Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
Mhadhiri Mwanadamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mjumbe wa zamani wa Tume ya Marekebisho ya Katiba,Prof. Palamaganda John Aidan Mwaluko Kabudi amesema kuwa kama Serikali mbili zitapita,Serikali hizo hazitakuwa imara kuulinda Muungano. Prof.Kabudi amesema hayo leo katika Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Hayati Dr.C.Mkoyogo aliyekuwa mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Ruaha Iringa almaarufu kama RUCO.
Prof. Kabudi alikuwa akiwasilisha mada katika Kumbukumbu hiyo. Alisema ya kwamba Wajumbe wa Bunge la Katiba walipaswa kuisoma vyema Rasimu ya Katiba mpya kwakuwa imelenga katika kuulinda Muungano na si kuuvunja kama inavyotafsiriwa na baadhi ya Wajumbe. Prof.Kabudi alisisitiza kuwa Wajumbe walipaswa kuisoma Rasimu katika ujumla wake kabla ya kuijadili.
Chanzo: Radio One Stereo,Taarifa ya HABARI