Konseli Mkuu Andrew
JF-Expert Member
- May 10, 2013
- 740
- 855
Salaam wakuu.
Ibara ya 11(2) ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inatamka kama ifuatavyo;
"Kila mtu anayo haki ya kujielimisha, na kila raia
atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia
upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake"
Hali ni tofauti kwa wafungwa wanaotumikia vifungo katika magereza yetu hapa Tanzania, kwani hakuna fursa ya kutafuta elimu katika fani aipendayo hadi kufikia upeo wowote, inaonekana ukifungwa basi ndio unapoteza haki zote za kibanadamu kama vile kupiga kura katika chaguzi mbali mbali na haki ya kupata elimu.
Pia vipo vyuo hapa Tanzania ambavyo vipo chini ya usimamizi wa TCU ambavyo vina sheria ngumu kwa wanafunzi walikutwa na hatia na mahakama adhabu yao ni kufutiwa masomo.
Naishauri serikali sasa ianze kuwapa fursa wafungwa nao kupata haki ya kupata elimu katika viwango mbali mbali vya kielimu.Mfano unakuta mtu alikuwa yupo chuo kikuu mwaka wa nne na kwa bahati mbaya akifungwa kifungo hata cha miaka minne tuu , hapo ndio basi suala la shule linakuwa limeisha, kiasi kwamba akija kutoka anaanza upya na si wote wanaoweza kukabiliana na hali hiyo.
Pia kama ikiwapendeza naomba Ibara hii ya 11 iingine katika sehemu ya III ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inazungumzia Haki na Wajibu muhimu.
KUWA MFUNGWA KUSIMZUIE MTU KUPATA HAKI YA KIELIMU