya Ajira itangaze kazi tunajikuta inaajiri asilimia 10 tu ya waliomaliza chuo. Mwishowe hao hao wasomi wanarudi kuajriwa na mabepari waliokuwa wanawachukia wakiwa chuo🤣🤣🤣🤣🤣.
Kuna kitu tunakosea mahala.
Credit to profesa Kamuzora