Prof. Lipumba aula!!

watanzania hatuangalii nani kafanya nini, tunaangalia nani yuko wapi na anapata sh./dolar ngapi kwa mwezi. huu ni udhaifu
 
Mkapa siku zote alikuwa anamwita profesa uchwala.
,

Wahenga walisema "asiekujua hakuthamini" leo huyoooo.... yeye Mkapa lipi kubwa alolifanya kabla hajawa Rais na mpaka alipokuwa Rais mpaka sasa zaidi ya kutukwibia mali zetu walalahoi! na KUJILIMBIKIZIA MALI ! kutesa kwa zamu ! amwache profesa nae atese !... Kila la Kheri Professor
 
Nadhani umewadia wakati sasa wa kuandika makala ya The rise and fall of C U F .... sijui kama kitakuwa kwenye medani za kisiasa huku bara ! na ni wazi Professor yupo kimya sana muda mwingi sasa... bora ibaki CCM iwe chama tishio cha wakati wote ...CCM juu zaidi !
 
tuweke taaluma pembeni na siasa, prof lipumba ktk fani ya uchumi ni mtaalam kamili hata kama tunatofautiana ktk itikadi za vyama he has done far commendable jobs all over the world ingawa issue apa iwe kua mtaalam wa fani fulani sio lazima uwe president mzuri lakini sio kubeza taaluma, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni! yeye ni prof hata PHD yake sio ya heshima kama hizi wanazogaina kama njugu mara dokta kikwete cjui mara dokta karume etc
 
Nabii hakubaliki kwao.....! Nlitegemea hata kwenye salaam za mwisho wa mwaka 2011 Rais JK angempongeza kama Rais maana Professors kutoka nchini mwake ameula maisha katika Bodi ya Uchumu wa Dunia !
 
Akirudi bongo atakuwa anaingiza dollar ngapi kwa wiki?
Bongo mshahara kwa mwezi ni laki 6 mpk mil 1. 10% (ten percent ni tsh 12,000,000), Mikataba feki ni $990,000,000 hizo ni dollar kwa mwaka. CHANGANYA NA ZAKO.
 
Igwe, unajua kuwa concept ya management agencies ni brain child ya Prof Lipumba? Aliwaambia Mwinyi na Kigoma Malima (Malima akiwa waziri wa fedha nae akiwa mshauri wa uchumi) kuwa income tax department iwe independent wakamuona juha. Museveni alipomchukua at the same capacity na aka implement concept hiyo Uganda na performance ya URA ikawa bomba tukalazimishwa na world bank kufuata model hiyo hiyo!

Kubali usikubali, Prof ni kichwa japo si politician.

O.K_mkuu,nakubali. My bad,i take it back.
 
mshahara mdogo sana huo kwa cheo chake hico bora arudi bongo tu
Hata Nehemia wa NHC amemzidi huo mshahara wa meneja wa benk bana,tena benki ya kawaida sana tena benki iliyopo bongo,huenda Prof ameamua ajitolee na hiyo huenda ni allowance ya kukaa(kama ile ya wabunge)
 
Kaifanyia nini Tanzania na hicho kichwa chake?

Ndugu zangu tumshukuru Mungu kwa kumpa ndugu yetu hiyo nafasi kwakuwa nasi tutaambuliapo sifa, kuhusu kuifanyia kitu Tanzania siyo lazima ajenge barabara ndiyo tujuwe kuwa kafanya kitu. yeye hakuwa kwenye nafasi ambayo angeweza kuonyesha kile ambacho alikusudia kutufanyia. Ingekuwa busala kama tungempa nafasi halafu ndiyo tuseme hajatimiza yale tuliyompa atekeleze. labda kama kuna majukumu tuliyompa hakuweza kuyatimiza mnaweza kutujuza!. Mbarikiwe sana!
 
Mmmh_na hili ndilo tatizo letu,mtu unamsifu kichwa wakati hajafanya lolote la maana kwao(tz),....haya kila la heri huko kwenye hiyo bodi ya dunia.

Pengine anakuwa hahitajiki. Wanaomhitaji ni kama hao waliomchukua. Mtu hawezi kuwa anapewa kazi kubwa kwenye international /worldwide reputable organisations na wakati huo huo kwenye chi yake hajafanya kitu, je ni kwamba anakuwa hataki? Kama sivyo tatizo linakuwa ni nini? Obvious anakuwa hahitajiki!
 
Back
Top Bottom