Prof.Kabudi: Serikali mbili hazitakuwa imara kulinda Muungano

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,484
2,000
Mhadhiri Mwanadamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mjumbe wa zamani wa Tume ya Marekebisho ya Katiba,Prof. Palamaganda John Aidan Mwaluko Kabudi amesema kuwa kama Serikali mbili zitapita,Serikali hizo hazitakuwa imara kuulinda Muungano. Prof.Kabudi amesema hayo leo katika Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Hayati Dr.C.Mkoyogo aliyekuwa mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Ruaha Iringa almaarufu kama RUCO.

Prof. Kabudi alikuwa akiwasilisha mada katika Kumbukumbu hiyo. Alisema ya kwamba Wajumbe wa Bunge la Katiba walipaswa kuisoma vyema Rasimu ya Katiba mpya kwakuwa imelenga katika kuulinda Muungano na si kuuvunja kama inavyotafsiriwa na baadhi ya Wajumbe. Prof.Kabudi alisisitiza kuwa Wajumbe walipaswa kuisoma Rasimu katika ujumla wake kabla ya kuijadili.

Chanzo: Radio One Stereo,Taarifa ya HABARI
 
MFUKUZI

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
934
1,000
Ukitafakari kwa kina ni mtu mmoja au wawili tu ndani ya CCM ndiyo wanayumbisha mstakabali wa taifa .... Wanahonga watu ili mfumo uliopo uendelee kwa lengo la kulinda maslahi yao...
 
Fukara

JF-Expert Member
Dec 28, 2013
1,516
2,000
kweli kabisa mdau,yani ni watu wachache tu wenye uchu wa madaraka na tamaa za mali ndio wanatuvurugia nchi yetu,kitu ambacho hatuwezi kukubali.haiwezekani hao watu wachache walete katiba waitakayo wao.hatutakubali kamwe
 
makubazi

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
2,048
1,195
Ooyooo hata kule nyuma wakati tunataka vyama vingi vije basi palikuwa na makelele utasema nchi hii inataka kuuzama na leo ni yale yale na haya yote ni masilai kwa vigogo tena wala hakuna kigogo hata mmoja mwenye uchungu na hii inchi na wananchiwake ni kukomba tu na kuwekeza ulaya na hii kitu inauma sana
 
ndenga

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
1,761
2,000
Hili somo linafaa limfikie na msomi mwenzake lakini msomi uchwara Dr Francis Michael..
 
ihs

Member
Jul 24, 2012
93
0
Nafikiri Prof kabudi anamfundisha Dr. Feki mwakyembe kujua nini maana ya kuitwa msomi,msomi sio veyti kama mwakyembe anavyodhani. Usomi ni tija kwa Taifa lako na ukweli wa kisayansi uliotukuka, najua Mwakyembe analijua hilo ila unafiki na umalaya wa fedha na madaraka umemwondolea heshima.

Hongera Prof wa ukweli, kabudi
 
bendaki

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
954
250
Kuna wasomi wengi ccm na wale mengine waliobaki Bunge la Katiba kama akina Lukuvi,Nchemba, Wasira, komba, maji marefu, rage, dewji, abood, Dr. Kigwangalla, Mhagama, injinia manyanya, sendeka anayelia kwa ajili ya serikali mbili, yule kipofu jina nimesahau na Kingunge, wote ujumbe uwafikie. Profesa Kabuda ameonyesha busara ya kwa vipi wewe kusoma mstari mmoja ukawa mjuvi wa biblia au koran takatifu? Na kesho yake ukahubiri kuliko padri au sheikh? Sijui akina Tibaijuka, Migiro, Kapuya, nk watatoka kuuonyesha uporofesa wao au ndio ile ukiisha shabikia ccm sharti ukae kizuzu zuzu? wanajisikiaje? Waitwe wajumbe wa tume wawafafanulie wabunge wetu ili rasmu ya katiba ieleweke na tupate katiba bora.
 
Communist

JF-Expert Member
Jun 1, 2012
5,392
2,000
Nafikiri Prof kabudi anamfundisha Dr. Feki mwakyembe kujua nini maana ya kuitwa msomi,msomi sio veyti kama mwakyembe anavyodhani. Usomi ni tija kwa Taifa lako na ukweli wa kisayansi uliotukuka, najua Mwakyembe analijua hilo ila unafiki na umalaya wa fedha na madaraka umemwondolea heshima.

Hongera Prof wa ukweli, kabudi
Mwakyembe ni Dk , na huyu ni Prof. Ujue maana yake. Mwakyembe anajikomba tu. Kumbe hafai hata kuwa waziri.
 
OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,976
2,000
Mhadhiri Mwanadamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mjumbe wa zamani wa Tume ya Marekebisho ya Katiba,Prof. Palamaganda John Aidan Mwaluko Kabudi amesema kuwa kama Serikali mbili zitapita,Serikali hizo hazitakuwa imara kuulinda Muungano. Prof.Kabudi amesema hayo leo katika Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Hayati Dr.C.Mkoyogo aliyekuwa mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Ruaha Iringa almaarufu kama RUCO.

Prof. Kabudi alikuwa akiwasilisha mada katika Kumbukumbu hiyo. Alisema ya kwamba Wajumbe wa Bunge la Katiba walipaswa kuisoma vyema Rasimu ya Katiba mpya kwakuwa imelenga katika kuulinda Muungano na si kuuvunja kama inavyotafsiriwa na baadhi ya Wajumbe. Prof.Kabudi alisisitiza kuwa Wajumbe walipaswa kuisoma Rasimu katika ujumla wake kabla ya kuijadili.

Chanzo: Radio One Stereo,Taarifa ya HABARI
Kama serikali mbili zitapita kutoka wapi? Kwenye rasimu hakuna serikali mbili zipo tatu hivo anayezungumzia serikali mbili kwenye hii Rasimu ya pili au ni mwenda wazimu au mlevi tuu wa kawaida!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom